Kikotoo cha Kutengwa na Karantini

Kutengwa na Karantini ya COVID-19: Idara ya Afya katika Jimbo la Washington (Kiingereza pekee)

Tafadhali tazama yanayofuata kuhusu jinsi ya kupiga hesabu ya kipindi chako cha kujitenga au karantini. Kwa maelezo zaidi kuhusu jambo la kufanya wakati wa kujitenga, tazama Jambo la kufanya iwapo utapatikana na maambukizo ya COVID-19 (PDF). Kwa maelezo zaidi kuhusu jambo la kufanya iwapo wewe ni mwasiliani wa karibu wa mtu aliyeambukizwa COVID-19, tafadhali tazama Jambo la kufanya ikiwa huenda ulikuwa na mfiduo na mtu aliye na COVID-19 (PDF).

Iwapo una kingamwiili dhaifu au ulikuwa umeugua COVID-19 sana, hesabu hizi huenda hazitumiki katika hali yako. Tafadhali tazama Jambo la kufanya iwapo utapatikana na maambukizo ya COVID-19 (PDF) kwa maelezo zaidi.

Iwapo unaishi au kufanya kazi katika mazingira yenye hatari ya juu hesabu hizi huenda hazitumiki katika hali yako. Mazingira yenye hatari ya juu yanajumuisha: vituo vya afya, vituo vya marekebisho, vituo vya wafungwa, makao ya wasio na numba, nyumba ya mpito, mazingira ya kibiashara ya bandarini (mfano, chombo cha kibiashara cha samaki, meli ya mzigo, meli ya usafiri), nyumba ya muda ya mfanyakazi, au vituo vya kazi vyenye umati mkubwa ambapo kukaa mbali na wengine hakuwezekani kwa sababu ya hali ya kazi (k.m, katika maghala, viwanda, na vituo vya uwekaji chakula kwenye mikebe na usindikaji wa nyama). Tafadhali tazama Jambo la kufanya iwapo utapatikana na maambukizo ya COVID-19 (PDF) kwa maelezo zaidi kuhusu kipindi chako cha kujitenga na Jambo la kufanya ikiwa huenda ulikuwa na mfiduo na mtu aliye na COVID-19 (PDF) kwa maelezo zaidi kuhusu kipindi cha karantini.

Nilipatikana na maambukizo na nina au nilikuwa na dalili: piga hesabu ya kipindi changu cha kutengwa

Kujitenga kwa Siku 5

Kipindi cha kujitenga kwa siku 5 kinatumika iwapo:

  • Dalili zako zimeanza kupotea, NA
  • Saa 24 zimepita tangu ulipokuwa au homa na umetumia dawa ya kupunguza homa, NA
  • Unaweza kuvaa barakoa inayokutoshea vizuri ukiwa karibu na wengine

Ikiwa vigezo hivi vinatumika, siku yako KAMILI ya mwisho ya kujitenga ni:
Kujitenga kwako KUTAISHA:

Hakikisha umevaa barakoa ukiwa karibu na watu wengine kwa siku 5 zaidi (until ) na uepukane na shughuli ambazo huwezi kuvaa barakoa. Pia unafaa kuepuka kuwa karibu na watu wengine walio katika hatari ya juu hadi . Tazama Usafiri | CDC (Kiingereza pekee) ili kupata taarifa kuhusu usafiri.

Iwapo una ufikiaji wa kipimo cha antijeni, unaweza kupunguza zaidi hatari yako ya kuwaambukiza wengine kwa kujipima siku ya 5 ya kujitenga. Iwapo kipimo chako kinaonyesha huna maambukizo, unaweza kutamatisha kujitenga baada ya siku 5, lakini uendelee kuvaa barakoa ukiwa karibu na watu wengine kwa siku 5 zaidi (hadi ). Iwapo matokeo yako ya kipimo yanaonyesha kuwa umeambukizwa, unafaa kuendelea kujitenga hadi .

Kujitenga kwa Siku 10

Iwapo kigezo kilicho hapo juu hakitumiki kwako, basi unafaa kujitenga kwa siku 10.

Ikiwa unajitenga kwa siku 10, siku yako KAMILI ya mwisho ya kujitenga ni:
Kujitenga kwako KUTAISHA:

Iwapo dalili zako hazijapotea au ukiendelea kuwa na homa (au unahitaji dawa za kupunguza homa) mnamo , subiri ili kutamatisha kujitenga kwako hadi dalili zako zitakapoanza kuisha na hujakuwa na homa kwa saa 24 bila kutumia dawa za kupunguza homa.

Nilipatikana na maambukizo lakini kamwe sijakuwa na dalili zozote: piga hesabu ya kipindi changu cha kutengwa

Kujitenga kwa Siku 5

Kipindi cha kujitenga kwa siku 5 kinatumika iwapo:

  • Unaweza kuvaa barakoa inayokutoshea vizuri ukiwa karibu na wengine

Iwapo kamwe hujakuwa na dalili zozote na unaweza kuvaa barakoa inayokutoshea vizuri ukiwa karibu na wengine, siku yako KAMILI ya mwisho ni:
Kujitenga kwako KUTAISHA:

Hakikisha umevaa barakoa ukiwa karibu na watu wengine kwa siku 5 zaidi (until ) na uepukane na shughuli ambazo huwezi kuvaa barakoa. Pia unafaa kuepuka kuwa karibu na watu wengine walio katika hatari ya juu hadi . Tazama Usafiri | CDC (Kiingereza pekee) ili kupata taarifa kuhusu usafiri.

Iwapo una ufikiaji wa kipimo cha antijeni, unaweza kupunguza zaidi hatari yako ya kuwaambukiza wengine kwa kujipima siku ya 5 ya kujitenga. Iwapo kipimo chako kinaonyesha huna maambukizo, unaweza kutamatisha kujitenga baada ya siku 5, lakini uendelee kuvaa barakoa ukiwa karibu na watu wengine kwa siku 5 zaidi (hadi ). Iwapo matokeo yako ya kipimo yanaonyesha kuwa umeambukizwa, unafaa kuendelea kujitenga hadi .

Kujitenga kwa Siku 10

Iwapo kigezo kilicho hapo juu hakitumiki kwako, basi unafaa kujitenga kwa siku 10.

Ikiwa unajitenga kwa siku 10, siku yako KAMILI ya mwisho ya kujitenga ni:
Kujitenga kwako KUTAISHA:

Nilikuwa wazi kwa maambukizo ya COVID-19 (inayotambuliwa kama mwasilani wa karibu): piga hesabu ya kipindi changu cha karantini

Ulikuwa karibu sana na mtu ambaye alipatikana na maambukizo ya COVID-19, lakini huna dalili zozote.

Angalia mwongozo wa Centers for Disease Control and Prevention (CDC, Kituo cha Uzuiaji na Udhibiti wa Ugonjwa) (Kiingereza pekee) ili kujua iwapo umepokea chanjo zote za COVID-19 Iwapo hujapokea chanjo zote za COVID-19, unafaa kukaa nyumbani na kuingia karantini.

Karantini ya Siku 5

Kipindi cha karantini ya siku 5 kinatumika iwapo:

  • Hujapokea chanjo zote za COVID-19, NA
  • Unaweza kuvaa barakoa inayokutoshea vizuri ukiwa karibu na wengine

Unafaa kukaa nyumbani na kuingia karantini kwa angalau siku 5 kamili (hata kama umepatikana kuwa huna maambukizo katika kipindi hiki). Siku yako KAMILI ya mwisho katika Karantini ni:
Karantini yako ITAISHA tarehe:

Vaa barakoa inayokutoshea vizuri (Kiingereza pekee) ukiwa karibu na watu wengine, epukana na shughuli ambapo huwezi kuvaa barakoa, na kuepukana na kuwa karibu na watu walioko katika hatari ya juu ya ugonjwa mkali kwa siku 5 zaidi (hadi ) na kuepukana na shughuli ambapo huwezi kuvaa barakoa. Tazama Usafiri | CDC (Kiingereza pekee) kwa maelezo zaidi kuhusu usafiri.

Pia unafaa kupimwa, hata kama huna dalili zozote. Pata kupimwa angalau siku 5 baada ya mtagusano wako wa mwisho wa karibu zaidi na mtu aliye na COVID-19 (tarehe au baada ya tarehe ). Kipimo kikionyesha kuwa una maambukizo, unafaa kukaa nyumbani na kujitenga mbali na wengine (kwa maelezo zaidi kuhusu kujitenga, tafadhali tazama Jambo la kufanya iwapo utapatikana na maambukizo ya COVID-19 (PDF)).

Karantini ya Siku 10

Kipindi cha karantini ya siku 10 kinatumika iwapo:

  • Hujapokea chanjo zote za COVID-19, NA
  • Huwezi kuvaa barakoa inayokutoshea vizuri ukiwa karibu na wengine

Unafaa kukaa nyumbani na kuingia karantini kwa angalau siku 10 kamili (hata kama umepatikana kuwa huna maambukizo katika kipindi hiki). Siku yako KAMILI ya mwisho katika Karantini ni:
Karantini yako ITAISHA tarehe:

Mnamo tarehe hii, unaweza kurejea shughuli zako za kawaida lakini bado unafaa kuchukua hatua za kupunguza hatari yako (kwa mfano, pata chanjo zote (Kiingereza pekee) za COVID-19, vaa barakoa kwakufuata mapendekezo na/au mahitaji, epukana na nafasi zisizo na mzunguko mzuri wa hewa, na kunawa mikono yako mara kwa mara; tazama Jinsi ya Kujikinga na Kuwakinga Wengine | CDC (Kiingereza pekee) kwa maelezo zaidi).

Hakuna Karantini

Iwapo umepokea chanjo zote (Kiingereza pekee) za COVID-19, huhitaji kukaa nyumbani isipokuwa ukiwa na dalili. Bado unafaa kuvaa barakoa inayokutoshea vizuri ukiwa karibu na wengine hadi na kupimwa, hata kama huna dalili zozote. Pata kupimwa angalau siku 5 baada ya mtagusano wako wa mwisho wa karibu zaidi na mtu aliye na COVID-19 (tarehe au baada ya tarehe ).

Iwapo ulikuwa umeambukizwa COVID-19 ndani ya siku 90 zilizopita (ulijipima kwa kutumia kipimo cha virusi (Kiingereza pekee)), huhitaji kukaa nyumbani isipokuwa ukiwa na dalili. Bado unafaa kuvaa barakoa inayokutoshea vizuri ukiwa karibu na watu wengine hadi na kupimwa kwa kutumia kipimo cha antijeni (si kipimo cha PCR) angalau siku 5 baada ya mtagusano wako wa mwisho wa karibu zaidi na mtu aliye na COVID-19 (tarehe au baada ya tarehe ).

Iwapo ulikuwa katika mgusano wa karibu na mtu aliemabukizwa COVID-19 na una dalili, tafadhali tazama Jambo la kufanya ikiwa huenda ulikuwa na mfiduo na mtu aliye na COVID-19 (PDF).