Kuwapa Vijana Chanjo

Maudhui yalisasishwa mwisho Mnamo tarehe 20, Mei 2022

Decorative

Usalama na Ufaafu wa Chanjo

Kumruhusu mtoto wako kupata chanjo dhidi ya COVID-19 kunaweza:

  • Kusaidia kupunguza hatari ya wao kuambukizwa COVID-19
  • Kupunguza nafasi yao ya kuwa wagonjwa sana, wakiambukizwa COVID-19
  • Kupunguza nafasi yao ya kuhitaji kulazwa hospitalini na kupunguza hatari yao ya kufa kutokana na COVID-19
  • Kusaidia kuwazuia dhidi ya kuambukizwa na aina ya COVID-19
  • Kuongezeka kwa idadi ya watu katika jumuiya ambao wamelindwa dhidi ya kuambukizwa COVID-19 — na kuleta ugumu wa kusambaa kwa ugonjwa huo
  • Kupunguza usumbufu wa watoto kusoma darasani na shughuli kwa kusaidia kupunguza msambao wa COVID-19
Decorative

Majaribio ya Kimatibabu

Watoto walio na umri wa miaka 5-11

Watoto walio na umri wa miaka 12-15

Uidhinishaji wa Chanjo

Chanjo ya Pfizer inapatikana kwa watoto walio na umri wa miaka 5-15 chini ya Emergency Use Authorization (EUA, Uidhinishaji wa Matumizi ya Dharura), na imeidhinishwa kamili kwa watu walio na umri wa miaka 16+.

EUA huruhusu Food and Drug Administration (FDA, Utawala wa Chakula na Dawa) kufanya bidhaa kupatikana wakati dharura ya jimbo imetangazwa kabla ya kupewa leseni kamili. Azma ya uidhinishaji wa matumizi ya dharura ni kuhakikisha kuwa watu wanaweza kupata chanjo za kuokoa maisha kabla ya uchanganuzi wa data kwa muda mrefu. EUA bado inahitaji ukaguzi wa data za kimatibabu wa kina zaidi—kwa kipindi kifupi cha wakati tu.

Decorative

EUA yoyote itakayotolewa na FDA itapigwa msasa zaidi na Advisory Committee on Immunization Practices (Kamati ya Ushauri kuhusu Matendo ya Chanjo) (Kiingereza pekee) ya Centers for Disease Control and Prevention (CDC, Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Ugonjwa) na Western States Scientific Safety Review Workgroup (Jopo Kazi la Ukaguzi wa Usalama wa Kisayansi wa Majimbo ya Magharibi).

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kwa Wazazi na Walezi

Kwa nini nafaa kuwa na wasiwasi kuhusu mtoto wangu kuambukizwa COVID-19?

Tangu kuanza kwa janga hili tandavu, zaidi ya watoto milioni 12 Marekani wameambukizwa COVID-19. Aina mpya za COVID-19 ni hatari mno na zinaweza kuambukizwa kwa vijana tofauti na aina za awali na kusababisha kilele cha vijana wanaolazwa hospitalini kwa sababu ya COVID-19.

Huku COVID-19 mara nyingi huwa si hatari kwa watoto ikilinganishwa na watu wazima, watoto bado wanaweza kuwa wagonjwa sana na kusambaza kwa marafiki na familia walio na kingamwili duni au walio na uwezo wa kudhurika katika njia nyingine.

Watoto walioambukizwa COVID-19 wanaweza kupata "COVID-19 ndefu" au dalili za mara kwa mara zinajumuisha uchovu, maumivu ya kichwa, kichefuchefu na upungufu wa pumzi. Chanjo ndiyo njia bora ya kufanya watoto kuwa na afya nzuri na salama.

Watoto walioambukizwa COVID-19 wanaweza kuwa katika hatari ya juu ya Dalili ya Ugonjwa wa Uvimbe katika Mifumo Kadhaa (MIS-C) (Kiingereza pekee). MIS-C ni hali ambapo viungo tofauti vya mwili vinaweza kuwa na uvimbe, ikiwa pamoja na moyo, mapafu, figo, ubongo, ngozi, macho, au viungo vya utumbo. Huku chanzo cha MIS-C bado hakijulikani, watoto wengi walioambukizwa MIS-C walikuwa na COVID-19, au walikuwa karibu na mtu ambaye alikuwa na COVID-19. MIS-C inaweza kuwa kali, au hata kusababisha kifo, lakini watoto wengi waliopatikana na hali hii wamepata nafuu kutokana na huduma ya afya.

Je, chanjo inahitajika ili kuingia katika shule ya K-12?

Washington State Board of Health (Bodi ya Afya katika Jimbo la Washington), si Department of Health (Idara ya Afya), ina mamlaka ya kuunda mahitaji ya chanjo kwa watoto waliopo katika shule za K-12 Revised Code of Washington (RCW, Msimbo wa Washington Uliorekebishwa) 28A.210.140. Hakuna mahitaji ya chanjo ya COVID-19 katika shule au kituo cha kutunzia mtoto kwa wakati huu.

Je, nahitajika kulipia chanjo?

La. Mtoto wako atapata chanjo bila gharama yoyote kwako. Serikali ya muungano inalipia gharama kamili ya chanjo.

Ukiwa na bima ya afya ya umma au ya kibinafsi, mtoaji wako wa chanjo anaweza kuwatumia bili ili waweze kurejeshewa pesa ya utoaji wa chanjo. Ikiwa huna bima, serikali ya muungano inatoa mpango utakaomlipa mhudumu kukupatia chanjo.

Hufai kutozwa gharama zozote za kujilipia mwenyewe au kupokea bili kutoka kwa mtoaji wako kwa ajili ya ada ya utoaji wa chanjo ya COVID-19. Hii inatumika kwa watu walio na bima ya kibinafsi, wana Apple Health (Medicaid), wana Medicare, au wasio na bima.

Madhara ya kawaida ya chanjo ya COVID-19 katika watoto ni gani?

Hatari za kiafya iwapo watoto wameambukizwa COVID-19 zipo juu zaidi ya hatari ya madhara ya chanjo.

Sawa na chanjo nyingine, madhara ya kawaida zaidi ni maumivu ya mkono, uchovu, maumivu ya kichwa, na maumivu ya misuli. Dalili hizi mara nyingi huwa chini.

Katika majaribio ya kimatibabu (Kiingereza pekee) watoto wengi waliripoti madhara baada ya dozi ya pili ikilinganishwa na dozi ya kwanza. Madhara kwa kawaida zilikuwa kiasi hadi wastani na yalitokea ndani ya siku mbili baada ya chanjo, na mengi yalipotea baada ya siku moja au mbili.

Kuna viambato gani katika chanjo ya Pfizer?

Viambato katika chanjo ya Pfizer ni za kawaida sana kwa chanjo. Chanjo ina viambato amilifu vya mRNA pamoja na viambato vingine kama mafuta, chumvi, na sukari zinazolinda kiambato amilifu, kuisaidia kufanya kazi vizuri kwa mwili, na kulinda chanjo wakati wa uhifadhi na usafirishaji.

Chanjo ya Pfizer haina seli za binadamu (ikijumuisha seli za kijusi), virusi vya COVID-19, mpira, vifaa vya kuhifadhi, au bidhaa yoyote kutoka kwa mnyama ikijumuisha bidhaa za nyama ya nguruwe. Chanjo hizi hazikuzwi kwenye mayai na hazina bidhaa zozote za mayai.

Tazama Maswali na Majibu; ukurasa wa wavuti kutoka Children's Hospital of Philadelphia (Hospitali ya Watoto ya Philadelphia) (Kiingereza pekee) kwa maelezo zaidi kuhusu viambato.

Mtoto wangu anaweza kupata chapa gani ya chanjo?

Chanjo ya COVID-19 ya Pfizer-BioNTech (Pfizer) ndiyo chanjo pekee iliyoidhinishwa kwa watoto walio na umri wa miaka 5 hadi 17. Hakuna chanjo nyingine ya COVID-19 ambayo imeidhinishwa kutumiwa na watu walio na umri wa chini ya miaka 18 kwa wakati huu.

Je, mtoto wangu atahitaji dozi ya kiongeza nguvu?

Kwa sasa, dozi za kuongeza chanjo nguvu zinapendekezwa tu kwa watu walio na umri wa miaka 5 na zaidi. Watu walio na umri wa miaka 17 na chini wanaweza kupata chanjo ya Pfizer pekee kwa ajili ya dozi yao ya kiongeza nguvu.

Mtoto wangu anahitaji dozi ngapi?

Watoto wote wanapendekezwa kupokea angalau dozi mbili. Dozi za ziada zinaweza kupendekezwa ili kuzingatiwa hadi sasa.

  • Watoto walio na umri wa miaka 5-11 hupata dozi ya watoto, ambayo ni kiwango tofauti na toleo la wanaobaleghe na watu wazima.
  • Watoto walio na umri wa miaka 12-17 wanastahiki kupata dozi ya wanaobaleghe/watu wazima.

Watoto walio na umri wa miaka 5 na zaidi ambao wana kingamwili duni kwa kiasi wastani au hatari wanafaa kupokea dozi ya ziada ya msingi siku 28 baada ya dozi yao ya 2 na watoto wa miaka 5+ wanafaa kupokea dozi ya kuongeza chanjo nguvu miezi. Dozi za ziada kwa vikundi vingine zinaweza kupendekezwa katika siku za baadaye.

Tafadhali kagua miongozo ya Centers for Disease Control and Prevention (CDC, Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa) kwa ajili ya watu walio na kingamwili duni au tembelea tovuti ya DOH.

Nafaa kuongea na nani nikiwa na maswali kuhusu chanjo?

Ongea na daktari wa mtoto wako au mhudumu mwingine wa afya unayemwamini, ongea na mhudumu wa afya katika jamii, au soma maelezo katika www.CovidVaccineWA.org.

Je, chanjo ya watoto walio na umri wa miaka 5-11 ni sawa na walio na umri wa miaka 12+?

Chanjo ya Pfizer-BioNTech ya watoto walio na umri wa miaka 5-11 ni viambato sawa vya chanjo, lakini ya dozi kidogo, theluthi moja ya ukubwa.

Bidhaa ya sasa kwa watu wazima na wanaobaleghe haifai kutumika katika watoto walio na umri wa miaka 5-11.

Je, naweza kumpeleka mtoto wangu kupata chanjo wapi?

Jimbo la Washington hutoa chanjo zote zilizopendekezwa bila gharama yoyote kwa watoto hadi watu wa miaka 18. Mwulize daktari wa mtoto wako au daktari wa mara kwa mara ikiwa wana chanjo ya COVID-19

Familia ambazo tayari hazina wahudumu wa afya wanaweza kupiga simu kwa Help Me Grow WA Hotline at 1-800-322-2588 au kwenda kwa ParentHelp123.org (katika Kiingereza na Kihispania pekee) ili kupata mhudumu wa afya, kliniki, au rasilimali nyingine za afya. Huduma hii haina malipo na usaidizi wa lugha pia unapatikana.

Pia unaweza kutembelea VaccineLocator.doh.wa.gov na utumie kichujio kuona orodha ya maeneo yaliyo na chanjo ya watoto karibu nawe.

Je, mtoto wangu anaweza kupokea chanjo ya COVID-19 wakipata chanjo nyingine kama za mafua?

Ndiyo. Mtoto wako anaweza kupata chanjo ya COVID-19 kwa wakati sawa na chanjo zake nyingine.

Huhitaji kuratibu chanjo za mtoto wako zinazotakikana shuleni (Kiingereza pekee) au chanjo nyingine zilizopendekezwa kando na chanjo ya COVID-19. Miadi ya chanjo ya COVID-19 ni nafasi nyingine ya kuhakikisha mtoto wako amepokea chanjo zote zilizopendekezwa.

Je, chanjo ya COVID-19 itahitajika ili mtoto wangu aweze kuhudhuria eneo la kuwatunzia watoto au makambi ya siku?

Washington State Board of Health (Kiingereza pekee) huamua ni chanjo gani zinahitajika kwa shule na maeneo ya kuwatunzia watoto. Hakuna mahitaji ya chanjo ya COVID-19 katika shule au kituo cha kutunzia mtoto kwa wakati huu.

Kwa makambi ya siku, angalia na shirika linaloendesha kambi hilo ili kujua mahitaji yao.