Sera ya Faragha ya WA Notify

Sera hii ya faragha inatumika kwa WA Notify (Arifu WA), teknolojia rasmi ya taarifa ya mfiduo ya Jimbo la Washington. WA Notify iliundwa kwa usimamizi na pendekezo la Department of Health (DOH, Idara ya Afya) ya Jimbo la Washington.

Tunakusanya na kutumia taarifa gani?

Data isiyojulikana inaweza kukusanywa katika WA Notify kuhusu matukio yanayofuata:

 • Kupakua au kuwezesha WA Notify.
 • Kupokea taarifa ya mfiduo.
 • Kuwasilisha msimbo wa uthibitishaji au kiungo cha uthibitishaji.
 • Kupakia misimbo nasibu ya watumiaji walioambukizwa ambao wamechagua kuwaarifu wengine.
 • Kukumbana na masuala ya kifundi kwenye programu (data ya utambuzi wa ugonjwa, ikiwemo takwimu za utendaji wa programu).

DOH hutumia taarifa ya tukio a hapo juu kufahamu jinsi ambavyo WA Notify inatumika. Data hii inaweza kushirikiwa na DOH, taasisi za afya ya umma, au mamlaka ya afya yaliyoruhusiwa. Inaweza pia kutumika kwa njia ya pamoja katika malengo ya utafiti wa kitakwimu au kisayansi. Taarifa hii haijumuishi taarifa yoyote ya kibinafsi au ya eneo wala haiwezi kutumika kutambua mtumiaji yeyote wa WA Notify.

WA Notify imeundwa ili kulinda faragha ya mtumiaji kama kipaumbele cha juu, ambayo inaendana na lengo la Google na Apple. WA Notify huzalisha vipengele vifuatavyo vya data, ambavyo havina data inayoweza kutambuamtu yeyote anayetumia zana hiyo:

Misimbo Nasibu.

 • Misimbo nasibu inashirikiwa kupitia Bluetooth kati ya simu mahiri za watumiaji wa WA Notify wakiwa karibu na kila mmoja.
 • Misimbo nasibu inazalishwa na kuhifadhiwa kwenye simu janja, si na WA Notify
 • Misimbo nasibu inatumika tu kuruhusu WA Notify na simu yako janja kuangalia iwapo kuna mifiduo ya COVID-19 inayowezekana.
 • Misimbo nasibu inahifadhiwa kwa kipindi kisichozidi siku 14.

Misimbo na viungo vya uthibitishaji

 • Ili kuwatahadharisha kwa haraka na bila kujulikana watumiaji wa WA Notify ambao wanaweza kuwa wamekuwa kwenye hatari ya kupata COVID-19, DOH hutuma taarifa na/au ujumbe mfupi wa maandishi wenye kiungo cha uthibitishaji kwenye namba zote za simu zinazohusiana na matokeo chanya ya kipimo cha COVID-19 yaliyoripotiwa DOH.
  • Kudonoa taarifa au kubofya kwenye kiungo cha uthibitishaji huruhusu misimbo yako nasibu ya kushirikiwa, ambayo huarifu bila kutaja majina watumiaji wengine uliokuwa karibu nao kuwa huenda wameambukizwa.
  • DOH hutuma ujumbe wa matini ulio na kiungo cha uthibitishaji kwa kila mtu anayepatikana na maambukizo ya COVID-19 kwa sababu hatujui anayetumia WA Notify. Ikiwa hutumii WA Notify, unaweza kuongeza WA Notify kwenye simu yako au kupuuza ujumbe huo.
  • Unaamua kama utadonoa taarifa au kubofya kwenye kiungo cha uthibitishaji ili kuarifu bila kujilikana watumiaji wengine wa WA Notify.
 • Ukipatikana na maambukizo ya COVID-19, mtu kutoka mamlaka yako ya ndani ya afya ya umma anaweza kuwasiliana nawe, na kuuliza ikiwa unatumia WA notify. Ikiwa unatuia na bado hujapokea ujumbe wa uthibitisho, watakupatia msimbo au kiungo cha uthibitisho ili uingiie kwenye WA Notify.

Kumbukumbu za Matumizi

 • Sawa na karibu kila programu au huduma yoyote ya intaneti, WA Notify huzalisha otomatiki kumbukumbu ukitumia huduma. Kumbukumbu hizi zinajumuisha maelezo kuhusu simu yako janja. Tunatumia maelezo haya kutatua masuala na WA Notify.
 • Kumbukumbu hizi hazijumuishi misimbo nasibu au viungo au misimbo ya uthibitishaji na haziwezi kutumika kufunga ama aina ya msimbo na wewe au simu yako mahiri.
 • Kumbukumbu hizi zinafutwa otomatiki siku 14 baada ya kuzalishwa.

Data ya Uchanganuzi

 • Ukichagua kuwezesha uchanganuzi wa ziada, jumla ya data yenye kikomo itashirikiwa na DOH ili kusaidia kuboresha programu hiyo.
 • Data hii inajumuisha takwimu kuhusu jinsi programu hiyo inatumika. Haijumuishi maelezo yoyote yanayoweza kutumika kukutambua.
 • Unaweza kuchagua kutoshiriki data hii kwa kuzima kushiriki uchanganuzi katika programu hiyo.
 • Kwa muundo, WA Notify haikusanyi data ya eneo kutoka kwa simu yako janja, na haikusanyi au kushiriki maelezo ambayo yanakufunganisha au kufunganisha simu yako janja kwa misimbo nasibu au misimbo ya uthibitishaji.

Data ya Utambuzi

 • Ilivyo na karibu kila programu au huduma ya intaneti, WA Notify huzalisha otomatiki data ya utambuzi ukitumia huduma hiyo.
 • Programu ya Android ya WA Notify imeundwa na Google, sawa na programu nyingine za mfiduo zinazotumia teknolojia sawa ya Apple/Google.
 • Google hutumia taarifa hii kutambua masuala yaliyo na WA Notify na programu nyingine za mfiduo kwa kutumia teknolojia sawa na ya Apple/Google.
 • Taarifa hii ya utambuzi haijumuishi taarifa yoyote ya kibinafsi au ya eneo wala haiwezi kutumika kutambua mtumiaji yeyote wa WA Notify.

Ni nini hufanyika ukiomba msimbo wa uthibitishaji:

Watumiaji wa WA Notify watakaopatikana na maambukizo ya COVID-19 kwa kutumia kipimo cha kibinafsi wanaweza kuomba msimbo wa uthibitishaji katika WA Notify ili kuwaarifu bila kujulikana watumiaji wengine wa WA Notify. Ili kupokea msimbo wa uthibitishaji, watumiaji wa WA Notify ni lazima waweke tarehe ya kipimo chao kinachoonyesha wameambukizwa na nambari yao ya simu. Kifaa kilichotumika kuomba msimbo ni lazima kitumike kuweka msimbo wa uthibitishaji au kubofya kiungo cha uthibitishaji ili kuarifu bila kujilikana watumiaji wengine wa WA Notify.

Ili kuzuia ripoti marudufu za matokeo sawa ya kipimo, WA Notify huhifadhi kwa muda mfupi toleo lililosimbwa la nambari ya simu iliyotumika kuomba msimbo kwa hadi siku 30. Taarifa hii haitajumuisha taarifa yoyote ya kibinafsi au ya eneo wala haitatumika kutambua mtumiaji yeyote wa WA Notify.

Tunashiriki maelezo yako wakati gani?

Hatutakusanya au kushiriki kwa hiari yoyote kati ya maelezo yako na mtu yeyote, isipokuwa ukichagua kuingiza msimbo wa uthibitishaji au kubofya kiungo cha uthibitishaji. Ukifanya hivyo, WA Notify itashiriki misimbo yako nasibu na simu janja nyingine ambazo zimekuwa karibu na simu yako janja. Kiungo au msimbo wa uthibitishaji hauwezi kuunganishwa tena na wewe na mtu ambaye hana ufikiaji wa simu yako janja. Tafadhali kagua sehemu ya "Tunakusanya na Kutumia Taarifa Gani?" ili kujifunza zaidi kuhusu taarifa ambayo inakusanywa na kutumika katika WA Notify.

Tunalinda vipi maelezo yako?

WA Notify inalinda misimbo nasibu kwa kutumia Exposure Notification Framework (Mfumo wa Taarifa ya Mfiduo) wa Google na Apple, ambao unajumuisha mahitaji maalum zaidi kuhusu jinsi ya kusimbua fiche na kuzihamisha. WA Notify haihifadhi au kuzalisha misimbo yako nasibu - simu yako janja hufanya hivyo.

Haki zako ni taarifa yako

Kwa sababu misimbo ya uthibitishaji na kumbukumbu za programu haziwezi kuhusishwa na wewe bila kufikia simu yako mahiri, DOH haina jia yoyote ya kufikia taarifa hii. Kwa sababu ya hii, DOH haiwezi kukupatia taarifa hii salama au kuifuta iwapo utaomba. Unadhibiti matumizi ya WA Notify. Simu yako janja inafaa kukuruhusu kuzima taarifa za mfiduo au kufuta kumbukumbu za mfiduo kwenye simu yako janja wakati wowote. Zaidi ya hayo, unaweza kuondoa WA Notify wakati wowote ule. Ukiondoa, misimbo yote nasibu iliyohifadhiwa itafutwa.