Kujenga Imani na Kuwezesha Uwongo

Unaweza kuwa na imani katika chanjo ya COVID-19!

Neguse ni Muunganishaji wa Jumuiya wa Jiji la Seattle kwa jumuiya ya Afrika Mashariki. Neguse anazungumza Kiingereza, Kiamhari na Kitigrinya, na imekuwa sababu kuu katika kusaidia wanajumuiya wengi wa Afrika Mashariki wanaosita kupata chanjo katika Seattle Children’s Hospital.

Neguse alielezea kwamba jumuiya yake inasita kwa sababu hawajafahamu matumizi ya chanjo katika utamaduni wao, lakini watapata chanjo hiyo ikiwa mwanajumuiya anayeaminika atachukua muda ili kuwaelimisha na kuwapa usafiri wa kwenda kwenye maeneo yanayopatikana ya chanjo.

Watu wengi Marekani wanapanga kupata chanjo dhidi ya COVID-19, lakini wengine wanaweza kutaka maelezo zaidi kabla ya kupata chanjo. Hii ni kawaida kabisa. Sote tunataka kuwa na imani katika kufanya uamuzi wowote unaoathiri maisha yetu.

Ili kuwa na imani, tunahitaji maelezo kutoka kwa vyanzo vinavyoaminiwa. Saidia marafiki na familia yako kutenganisha kati ya uvumi na ukweli kuhusiana na chanjo ya COVID-19.

Unaweza kuwasaidia watu kuwa na imani zaidi katika uamuzi wao wa kupata chanjo. Unaweza kufanya hii kwa:

  • Kuchukua muda kusikiliza wasiwasi wa rafiki au mwanafamilia wako. Angalia mwongozo huu wa Kuongea kuhusu Chanjo (Kiingereza pekee) ili kupata vidokezo kuhusu jinsi ya kuwa na mazungumzo kuhusu chanjo.
  • Kujibu maswali yao. Ikiwa hujui jibu, unaweza kupendekeza waongee na mhudumu wako wa afya.
  • Ukiamua kupata chanjo, shiriki sababu za kufanya hivyo. Hadithi yako ya kibinafsi inaweza kuwa ushawishi mkubwa kwenye familia na jamii yako.

Una uwezo wa kushawishi walio karibu nawe kwa kile ambacho unasema au kufanya. Tazama vidokezo hivi kuhusu jinsi ya kuongea kuhusu chanjo za COVID-19 na marafiki na familia. (Kiingereza pekee)

Angalia ukweli wa chanjo unaofuata na uushiriki na wale unaowajua. Tumeujumuisha katika maeneo maalum ya mada.

Usalama na Ufaafu

Je, kwa nini ni muhimu nikipata au kutopata chanjo ya COVID-19?

Ni chaguo lako bila shaka kupata chanjo ya COVID-19, lakini tunawahitaji watu wengi zaidi kupata chango kadri iwezekanavyo ili kumaliza janga hili. Ni vigumu kwa virusi vya COVID-19 kusambaa wakati watu wengi katika jamii wana kingamwili - kupitia chanjo au maambukizo ya hivi karibuni. Kiwango chetu cha chanjo kikiwa juu, kiwango chetu cha maambukizo kitakuwa chini.

Watu ambao hawajapata chanjo bado wanaweza kupata virusi na kusambaza kwa wengine. Baadhi ya watu hawawezi kupata chanjo kutokana na sababu za kimatibabu, na hii huwaacha na uwezo wa kudhurika na COVID-19. Ikiwa hujapata chanjo, wewe pia uko katika hatari ya juu ya kulazwa hospitalini au kufa kutokana na aina ya COVID-19 (Kiingereza pekee). Kupata chanjo haikulindi tu wewe, bali pia inalinda familia, majirani na jamii yako.

Kwa nini nafaa kupata chanjo ya COVID-19 ikiwa watu wengi hunusurika?

Watu wengi wanaopata COVID-19 wana dalili za chini pekee. Hata hivyo, virusi haviwezi kutabiriwa kabisa, na tunajua baadhi ya aina za COVID-19 zina uwezekano mkubwa wa kukufanya mgonjwa zaidi. Baadhi ya watu wanaweza kuwa wagonjwa sana au hata kufariki kwa sababu ya COVID-19, hata watu wadogo wasio na hali za afya za muda mrefu. Wengine, wanaojulikana kama "waathiriwa wa COVID kwa muda mrefu" wanaweza kupata dalili zinazokaa kwa miezi na kuathiri ubora wa maisha yao. Pia bado hatujui athari zote za muda mrefu za COVID-19 kwani ni virusi vipya. Kupata chanjo ni ulinzi wetu bora dhidi ya virusi.

Je, chanjo hizi huwa salama au zinafanya kazi kwa kweli?

Ndiyo, chanjo za COVID-19 ziko salama na zinafanya kazi. Wanasayansi walipima chanjo hizo kwa maelfu ya washiriki katika majaribio ya kimatibabu. Chanjo zilitimiza viwango vya U.S. Food and Drug Administration (FDA, Usimamizi wa Chakula na Dawa Marekani) vya usalama, ufaafu, na ubora wa utengenezaji unaohitajika ili kupata uidhinishaji wa matumizi ya dharura. Zote zilipatikana kuwa nzuri katika kuwazuia watu dhidi ya kuwa wagonjwa wa COVID-19. Tangu hapo, chanjo hizi zimetolewa kwa mamilioni ya watu salama.

Tazama video hizi ili kujifunza zaidi kuhusu jinsi ambavyo chanjo za COVID-19 zinaundwa:

Je, chanjo hiyo ni salama kwa watoto?

Ndiyo. Chanjo ya Pfizer ilipimwa kwa maelfu ya vijana na kuonyeshwa kuwa salama. Pia ilikuwa faafu zaidi - hakuna yeyote kati ya vijana waliopata chanjo hiyo aliyepata COVID-19. Centers for Disease Control and Prevention (CDC, Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa) vinapendekeza chanjo ya COVID-19 kwa kila mtu aliye na umri wa miaka miezi 6 na zaidi.(Kiingereza pekee)

Nitaamini aje kuwa chanjo ziko salama?

Kuhakikisha kuwa chanjo za COVID-19 ni salama, Centers for Disease Control and Prevention (CDC, Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa) ilipanua na kuwezesha uwezo wa nchi wa kufuatilia usalama wa chanjo. Kwa matokeo, wataalamu wa usalama wa chanjo wanaweza kufuatilia na kugundua masuala ambayo huenda hayajaonekana wakati wa majaribio ya kimatibabu ya COVID-19.

Je, naweza kupata COVID-19 kutokana na chanjo ya COVID-19?

La, huwezi kupata COVID-19 kutokana na chanjo. Chanjo za COVID-19 hazina virusi vinavyosababisha COVID-19.

Je, nahitaji kupata chanjo iwapo tayari nilikuwa na COVID-19?

Ndiyo, bado unafaa kupata chanjo ikiwa tayari umeambukizwa COVID-19. Data inaonyesha kuwa si kawaida kuambukizwa tena na COVID-19 katika siku 90 baada ya kuambukizwa. Hiyo inamaanisha kuwa huenda una baadhi ya ulinzi wa COVID-19 (unaoitwa kingamwili asili) kwa muda mfupi. Hata hivyo, hatujui muda ambao kingamwili asilia hudumu. Jifunze zaidi kuhusu ni kwa nini bado unafaa kupata chanjo ya COVID-19.( Kiingereza pekee)

Kuna tofauti gani kati ya chanjo na kinga?

Kinga ya asili dhidi ya maambukizi hutoa kiwango fulani cha kinga dhidi ya kuambukizwa tena lakini ni muhimu kusisitiza kwamba maambukizi ya kwanza kati ya watu ambao hawajachanjwa huongeza hatari ya kupata maradhi makali, kulazwa hospitalini na kufariki. Ingawa watu wengine wanaweza kukuza kingamwili baada ya kuambukizwa COVID-19, wengine hawawezi. Kwa wale wanaokuza kinga kwa kiwango fulani baada ya kuambukizwa, hakuna njia ya kujua kiasi cha nguvu cha ulinzi huo, utaendelea kuwepo kwa muda gani au ulinzi huo unatumika kupambana na aina gani ya virusi.

Kwa sababu hatuwezi kutegemea kinga ya asili ili kuzuia kuambukizwa tena au kupata maradhi makali kutokana na COVID-19, kupata chanjo za hivi karibuni kunasalia kuwa ulinzi bora na mkakati wa msingi wa kuzuia maambukizi, matatizo yanayohusiana na usambazaji wa baadaye wa SARS-COV-2.

Afya ya Uzazi

Tutaweza kuwa na watoto nikipata chanjo ya COVID-19?

Ndiyo. Hofu zako kuhusu afya ya uzazi na chanjo zinaeleweka. Haya ndiyo tunajua: hakuna ushahidi wa kisayansi kuwa chanjo zinasababisha utasa. Chanjo ikiingia mwilini mwako, inafanya kazi na mfumo wako wa kingamwili ili kuunda kingamaradhi za kupigana na virusi vya korona. Mchakato huu hauingiliani na viungo vyako vya uzazi.

American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG, Chuo cha Marekani cha Madaktari wa Njia ya Uzazi) kinapendekeza chanjo ya COVID-19 kwa kila mtu ambaye huenda anataka kuwa mjamzito baadaye au kwa sasa ni mjamzito au ananyobyesha. Watu wengi waliopata chanjo dhidi ya COVID-19 wameweza kupata ujauzito au kuzaa watoto walio na afya.

Tazama Virusi vya korona (COVID-19), Ujauzito, na Kunyonyesha: Ujumbe wa Wateja (Kiingereza pekee) kwa maelezo zaidi.

Je, chanjo hiyo ni salama kwa wajawazito?

Ndiyo, unaweza kupata chanjo ukiwa mjamzito, na American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG) (Kiingereza pekee) inapendekeza chanjo kwa wajawazito. Hakuna ushahidi kuwa chanjo ya COVID-19 inasababisha matatizo yoyote ya ujauzito, ukuaji wa mtoto wako, uzazi, au utasa.

Tazama Virusi vya korona (COVID-19), Ujauzito, na Kunyonyesha: Ujumbe wa Wateja (Kiingereza pekee) kwa maelezo zaidi.

Je, chanjo hiyo ni salama kwa watu wanaonyonyesha?

Ndiyo, unaweza kupata chanjo iwapo unanyonyesha. Huhitaji kuacha kunyonyesha ikiwa unataka kupokea chanjo. Kwa kweli, ripoti za mapema zinapendekeza kuwa chanjo huenda ikasaidia mwili wako kupitisha kingamaradhi kwa mwili wa mtoto wako kupitia kunyonyesha. Utafiti zaidi unahitajika, lakini hii ikithibitishwa, itasaidia kulinda mtoto wako dhidi ya COVID-19.

Soma mengi kuhusu jinsi ambavyo chanjo ya COVID-19 hulinda mama na watoto wao wachanga. (Kiingereza pekee)

Je, chanjo itabadilisha mzunguko wangu wa hedhi?

Watu wengine wameripoti mabadiliko katika mizunguko yao ya hedhi baada ya kupata chanjo, lakini hakuna data yoyote kwa sasa inayopatikana ili kupendekeza kuwa haya ni athari za muda mrefu. Mizunguko ya hedhi inaweza kubadilika kwa sababu ya vitu vingi tofauti, kama msongo wa mawazo.

Viambato

Kuna viambato gani katika chanjo?

Unaweza kuona baadhi ya uvumi na viambato visivyo sahihi vikiwa vimeorodheshwa mtandaoni au kwenye mtandao wa kijamii. Huu ni uwongo wa kawaida. Viambato katika chanjo za COVID-19 chanjo (Kiingereza pekee) ni kawaida sana kwa chanjo. Zina viambato amilifu vya mRNA au virusi vya adeno vilivyorekebishwa pamoja na viambato vingine kama mafuta, chumvi, na sukari zinazolinda kiambato amilifu, kuisaidia kufanya kazi vizuri kwa mwili, na kulinda chanjo wakati wa uhifadhi na usafirishaji.

Chanjo ya COVID-19 ya Novavax ni chanjo ya kitengo kidogo cha protini iliyo na nyongeza, pamoja na mafuta na sukari za kusaidia chanjo kufanya kazi vizuri katika mwili. Chanjo hiyo haitumii mRNA.

Tazama orodha kamili za viambato katika karatasi za ukweli za Pfizer (Kiingereza pekee), Moderna (Kiingereza pekee), Novavax (Kiingereza pekee) and Johnson & Johnson.(Kiingereza pekee)

Je, chanjo ya Johnson & Johnson ina tishu ya kijusi?

Chanjo ya COVID-19 ya Johnson & Johnson iliundwa kwa kutumia teknolojia sawa na chanjo nyingine nyingi. Haina sehemu za kijusi au seli za kijusi. Kipande kimoja cha chanjo kimeundwa ndani ya nakala za seli zilizoundwa ndani ya maabara ambazo asili yao ni mimba ya kuavya iliyofanyika zaidi ya miaka 35 iliyopita. Tangu wakati huo, laini za seli kwa ajili ya chanjo hizi zimedumishwa kwenye maabara. Hakuna vyanzo zaidi vya seli za kijusi vilivyotumika kuunda chanjo hizi. Hii inaweza kuwa taarifa mpya kwa baadhi ya watu. Hata hivyo, chanjo ya tetekuwanga, surua, na homa ya manjano A, zimeundwa kwa njia sawa.

Je, chanjo zina mikrochipu

La, chanjo hazina mikrochipu au kifaa cha ufuatiliaji. Zina kiambato amilifu tu kinachosaidia mwili wako kuungda kingamwili za kupigana na COVID-19 pamoja na mafutam chumvi na Sukari.

Je, chanjo ya COVID-19 itafanya niwe na sumaku?

La, hutakuwa na safu ukipata chanjo ya COVID-19. Chanjo hazina viambato vilivyoweza kuunda uwanja wa sumaku ya elektro, na hazina chuma. Unaweza kutazama orodha kamili za viambato katika karatasi za ukweli za Pfizer, (Kiingereza pekee) Moderna, (Kiingereza pekee) and Johnson & Johnson (Kiingereza pekee) kwa maelezo zaidi

Wasiwasi wa Afya

Naweza kupata mgandano wa damu kutoka kwa chanjo?

Hatari ya kupata mgando wa damu iko chini kabisa. Idadi ya watu waliopata mgando wa damu baada ya chanjo ya Johnson & Johnson ilikuwa chini zaidi ikilinganishwa na mamilioni ya watu waliopata chanjo na hakupata mgando wa damu. Hata hivyo, Washington State Department of Health (DOH, Idara ya Afya katika Jimbo la Washington) na Centers for Disease Control and Prevention (CDC, Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Ugonjwa) zinapendekeza watu walio na miaka 18 na zaidi kuchagua kupata dozi ya mRNA ya chanjo ya COVID-19 ya (Pfizer au Moderna) badala ya chanjo ya Johnson & Johnson kwa sababu ya hatari inayoweza kutokea ya mvilio kwenye mishipa ya damu iliyo na thrombocytopenia syndrome (TTS, mgando wa damu pamoja na idadi ya chini ya plateleti), ambayo inajumuisha mgando wa damu na plateleti kidogo, na Guillain-Barré syndrome (GBS, tatizo ambapo kingamwili ya mtu huharibu neva), ambayo ni tatizo la kiotomatiki la kingamwili inayoweza kusababisha kuharibika kwa neva.

Chanjo ya Johnson & Johnson bado inapatikana iwapo huwezi au hauko tayari kupata chanjo ya mRNA. Unaweza kuongea na mhudumu wako wa afya kuhusu hatari yako. Ripoti kadhaa za mgando wa damu baada ya chanjo ya Johnson & Johnson zilikuwa katika wanawake wakubwa wa chini ya miaka 50. Iwapo wewe ni mwanamke wa kati ya miaka 18 na 50, unafaa kufahamu kuwa una hatari ya juu ya kupata migando ya damu, inayoweza kusababisha kifo. Hofu ya kuganda kwa damu ilihusika tu na chanjo ya COVID-19 ya Johnson & Johnson, si chanjo za Pfizer au Moderna.

Jifunze mengi kwa kusoma kuhusu chanjo ya COVID-19 ya Johnson & Johnson (Kiingereza pekee).

Nafaa kuwa na hofu kuhusu uvimbe wa mishipa ya moyo?

Visa vya uvimbe wa misuli ya moyo na uvimbe wa kuta za moyo baada ya chanjo ya COVID-19 ni nadra sana. Idadi kidogo tu ya watu ndio wanaweza kuupitia baada ya chanjo. Kwa watu wanaopitia, visa vingi vinapatikana katika vijana na watu wazima wadogo, dalili ni kidogo mara nyingi, na watu kimsingi hupata nafuu wao wenyewe au kwa matibabu kidogo mno. Uvimbe wa misuli ya moyo na uvimbe wa kuta za moyo ni wa kawaida zaidi ukiambukizwa COVID-19.

Kufikia Julai 30, 2021, kati ya chini ya ripoti 1500 kwa Vaccine Adverse Event Reporting System (VAERS, Mfumo wa Kuripoti Tukio Hatari ya Chanjo) kuna visa 699 pekee vilivyothibitishwa Marekani, (Kiingereza pekee) huku zaidi ya watu milioni 177 wamekuwa na angalau dozi moja ya chanjo ya COVID-19.

Unaweza kuongea na daktari wako kuhusu hatari yako. Ikiwa una dalili zozote baada ya chanjo, unaweza kuziripoti kwa VAERS (Kiingereza pekee).

Jifunze zaidi kuhusu uvimbe wa misuli ya moyo na uvimbe wa kuta za moyo baada ya chanjo ya COVID-19.(Kiingereza pekee)

Je, naweza kupata chanjo ikiwa nina hali ya afya iliyopo tayari?

Watu wengi walio na hali zilizopo awali za kiafya au kimatibabu wanaweza kupata chanjo za COVID-19. Ruhusu mhudumu wako wa afya kujua kuhusu mizio na hali zote za kiafya. Kwa kweli, hali nyingi zilizopo hukuweka katika hatari ya juu ya matatizo kutokana na ugonjwa wa COVID-19, hivyo chanjo ni muhimu zaidi katika kukulinda dhidi ya kuwa mgonjwa.

Vikundi hivi maalum vya watu wanaweza kupata chanjo ya COVID-19:

  • Watu walio na maambukizo ya virusi vya UKIMWI na walio na mifumo dhaifu ya kingamwili.
  • Watu walio na hali za kingamwili otomatiki.
  • Watu ambao awali walikuwa na Guillain-Barré syndrome (GBS, Tatizo la Guillain-Barré).
  • Watu ambao awali walikuwa na kifafa cha Bell's.

Ikiwa una historia ya mizio mikali au unadhani kuwa huenda una mizio mikali kwa viambato vya chanjo, soma kuhusu chanjo za COVID-19 kwa watu walio na mzimio.(Kiingereza pekee) Mmenyuko wa mzio baada ya chanjo ya COVID-19 (Kiingereza pekee) ni nadra na imefanyika kwa karibu watu 2 hadi 5 kwa kila milioni waliopokea chanjo Marekani.

Maelezo haya (Kiingereza pekee) inalenga kuwasaidia watu katika vikundi vilivyo hapo juu kufanya uamuzi wa kipekee kuhusu kupokea chanjo ya COVID-19.

Je, chanjo itabadilisha DNA yangu?

La, Chanjo za COVID-19 hazibadilishi au kubadilisha DNA yako. Chanjo huwasilisha maelekezo kwa seli zetu ili kuanza kujenga ulinzi dhidi ya virusi vinavyosababisha COVID-19. Chanjo haiingii katika sehemu ya seli ambapo DNA yetu inahifadhiwa. Badala yake, chanjo hizo zinafanya kazi ulinzi asili wa mwili wetu kujenga jumuiya. Jifunze zaidi kuhusuchanjo za COVID-19 za mRNA (Kiingereza pekee) na aina iliyosambaa.(Kiingereza pekee)

Je, chanjo inasababisha madhara yoyote ya muda mrefu?

Tuna data nyingi sana ya kisayansi kuhusu chanjo za COVID-19 na magonjwa mengine. Kutegemea data hizo, wataalam wana ujasiri kuwa chanjo ziko salama. Karibu hisia zote kuhusu COVID-19 (chanjo) zimekuwa tulivu, kama uchovu au mkono uliovimba, na kukaa tu kwa siku kadhaa. Hisia kali au za muda mrefu ni nadra kabisa

Madhara yoyote ya muda mrefu mara nyingi hutokea ndani ya wiki nane za maambukizo. Hii ndiyo sababu ambayo watengenezaji wa chanjo walihitajika kusubiri angalau wiki nane baada ya majaribio ya kimatibabu kabla ya wao kuweza kutuma ombi la Uidhinishaji wa Matumizi ya Dharura kutoka Food and Drug Administration (FDA, Usimamizi wa Chakula na Dawa Marekani). Wataalamu pia wanaendelea kufuatilia chanjo za COVID-19 kwa sababu ya hofu za usalama. FDA huchunguza ripoti zozote za madhara makali.