Matini za WA Notify

Je, ulipata matini au taarifa kutoka kwa Washington state Department of Health (DOH, Idara ya Afya ya jimbo la Washington)?

Kuna aina mbili za ujumbe wa maandishi/taarifa unaoweza kupokea kwa simu.

Taarifa ya kipimo chanya cha COVID-19:

DOH hutuma taarifa na/au ujumbe wa maandishi ukiwa na kiungo cha uthibitishaji kwenye namba zote za simu zinazohusiana na matokeo chanya ya kipimo cha COVID-19 yaliyoripotiwa DOH. Taarifa hii inatoa maelezo kuhusu jinsi ya kuwaarifu bila kujulikana watumiaji wengine wa WA Notify (Arifu WA) ambao huenda wamekuwa na mfiduo wa COVID-19.

Ikiwa wewe ni mtumiaji wa WA Notify, unahitaji tu kugusa taarifa au kubofya kwenye kiungo katika ujumbe wa maandishi na kufuata hatua zote katika WA Notify ili kuwaarifu watumiaji wengine bila kujulikana kuhusu mfiduo ambao huenda ulitokea.

Ikiwa wewe si mtumiaji wa WA Notify, unaweza kupuuza ujumbe wa maandishi. Ikiwa utapenda kujifunza zaidi kuhusu WA Notify, ikijumuisha jinsi ya kuiongeza kwenye simu, tembelea WANotify.org

Watumiaji wa WA Notify wanaotumia kipimo cha kibinafsi (kinachoitwa pia vipimo vya nyumbani) na kupatikana na maambukizo ya COVID-19 wanaweza kuomba msimbo wa uthibitisho ili kuwaarifu bila kujulikana watumiaji wengine wa WA Notify (Arifu WA) ambao huenda wamekuwa na mfiduo wa COVID-19. Tembelea sehemu ya "Jinsi ya kuwaarifu wengine ukipatikana na maambukizo ya COVID-19 kwa kipimo cha kibinafsi" kwenye WANotify.org.

Taarifa ya mfiduo wa COVID-19 ambao huenda ulitokea

Watumiaji wa WA Notify ambao huenda walikuwa na mfiduo watapokea taarifa ya mfiduo.

Ujumbe na taarifa hukaa vipi?

Taarifa ya kipimo chanya cha COVID-19

Picha ya ujumbe na taarifa

pop up notification screenshot

 

Maudhui ya taarifa na ujumbe

Shiriki Utambuzi wako wa COVID-19

Donoa hapa ili kuwafahamisha wengine bila kufahamika kuwa ni wewe kwamba huenda wamekuwa na mfiduo wa COVID-19. Fuata hatua ili kuiweka jamii yako salama. Maelezo yako ya kibinafsi hayatashirikiwa.

Picha ya ujumbe na taarifa

text message screenshot

 

Maudhui ya taarifa na ujumbe

Message from (Mensaje del) WA Dept. of Health:

This number was given for a recent COVID-19 test. If this phone uses WANotify AND belongs to the person tested, please click the link within 24 hours. Follow the steps to anonymously alert others who may have been exposed.

https://us-wa.en.expressly/v?c=8w5io5c38ipo24fc

Se dio este numéro para una prueba reciente de COVID-19. Si este teléfono usa WANotify Y es de quien se hizo la prueba, haga clic en el enlace en las próximas 24 horas. Siga los pasos para alertar anónimamente a quienes tal vez hayan sido expuestos.

NOT the person tested? Need more information? Visit wanotify.org/text

¿NO es quien se hizo la prueba? ¿Desea más información? Visite notificawa.org/texto

Picha ya ujumbe na taarifa

text message screenshot

 

Maudhui ya taarifa na ujumbe

Message from WA Dept. of Health:

If this phone uses WANotify AND belongs to the person tested, please click the link within 24 hours. Follow the steps to anonymously alert others who may have been exposed.

https://us-wa.en.expressly/v?c=5b56h13n80q9onll

NOT the person tested? Need more information? Visit wanotify.org/text.

Picha ya ujumbe na taarifa

text message screenshot

 

Maudhui ya taarifa na ujumbe

Mensaje del Departamento de Salud del Estado de Washington:

Si este teléfono usa WANotify Y es de quien se hizo la prueba, haga clic en el enlace en las próximas 24 horas. Siga los pasos alertar anónimamente a quienes tal vez hayan sido expuestos.

https://us-wa.en.expressly/v?c=dvo8iije3v33saoj

¿NO es quien se hizo la prueba? ¿Desea más información? Visite notificawa.org/texto.

Taarifa ya mfiduo wa COVID-19 ambao huenda ulitokea

Picha ya ujumbe na taarifa

exposure notification screenshot

Maudhui ya taarifa na ujumbe

Inawezekana kwamba umeambukizwa COVID-19

Umekuwa karibu na mtu aliyeambukizwa virusi vya COVID-19 hivi karibuni. Utakachofanya baada ya hapa ni muhimu na tuko hapa kusaidia. Bonyeza ili kujifunza mengi zaidi.

Nafaa kufanya nini ikiwa nilipokea matini au taarifa?

Watumiaji wa WA Notify wanafaa kubofya kwenye kiungo katika ujumbe wa matini au kudonoa taarifa na kufuata hatua zote ili kuthibitisha matokeo yao katika programu bila kujulikana. Hii huwaarifu watumiaji wengine wa WA Notify bila kutaja jina kuwa hivi karibuni walikuwa karibu na mtu aliye na maambukizo ya COVID-19. Kuruhusu watumiaji wa WA Notify kuthibitisha matokeo yao bila wao kujulikana huzuia msambao wa COVID-19 kwa haraka mno. Afya ya umma bado inaweza kuwasiliana na kutoa kiungo au msimbo wa uthibitisho wakati wa mchakato wa uchunguzi wa kisa.

Tafadhali wasiliana na daktari wako wa utunzaji wa msingi au mhudumu wa kipimo ikiwa:

  • ulipokea ujumbe wa matini na/au taarifa, lakini bado hujapokea matokeo yako rasmi ya kipimo, au
  • una maswali kuhusu matokeo yako ya kipimo

Maswali ya kawaida

Ikiwa WA Notify haijui mimi ni nani, nilipataje ujumbe na/au taarifa?

Ujumbe wa matini na taarifa zinatumwa na DOH, si WA Notify. DOH hutuma ujumbe wa matini na/au taarifa kwa kila mtu anayepatikana na maambukizo ya COVID-19 kwa sababu hatujui anayetumia WA Notify. Ikiwa hutumii WA Notify, unaweza kupuuza ujumbe na taarifa hiyo.

DOH hujuaje mtu wa kutumia matini au taarifa?

Kisheria, matokeo chanya ya kipimo kutoka kwa magonjwa kadhaa yanayoweza kuambukizwa lazima yaripotiwe kwa jimbo, pamoja na maelezo ya mwasilani. DOH hutumia maelezo ili kufanya uvhunguzi wa kisa na ufuatiliaji wa mwasilani (Kiingereza Pekee) ili kukomesha msambao wa ugonjwa. Kuarifu kila mtu anayepatikana na maambukizo huruhusu watumiaji wa WA Notify kuwajibika kwa haraka na kuwaarifu wengine bila kujulikana kuhusu maambukizo.

Situmii WA Notify. Kwa nini ulinitumia ujumbe?

DOH hutuma ujumbe wa matini na/au taarifa ibukizi kwa nambari za simu zilizotumika na watu ambao hivi karibuni walipatikana na maambukizo ya COVID-19.

DOH inajua tu mtu anayepatikana na maambukizo - hatujui mtu anayetumia WA Notify. Kwa kutuma ujumbe kwa kila mtu, tunaweza kusaidia watumiaji wa WA Notify kuwaarifu wengine bila kujulikana kuhusu maambukizo ambayo huenda yalitokea kwa haraka zaidi na kuokoa maisha.

Ikiwa hutumii WA Notify, hakuna hatua inayohitajika. Ikiwa ungependa kujifunza mengi kuhusu WA Notify, ikijumuisha jinsi ya kuiongeza kwenye simu yako, tembelea WANotify.org

Nambari ya Simu ambayo utatuma ujumbe huo ni gani?

Nambari ambayo DOH itatumia kutuma ni 1-844-986-3040.

Nilipokea taarifa na/au ujumbe wa matini lakini mtu aliyepimwa alikuwa mwanafamilia au mtu wa kaya. Nafaa kufanya nini?

Mtumiaji wa WA Notify aliyepatikana na maambukizo anafaa kuruhusu hatua za kuwaarifu wengine bila kujulikana ambao huenda wakaambukizwa, hivyo unafaa kupuuza ujumbe wowote au taarifa ambazo si zako.

Ikiwa mwanafamilia au mwanachama wa kaya yako ni mtumiaji wa WA Notify, amepatikana na maambukizo, na bado wanahitaji kuthibitisha matokeo yao katika WA Notify, wanaweza kufuata hatua katika sehemu ya "Jinsi ya kuwaarifu wengine ukipatikana na maambukizo ya COVID-19 kwa kutumia kipimo cha kibinafsi" kwenye WANotify.org.

Nina muda upi wa kudonoa taarifa au kuwezesha kiungo cha uthibitishaji?

Una saa 24 baada ya kupokea taarifa au ujumbe wa matini ili kufuata hatua za kuwaarifu wengine katika WA Notify. Iwapo huwezi kudonoa taarifa au kubofya kiungo cha uthibitisho ndani ya muda, unaweza kuomba kiungo cha uthibitisho katika WA Notify kwa kufuata hatua katika sehemu ya ""Jinsi ya kuwaarifu wengine ukipatikana na maambukizo ya COVID-19 kwa kutumia kipimo cha kibinafsi" kwenye WANotify.org.

Je, zaidi ya mtu mmoja anaweza kutumia ujumbe wa matini au taarifa kuwezesha kiungo cha uthibitishaji katika WA Notify?

La. Ikiwa mwanafamilia au mwanachama wa kaya yako ni mtumiaji wa WA Notify, amepatikana na maambukizo, na bado wanahitaji kuthibitisha matokeo yao katika WA Notify, wanaweza kufuata hatua katika sehemu ya "Jinsi ya kuwaarifu wengine ukipatikana na maambukizo ya COVID-19 kwa kutumia kipimo cha kibinafsi" kwenye WANotify.org.

Nitapataje tarehe yangu ya mfiduo katika WA Notify?

Kwenye iPhone:

  1. Nenda kwenye Settings (Mipangilio)
  2. Teua Exposure Notifications (Taarifa za Mfiduo) au weka Exposure Notifications katika Mwambao wa Utafutaji
  3. Tarehe yako ya karibu ya mfiduo unaoweza kutokea itaonyeshwa chini ya "You may have been exposed to COVID-19 (Huenda umeambukizwa COVID-19)"

Kwenye Android:

  1. Fungua programu ya WA Notify
  2. Teua See Details (Tazama Maelezo) chini ya "Possible exposure reported (Mfiduo unaowezekana ulioripotiwa)"
  3. Tarehe yako ya karibu ya mfiduo unaoweza kutokea itaonyeshwa chini ya "Possible Exposure Date (Tarehe ya Mfiduo Inayowezekana)"