Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara | Kipimo cha COVID-19

Kufikia vifaa vya kipimo

Je, naweza kupata wapi chanjo ya COVID-19?

Tafadhali jaribu chaguo zifuatazo:

 • Huku bado kukiwa na usambazaji, agiza kifaa cha kipimo cha bila malipo kutoka kwa Sema Ndiyo! Kipimo cha COVID (katika Kiingereza) au piga 1-800-525-0127 na kubonyeza # ili kufikia usaidizi wa lugha. Weka kikwazo cha agizo moja kwa kila kaya.
 • Agiza kifaa cha bila malipo cha kipimo kutoka mpango wa Shirikisho kupitia COVIDTests.gov (katika Kiingereza) Weka kikwazo cha agizo moja kwa kila kaya.
 • Nunua kifaa cha kujipima nyumbani katika wauzaji rejareja na famasia.
 • Iwapo una bima ya afya, watoaji bima wengi sasa watakulipa kwa hadi vipimo 8 vya nyumbani kila mwezi, kwa kila mtu kwenye mpango wako. Soma maelezo zaidi hapa (katika Kiingereza).
 • Pata kipimo katika Eneo la Kipimo karibu nawe (katika Kiingereza).

Ikiwa unahitaji usaidizi wa kupata kituo cha kipimo karibu nawe, angalia na idara au wilaya yako ya afya ya ndani (katika Kiingereza). Unaweza pia kupiga 1-800-525-0127 na kubonyeza #. Wakipokea, sema lugha yako ili kufikia huduma za ukalimani.

Sina ufikiaji wa intaneti / Tovuti haipatikani katika lugha yangu. Nawezaje kuagiza kifaa cha bila malipo katika WA?

Tafadhali piga 1-800-525-0127, kisha ubonyeze #. Usaidizi wa lugha unapatikana. Kituo cha simu kinaweza kuagiza kwa niaba yako kupitia vituo vya mtandaoni vya WA na shirikisho.

Nahitaji kujua nini ilikuhusu Sema Ndiyo! Kipimo cha COVID cha kituo cha mtandaoni?

Mpango huu ni juhudi ya ushirikiano kati ya Jimbo la Washington, National Institutes of Health (Taasisi ya Kitaifa ya Afya), na Centers for Disease Control and Prevention (Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Ugonjwa). Huku bado kukiwa na vifaa, watu katika Washington wanaweza kuagiza vifaa viwili vya kipimo cha haraka cha COVID-19, na kutumwa moja kwa moja hadi nyumbani mwao na Amazon.

Ni maagizo mawili tu ndiyo yanaweza kufanywa kwa kila kaya/anwani ya makao, kwa mwezi, na kila agizo huja kwa vipimo 5 vya haraka. Maagizo yote na usafirishaji ni wa bila malipo.

Kwa maswali yanayohusiana na kipimo chenyewe au jinsi ya kujipima, tembelea Sema Ndiyo! Kipimo cha COVID Kisaidizi cha Kidijitali au piga 1-833-784-2588.

Je, unaweza kuagiza Sema Ndiyo! Kipimo cha COVID kutoka kwa DOH na kifaa cha kipimo cha Shirikisho?

Ndiyo, iwapo unaishi katika jimbo la Washington, unaweza kuweka maagizo katika tovuti ya Sema Ndiyo! Kipimo cha COVID na katika Tovuti ya Shirikisho ili kupokea vifaa vya kujipima COVID-19 kwa haraka nyumbani.

Naweza kwenda wapi nikiwa na maswali?

Iwapo una maswali zaidi kuhusu mpango wa DOH Say Yes! (DOH wa Sema Ndiyo!) COVID Test program (Kipimo cha COVID), tembelea ukurasa wa Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara au piga simu kwa nambari ya COVID-19 ya DOH kupitia 1-800-525-0127 (usaidizi wa lugha unapatikana). Kwa maswali kuhusu mpango wa kipimo wa Shirikisho, tambelea ukurasa wao wa Maswali Yanayoulizwa Mara Kwa Mara.

Je, nitapokea vipimo vyangu vya bila malipo lini?

Vipimo vilivyoombwa kupitia programu yoyote (Say YES! (Sema NDIYO) COVID Test (Kipimo cha COVID) au Federal Program (Mpango wa Shirikisho)) vitasafirishwa kawaida ndani ya wiki 1-2 baada ya kuagiza.

Baada ya kufuata chaguo zote za kipimo zilizopendekezwa, bado siwezi kupata kipimo popote. Nafaa kufanya nini iwapo nadhani nina COVID-19?

Samahani una wakati mgumu wa kupata mahali pa kipimo cha COVID-19, tunajua usambazaji ni kiasi kwa sasa kote nchini.

Iwapo una dalili za COVID-19 au umekuwa na mfiduo wa COVID-19 na una wasiwasi kuwa huenda umeambukizwa, tunapendekeza yafuatayo:

 • Fuata mwongozo sawa wa jambo la kufanya iwapo utapatikana na maambukizo ya COVID-19.
 • Iwapo huwezi kujitenga, unafaa kufanya mambo yafuatayo:
  • Vaa barakoa inayofunika pua na mdomo wako wakati wowote ambao upo karibu na watu wengine nje ya nyumba yako (KN95, KF-94, au barakoa ya upasuaji yenye safu 3, iwapo inawezekana).
  • Kaa angalau futi 6/mita 2 mbali na watu wengine.
  • Nawa mikono yako mara kwa mara.
  • Epuka umati na mikusanyiko mikubwa ya watu.
Kuna zaidi ya watu wanne katika kaya yangu. Nawezaje kufikia vipimo vya wanachama wote wa familia yangu?
 • Unaweza kufikia vifaa viwili vya kipimo kila mwezi (kikiwemo hadi vipimo 5) kupitia tovuti ya Sema Ndiyo! Kipimo cha COVID katika Washington.
 • Unaweza kufikia vifaa viwili vya ziada vya kipimo (vinajumuisha vipimo 4) kutoka kwenye mpango wa Shirikisho kupitia COVIDtests.gov.
 • Unaweza kununua vifaa vya ziada vya kipimo cha nyumbani katika wauzaji rejareja na famasia wa ndani au mtandaoni.
 • Unaweza kupata kipimo cha PCR katika eneo la kipimo karibu nawe. Pata moja hapa.
Nitatumiaje kifaa changu cha kipimo?

Ni muhimu kufuata maelekezo ndani ya kifaa cha vipimo vya haraka nyumbani ili kupata matokeo sahihi zaidi. Wasiliana na mtengenezaji (maelezo yao yatakuwa kwenye kisanduku) ukiwa na maswali yoyote maalum.

Matokeo ya uwongo yanayoonyesha huna maambukizo yanaweza kutokea kwa vipimo vya haraka. Baadhi ya vifaa vya kipimo vinaweza kujumuisha vipimo viwili (unafaa kufuata maelekezo kwenye kisanduku ili kujua wakati wa kujipima).

Kipimo cha jumla

Nani anafaa kupimwa?

Jipime wakati unahisi wewe ni mgonjwa. COVID-19 ina masafa marefu ya dalili, hivyo iwapo huhisi vizuri, ni vyema ujipime haraka iwezekanavyo.

Pima kama umekuwa na mfiduo na mtu aliyepatikana na maambukizo ya COVID-19. Pimwa mara moja iwapo una dalili. Iwapo huna dalili, subiri kwa siku tano baada ya mfiduo na kisha upumzike.

Biashara na nafasi za tukio katika Washington zinaweza kuwa na mahitaji ya kipimo na/au chanjo kabla ya kuingia kwenye jengo au tukio. Piga simu mapema au angalia tovuti yao kabla ya kuwatembelea.

Huenda ukahitaji kujipima kabla ya na/au baada ya kusafiri. Angalia mwongozo wa hivi karibuni zaidi wa Centers for Disease Control and Prevention (CDC, Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa).

Wakati unaenda kukutana na kikundi cha watu, haswa walio katika hatari ya juu ya magonjwa makali au huenda hawajapokea chanjo zao zote za COVID-⁠19.

Ni nini itafanyika nikipatikana na maambukizo?

Fuata mwongozo wa hivi karibuni zaidi wa Centers for Disease Control and Prevention (CDC, Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa) na DOH na ujitenge nyumbani, mbali na wengine. Waasiliani wote wa karibu wanafaa kukaa karantini.

 • Kila mtu ambaye anadhani ameambukizwa au amethibitisha kuwa ana COVID-19 anafaa kukaa nyumbani na kujitenga na watu wengine kwa angalau siku 5 kamili (siku ya 0 ni siku ya kwanza ya dalili kutokea au tarehe ya siku ya kipimo kilichoonyesha kuwa umeambukizwa kwa watu wasio na dalili). Wanafaa kuvaa barakoa wakiwa karibu na wengine nyumbani na katika maeneo ya umma kwa siku 5 za ziada.
 • Iwapo mtu binafsi ana ufikiaji wa kipimo na anataka kupimwa, mtazamo bora ni kutumia kipimo cha antijeni mwishoni wa kipindi cha kujitenga cha siku 5. Kusanya sampuli ya kipimo iwapo tu huna homa kwa saa 24 bila kutumia dawa za kupunguza homa na dalili zako nyingine zimepata nafuu (kupoteza hisi ya kuonja na kunusa huenda kukaendelea kwa majuma au miezi kadhaa baada ya kupona na hili lisikufanye ucheleweshe kuacha kujitenga).
  • Iwapo matokeo yako ya kipimo yanaonyesha kuwa umeambukizwa, unafaa kuendelea kujitenga hadi siku ya 10.
  • Iwapo matokeo yako ya kipimo yanaonyesha kuwa hujaambukizwa, unaweza kuacha kujitenga na wengine, lakini uendelee kuvaa barakoa inayokutoshea vizuri ukiwa karibu na wengine nyumbani na maeneo ya umma hadi siku ya 10.

Ili kuripoti matokeo ya nyumbani ya kipimo cha COVID-19 yanayoonyesha kuwa umeambukizwa na kufikia huduma za ufikiaji, tafadhali piga Nambari ya Simu ya COVID ya Jimbo la Washington kupitia 1-800-525-0127. Usaidizi wa lugha unapatikana.

Iwapo tayari umepakua WA Notify (Arifu WA) au umeiwezesha kwenye simu yako mahiri, unaweza kutumia zana hii pia kuripoti matokeo yanayoonyesha kuwa umeambukizwa.

Maelezo zaidi yanaweza kupatikana hapa: Jambo la kufanya iwapo utaambukizwa.

Baada ya kuwa na mfiduo, mtu atapatikana na maambukizo lini?

Mara tu mtu ameambukizwa COVID-19, kipimo cha PCR huenda kisionyeshe uwepo wa virusi kwa siku tano baada ya mfiduo. Hivyo huenda una maambukizo, lakini kipimo huenda kisionyeshe kwa muda. Upimaji muda ni muhimu kwa kupata matokeo yanayoonyesha una maambukizo. Iwapo huenda ulikuwa na mfiduo wa COVID-19 lakini wewe si mgonjwa, ni bora kupimwa angalau siku 5 baada ya mfiduo wa mwisho ambao huenda ulitokea. Vipimo vya antijeni ni sahihi zaidi watu wakiwa na dalili lakini vinaweza kutumika kwa watu wasio na dalili katika baadhi ya hali.

Vipimo huchukua kipindi kipi?

Inategemea aina ya kipimo, na mahali ambapo sampuli imetumwa ili kupimwa. Matokeo ya vipimo vya antijeni vinaweza kutoka kwa haraka kama baada ya dakika 10. Kwa vipimo vya PCR, inaweza kuchukua siku kadhaa.

Kipimo kipi ni bora kutumia?

Kipimo bora ni kile kinachopatikana kwanza kwako. Hiyo inamaanisha kuwa ikiwa una kipimo cha nyumbani tayari, kitumie. Ukiona miadi inayopatikana ya kituo cha kipimo, itumie. Isipokuwa tu wakati ambapo kipimo maalum kinahitajika katika hali (kwa mfano usafiri).

Je, nafaa kuwa na akiba ya vipimo?

Ni wazo zuri la kuwa na vipimo kiasi karibu nawe. Agiza vipimo vinapopatikana kupitia tovuti za serikali. Ikiwa umeenda kufanya ununuzi na ukaona vipimo vinavyopatikana, nunua vichache. Lakini uwe jirani mzuri na kutumia uamuzi wako bora. Kuwa na vipimo kadhaa huzuia ufikiaji kwa wengine ambao huenda wanahitaji na unahatarisha kuwa na vipimo ambavyo vimeisha muda kabla ya kuweza kuvitumia.