Chanjo ya COVID-19

Chanjo ya COVID-19 ni ya bila malipo na inapatikana kwa watu wote walio na umri wa miaka miezi 6 na zaidi bila kujali hali yao ya uhamiaji.

Huwezi kutoka nyumbani na unahitaji chanjo ya COVID-19? Tafadhali tazama hapa

Maudhui yamesasishwa mara ya mwisho tarehe 22 Julai 2022

Mapendekezo ya dozi ya kiongeza nguvu ya Center for Disease Control and Prevention (CDC, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa) na Western States Scientific Safety Review Workgroup (Kundi la Kazi la Ukaguzi wa Usalama wa Kisayansi wa Mataifa ya Magharibi) yaliyosasishwa ni kama ifuatavyo:

 • Watoto walio na umri wa miaka 5 hadi 11 wanapaswa kupata dozi ya kiongeza nguvu miezi mitano baada ya kukamilisha chanjo yao ya msingi ya Pfizer-BioNTech Watoto walioathiriwa kingamaradhi wanapaswa kupata kiongeza nguvu chao angalau miezi mitatu baada ya chanjo yao ya msingi.
 • Kila mtu aliye na miaka 12 na zaidi anapaswa kupata dozi ya kiongeza nguvu miezi mitano baada ya kukamilisha mfululizo wa chanjo yao ya msingi ya Pfizer au Moderna, au miezi miwili baada ya kupata chanjo ya mara moja ya Johnson & Johnson (J&J).
 • Kila mtu aliye na miaka 50 na zaidi anapaswa kupata dozi ya kiongeza nguvu ya pili miezi minne baada ya kupata dozi yake ya kwanza ya kiongeza nguvu.
 • Watu walio na miaka 12 na zaidi ambao kingamaradhi yao imeathiriwa kiasi au vibaya wanapaswa kupata dozi ya pili ya kiongeza nguvu miezi minne baada ya kupata dozi yake ya kwanza ya kiongeza nguvu.
 • Watu walio na miaka 18 na zaidi waliopataa chanjo ya msingi na dozi ya kiongeza nguvu ya chanjo ya J&J miezi minne iliyopita wanaweza kupata dozi ya pili ya kiongeza nguvu cha chanjo ya mRNA COVID-19.

Tunataka kukupatia maelezo unayohitaji. Tutakupa habari kila mara ili uweze kufanya chaguo zinazofaa kwa afya yako.

Nahitaji kujua nini ili kupata chanjo ya COVID-19?

Nitapataje chanjo hiyo?

Tembelea Kionyesha Chanjo ili kupata na kuratibu miadi.

Unaweza pia kutuma msimbo wako wa ZIP kwa 438-829 (GET VAX) ili kupata maeneo ya chanjo ya karibu na wewe.

Je, una maswali kuhusu chanjo ya COVID-19? Je, unahitaji usaidizi wa kupata miadi ya chanjo? Piga Nambari ya Simu ya Maelezo ya COVID-19 katika 1-800-525-0127, kisha ubonyeze #. Usaidizi wa lugha unapatikana.

Ikiwa unaratibu miadi ya dozi yako ya chanjo ya pili (Moderna/Spikevax au Pfizer/Comirnaty), unafaa kupata chanjo sawa na dozi yako ya kwanza.

Ikiwa wewe au mtu unayemjua yuko nyumbani na hawezi kutoka, jaza fomu salama ya mtandaoni (Kiingereza pekee). Majibu yako yataturuhusu kuunganisha watu binafsi na Timu za Chanjo katika Kaunti na/au Jimbo.

Kwa ajili ya masuala mengine yanayohusiana na COVID-19, kama nyumba, usaidizi wa matumizi, bima ya afya, piga simu kupiti 211 au tembelea wa211.org

Kwa taairfa zaidi, tazama karatasi ya ukweli ya Chanjo za COVID-19: Jambo la Kujua.

Je, ni lazima niwe raia wa Marekani ili kupata chanjo?

La, huhitaji kuwa raia wa Marekani ili kupata chanjo. Hiyo inamaanisha kuwa huhitaji nambari ya usalama wa jamii, au nyaraka nyingine na hali yako ya uhamiaji ili kupata chanjo. Baadhi ya watoaji wa chanjo wanaweza kukuuliza nambari ya usalama wa jamii, lakini si lazima uwape.

Mtoto wako hahitaji kuwa raia wa Marekani ili kupata chanjo. Wahudumu wa afya hawatauliza hali ya uhamiaji ya mtu yeyote. Mara nyingi, wazazi na walezi watahitaji kutoa ridhaa ya kutoa chanjo kwa kijana aliye na umri wa chini ya miaka 18.

Washington State Department of Health (Idara ya Afya katika Jimbo la Washington) inapendekeza kuwa watu wote walio na umri wa miaka miezi 6 na zaidi watapate chanjo.

Je, nitatozwa ili kupewa chanjo?

La. Hufai kutozwa chochote ukipata chanjo, au kupokea bili kutoka kwa mtoaji wako au kutoka kwa kituo cha chanjo. Hii inatumika kwa watu walio na bima ya kibinafsi, wana Apple Health (Medicaid), wana Medicare, au wasio na bima.

Ukipata huduma nyingine ukiwa katika mtoaji wako ili kupata chanjo, unaweza kupata bili ya ziara ya ofisi. Ili kuzuia hii, unaweza kumwuliza mtoaji wako mapema kuhusu gharama.

Ikiwa huna bima ya afya, watoaji hawawezi kukutoza ili kukupa chanjo na wanaweza kuwa wanakiuka mahitaji ya mpango wa chanjo ya COVID-19. Tafadhali tuma barua pepe kwa covid.vaccine@doh.wa.gov iwapo utatozwa.

Ikiwa una bima ya afya na umetozwa ada, wasiliana na mpango wa bima yako kwanza. Ikiwa hii haitatatua suala hilo, unaweza pia kuwasilisha malalamiko (Kiingereza pekee) na Ofisi ya Kamishna wa Bima.

 • Piga 800-562-6900 ili kupata huduma ya mkalimani kupitia kwa simu (inapatikana katika zaidi ya lugha 100 bila gharama yoyote kwako)
 • TDD/TYY: 360-586-0241
 • TDD: 800-833-6384
Je, kama sina bima ya afya?

Ikiwa huna bima, mwambia mhudumu wako. Bado utapata chanjo bila gharama yoyote.

Ikiwa sitatozwa kabla ya kupewa chanjo, kwa nini naulizwa maelezo yangu ya bima ya afya?

Ukipata chanjo, mtoaji wako wa chanjo anaweza kuuliza ikiwa una kadi ya bima. Hii ni ili waweze kurejeshewa pesa zao kwa sababu ya kukupatia chanjo (ada ya utoaji chanjo). Mfahamishe mtoaji wako ikiwa huna bima. Bado utaweza kupata chanjo bila gharama yoyote.

Ada ya utoaji wa chanjo ni nini na nani huilipia?

Ada ya utoaji wa chanjo ni ada ambayo mhudumu wa afya hutoza ili kukupatia chanjo. Hii ni tofauti na gharama ya chanjo yenyewe.

Serikali ya muungano inalipia gharama kamili ya chanjo. Ukiwa na bima ya afya ya umma au ya kibinafsi, mtoaji wako wa chanjo anaweza kuwatumia bili ili waweze kurejeshewa pesa ya utoaji wa chanjo.

Hufai kutozwa gharama zozote za kujilipia mwenyewe au kupokea bili kutoka kwa mtoaji wako kwa ajili ya ada ya utoaji wa chanjo ya COVID-19. Hii inatumika kwa watu walio na bima ya kibinafsi, wana Apple Health (Medicaid), wana Medicare, au wasio na bima.

Ni chanjo gani za COVID-19 zinapatikana kwa sasa?

Chanjo tatu zimeidhinishwa kwa matumizi ya dharura au kuidhinishwa kamili na U.S Food and Drug Administration (FDA, Usimamizi wa Chakula na Dawa Marekani).Chanjo hizi zinatolewa kwa sasa katika jimbo la Washington. Chanjo za Pfizer (Comirnaty) na Moderna (Spikevax) zinapendekezwa zaidi ya chanjo ya Johnson & Johnson kwa sababu ya hatari nadra ya hali inayojulikana kama mvilio kwenye mishipa ya damu iliyo na thrombocytopenia syndrome (TTS, mgando wa damu pamoja na idadi ya chini ya plateleti) na Guillain-Barré syndrome (GBS, tatizo ambapo kingamwili ya mtu huharibu neva).

Chanjo ya COVID-19 ya Pfizer-BioNTech (Comirnaty):

Dozi tatu zilitolewa kwa watoto walio na umri wa miezi 6 hadi miaka 4. Dozi mbili za kwanza zinafaa kupeanwa siku 21 baada ya dozi ya kwanza na dozi ya tatu wiki 8 baada ya dozi ya pili.

Hii ni chanjo ya dozi mbili, zinazopeanwa siku 21 kati ya dozi hizo mbili, pamoja na:

 • Watu ambao wana kingamwili duni na walipokea chanjo ya mRNA ya COVID-19 ya dozi mbili wanafaa kupokea dozi ya msingi ya ziada
 • Dozi za kuongeza chanjo nguvu ya watu walio na miaka 5 na zaidi, angalau miezi 5 baada ya dozi ya pili
 • Watu walio na umri wa zaidi ya miaka 50, na watu fulani walio na kingamwili dhaifu, wanaweza sasa kupokea dozi ya ziada ya kuongeza chanjo nguvu ya chanjo ya mRNA ya COVID-19 iwapo miezi 4 au zaidi imepita tangu walipopokea dozi yao ya mwisho ya kiongeza nguvu.

Mtu anakuwa amepokea chanjo zote za COVID-19 iwapo wamepokea dozi zote zilizopendekezwa katika misururu ya msingi na busta zote wanapostahiki.

Chanjo hii imeidhinishwa kamili kwa watu walio na umri wa miaka 12 au zaidi chini ya jina Comirnaty. Chanjo hiyo imeidhinishwa kwa matumizi ya dharura kwa vijana walio na umri wa miaka miezi 6 hadi 11. Majaribio ya matibabu yalionyesha kuwa hakuna matukio hatari yasiyotabiriwa.

Chanjo ya COVID-19 ya Moderna (Spikevax):

Hii ni chanjo ya dozi mbili, zinazopeanwa siku 28 kati ya dozi hizo mbili, pamoja na:

 • Dozi ya ziada (dozi ya tatu) ya chanjo ya watu walio na kingamwili dhaifu.
 • Dozi za kuongeza chanjo nguvu ya watu walio na miaka 18 na zaidi, angalau miezi 5 baada ya dozi ya pili
 • Watu walio na umri wa zaidi ya miaka 50, na watu fulani walio na kingamwili dhaifu, wanaweza sasa kupokea dozi ya ziada ya kuongeza chanjo nguvu ya chanjo ya mRNA ya COVID-19 iwapo miezi 4 au zaidi imepita tangu walipopokea dozi yao ya mwisho ya kiongeza nguvu.

Chanjo hii imeidhinishwa kamili kwa watu walio na umri wa miaka 18 na zaidi. Chanjo ya Moderna inapatikana kwa watoto walio na umri wa miezi 6 hadi miaka 17 chini ya Emergency Use Authorization (EUA, Uidhinishaji wa Matumizi ya Dharura). Mtu anakuwa amepokea chanjo zote za COVID-19 iwapo wamepokea dozi zote zilizopendekezwa katika misururu ya msingi na busta zote wanapostahiki.

Majaribio ya matibabu yalionyesha kuwa hakuna matukio hatari yasiyotabiriwa.

Chanjo ya COVID-19 ya Johnson & Johnson – Janssen:

Chanjo hii imeidhinishwa kwa matumizi ya dharura kwa watu walio na umri wa miaka 18 na zaidi. Hii ni chanjo ya dozi moja (sindano moja). Huzingatiwi kuwa umelindwa kamili hadi wiki moja hadi mbili baada ya wewe kupokea chanjo. Watu walio na umri wa miaka 18 na zaidi wanafaa kupata dozi ya ziada miezi miwili au zaidi baada ya dozi yao ya kwanza. Majaribio ya matibabu yalionyesha kuwa hakuna matukio hatari yasiyotabiriwa. Chanjo za Pfizer na Moderna zimependekezwa badala ya chanjo ya Johnson & Johnson. Watu wazima waliopokea chanjo ya msingi na dozi ya ziada ya chanjo ya COVID-19 ya Janssen ya Johnson & Johnson angalau miezi 4 iliyopita sasa wanaweza kupokea dozi ya pili ya chanjo ya ziada kwa kutumia chanjo ya COVID-19 a mRNA.

Chanjo ya COVID-19 ya Novavax:

 • Dozi mbili zinatumiwa siku 21 tofauti kwa walio na miaka 12 na zaidi

Chanjo hii imeidhinishwa kwa matumizi ya dharura kwa watu walio na umri wa miaka 12 na zaidi. Mtu anakuwa amepokea chanjo zote za COVID-19 iwapo wamepokea dozi zote zilizopendekezwa katika misururu ya msingi na busta zote wanapostahiki. Majaribio ya matibabu yalionyesha kuwa hakuna matukio hatari yasiyotabiriwa.

Nikichelewa kupata dozi yangu ya pili, nitahitaji kuanza upya misururu ya chanjo?

Ukichelewa kupata dozi yako ya pili, hutahitaji kuanza upya misururu ya chanjo.

Pata dozi ya pili haraka iwezekanavyo baada ya idadi ya siku zilizopendekezwa kupita tangu ulipopokea dozi yako ya kwanza.

Ni muhimu kupata dozi zote mbili bila kujali umbali wa muda kati ya dozi ya kwanza na ya pili.

Ikiwa kingamwili yako imedhoofika na unafuzu kupata dozi ya ziada, unafaa kusubiri angalau siku 28 baada ya dozi yako ya pili.

Je, naweza kupata chanjo ya COVID-19 iwapo nini ni mjamzito, nanyonyesha, au napanga kuwa mjamzito?

Ndiyo, data inaonyesha kuwa chanjo za COVID-19 ni salama wakati wa ujauzito. Centers for Disease Control and Prevention (CDC,Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Ugonjwa) (Kiingereza pekee), American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG, Chuo cha Marekani cha Madaktari wa Uzazi na Wanajinakolojia), na Society for Maternal-Fetal Medicine (SMFM, Jamii ya Dawa ya Mama na Kijusi) (Kiingereza pekee) inapendekeza chanjo ya COVID-19 kwa watu wajawazito, wanaonyonyesha, au wanaopanga kuwa wajawazito. Baadhi ya utafiti unaonyesha kuwa ikiwa umepokea chanjo, mtoto wako anaweza hata kupata kinga maradhi dhidi ya COVID-19 kupitia ujauzito au kunyonyesha. Watu wajawazito ambao hawajapokea COVID-19 wapo kwenye hatari ya matatizo makali kama kuzaa kabla ya siku au kuzaa mtoto amekufa. Isitoshe, watu wanaopata chanjo ya COVID-19 wakiwa wajawazito kwa kiwango cha mara mbili au tatu wana uwezekano mkubwa wa kuhitaji vifaa vya kusaidia maisha au mishipa ya kupumua.

Kupata rasilimali zaidi kuhusu kupata chanjo ya COVID-19 ukiwa mjamzito na unaponyonyesha, tafadhali tazama maelezo yaliyosasishwa kwenye tovuti ya One Vax, Two Lives.

Je, naweza kupata chanjo ya COVID-19 ikiwa naendelea napata chanjo za kawaida?

Ndiyo. Advisory Committee on Immunization Practices (ACIP, Kamati ya Ushauri kuhusu Matendo ya Chanjo) ilibadilisha mapendekezo ya mnamo Mei 12, 2021. Sasa unaweza kupata chanjo ya COVID-19 kwa wakati sawa na chanjo zako nyingine.

Huhitaji kuratibu chanjo za mtoto wako zinazotakikana shuleni (Kiingereza pekee) au chanjo nyingine zilizopendekezwa kando na chanjo ya COVID-19. Miadi ya chanjo ya COVID-19 ni nafasi nyingine ya kuhakikisha mtoto wako amepokea chanjo zote zilizopendekezwa.

Kadi ya rekodi ya chanjo ni nini?

Unafaa kupokea karatasi ya kadi ya chanjo ukipata dozi yako ya kwanza ya chanjo ya COVID-19. Kadi hii itakuambia aina ya chanjo uliyopata (Comirnaty/Pfizer-BioNTech, Spikevax/Moderna, au Johnson & Johnson) na tarehe uliyopokea chanjo hiyo.

Ikiwa ulipata chanjo ya Comirnaty/Pfizer-BioNTech au Spikevax/Moderna, mtoaji wako anafaa kukupatia miadi ya dozi yako ya pili wakati anakupatia dozi yako ya kwanza. Weka kadi hii ili mtoaji wako wa chanjo aweze kuikamilisha baada ya dozi yako ya pili.

Iwapo utapata dozi ya ziada au dozi ya kiongeza nguvu, unafaa pia kubeba kadi yako ya rekodi ya chanjo ukienda katika miadi yako. Mtoaji wako wa chanjo atarekodi dozi hiyo.

Hapa ni baadhi ya vidokezo muhimu vya kukumbuka unaposhughulikia kadi yako ya chanjo:

 • Weka kadi yako ya chanjo katikati ya dozi na baadaye.
 • Piga picha za mbele na nyuma ya kadi yako ili kuwa na nakala ya kidijitali karibu nawe.
 • Zingatia kujitumia kadi hiyo kwa barua pepe, kuunda albamu, au kuongeza lebo kwenye picha hiyo ili uweze kuipata tena kwa urahisi.
 • Piga chapa ya kadi hiyo ikiwa unataka kubeba moja popote uendapo.

Bado unaweza kupata dozi yako ya pili hata kama hutaleta kadi yako ya chanjo kwenye miadi yako. Mwambie mtoaji wako atafute aina (chapa) ya chanjo uliyopokea kwenye dozi yako ya kwanza ili kuhakikisha umepata aina sawa ya chanjo tena. Ukipoteza kadi yako ya chanjo, ingia kwenye MyIR (My Immunization Registry (Usajili wa Chanjo Yangu)) (Kiingereza pekee) ili kuangalia rekodi yako ya chanjo ya COVID-19, na kisha kupiga picha ya skrini au picha ya maelezo haya. Ikiwa huna akaunti, unaweza kujisajili kwenye MyIR wakati wowote.

Tafadhali kumbuka kuwa uthibitishaji wa rekodi zako kupitia MyIR huenda usiwe wa mara moja, na ufikiaji kwa sasa umewekewa kikomo kwa lugha ya Kiingereza pekee. Usaidizi wa simu moja kwa moja unapatikana ili kusaidia katika maswali ya MyIRmobile au rekodi ya chanjo kwa kupiga nambari ya simu ya Department of Health COVID-19 (Idara ya Afya, COVID-19) kupitia 833-VAX-HELP au wasiliana kupitia barua pepe waiisrecords@doh.wa.gov.

Usalama na Ufaafu

Kwa nini nafaa kupata chanjo ya COVID-19?

Ni chaguo lako bila shaka kupata chanjo ya COVID-19, lakini tunawahitaji watu wengi zaidi kupata chango kadri iwezekanavyo ili kumaliza janga hili. Ni vigumu kwa virusi vya COVID-19 kusambaa wakati watu wengi katika jamii wana kingamwili - kupitia chanjo au maambukizo ya hivi karibuni. Kiwango chetu cha chanjo kikiwa juu, kiwango chetu cha maambukizo kitakuwa chini.

Chanjo za COVID-19 zinaweza kukulinda katika njia nyingi:

 • Zinapunguza pakubwa nafasi yako ya kuwa mgonjwa sana ikiwa utaambukizwa COVID-19
 • Kupata chanjo kamili hupunguza nafasi zako za kulazwa hospitalini na kurudisha chini hatari ya kufa kutokana na COVID-19
 • Chanjo zinaongeza idadi ya watu ambao wamelindwa katika jumuiya, na kuleta ugumu wa kusambaa kwa ugonjwa huo
 • Wataalamu wanaendelea kuchunguza uwezo wa chanjo kuwazuia watu dhidi ya kusambaza virusi kwa wengine.

Mara tu umepewa uchanjo kamili, bado inawezekana kupata COVID-19, lakini ni nafasi kidogo sana ikiwa hukuwa umepewa chanjo.

Watu ambao hawajapata chanjo bado wanaweza kupata virusi na kusambaza kwa wengine. Baadhi ya watu hawawezi kupata chanjo kutokana na sababu za kimatibabu, na hii huwaacha na uwezo wa kudhurika na COVID-19. Ikiwa hujapata chanjo, wewe pia uko katika hatari ya juu ya kulazwa hospitalini au kufa kutokana na aina ya COVID-19 (Kiingereza pekee). Kupata chanjo husaidia kukulinda wewe na familia, majirani, na jamii yako.

Kwa nini nafaa kupata chanjo ya COVID-19 ikiwa watu wengi hunusurika wakiwa na ugonjwa huo?

Kifo si hatari pekee inayotokana na kuambukizwa COVID-19. Watu wengi wanaopata COVID-19 wana dalili za chini pekee. Hata hivyo, virusi haviwezi kutabiriwa kabisa, na tunajua baadhi ya aina za COVID-19 (Kiingereza pekee) zina uwezekano mkubwa wa kukufanya mgonjwa zaidi. Baadhi ya watu wanaweza kuwa wagonjwa sana au hata kufariki kwa sababu ya COVID-19, hata watu wadogo wasio na hali za afya za muda mrefu. Wengine, wanaojulikana kama "waathiriwa wa COVID kwa muda mrefu" wanaweza kupata dalili zinazokaa kwa miezi na kuathiri ubora wa maisha yao. Pia bado hatujui athari zote za muda mrefu za COVID-19 kwani ni virusi vipya. Kupata chanjo ni ulinzi wetu bora dhidi ya virusi. Hata kama wewe ni mdogo na mwenye afya nzuri, unafaa kupata chanjo ya COVID-19.

Aina ya COVID-19 ni nini?

Virusi hubadilika wakati vinasambaa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. 'Aina' ni kirusi kilichobadilika. Baadhi ya aina hupotea baada ya muda na nyingine huendelea kusambaa katika jamii.

Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Ugonjwa (CDC) vinatambua aina za virusi zinazoleta wasiwasi. Kwa sasa, aina kadhaa zinaleta wasiwasi kwa sababu zinasambaa kwa haraka na urahisi, na kusababisha maambukizo ya COVID-19.

Je, chanjo ya COVID-19 hufanya kazi dhidi ya aina za virusi?

Kupata chanjo husaidia kupunguza msambao wa virusi, na kupunguza msambao wa aina za virusi. Pia unakupa kinga imara dhidi ya kulazwa hospitalini na vifo kwa aina zote za virusi zinzojulikana, wakati wa dalili za chini.

Baadhi ya watu waliopokea chanjo bado wanaweza kuambukizwa na aina ya kirusi, lakini utafiti unaonyesha kuwa huwa wanapata dalili za chini. Ni muhimu kupata dozi zote zilizopendeke ili uwe na ulinzi wa juu dhidi ya aina.

Chanjo ndiyo njia bora ya kujilinda, kulinda wapendwa na jamii yako. Chanjo katika eneo kubwa itapunguza msambao wa virusi na kusaidia kuzizia kuchipika kwa aina mpya za virusi.

Tutajuaje kwamba chanjo ziko salama?

Kuhakikisha kuwa chanjo za COVID-19 ni salama, Centers for Disease Control and Prevention (CDC, Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa) ilipanua na kuwezesha uwezo wa nchi wa kufuatilia usalama wa chanjo. Kwa matokeo, wataalamu wa usalama wa chanjo wanaweza kufuatilia na kugundua masuala ambayo huenda hayajaonekana wakati wa majaribio ya kimatibabu ya COVID-19.

Ni nini inaendelea na chanjo ya Johnson & Johnson?

Kufikia Desemba 2021, Washington State Department of Health (DOH, Jimbo la Washington, Idara ya Afya) inapendekeza uchague kupata chanjo ya mRNA ya COVID-19 (Pfizer-BioNTech au Moderna) badala ya dozi moja ya chnjo ya Johnson & Johnson (J&J).

Sasisho hili linafuata mwongozo kutoka Centers for Disease Control and Prevention (Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Ugonjwa) baada ya data mpya iliwasilishwa kuhusu hali mbili za nadra ambazo hutokea baada ya kupokea chanjo ya J&J.

Chanjo hizi zinahusishwa tu na chanjo ya COVID-19 ya J&J, si chanjo za Pfizer au Moderna. Kwa watu wanaotafuta chanjo ya COVID-19, DOH inapendekeza chanjo za Moderna na Pfizer . Hata hivyo, chanjo ya J&J bado inapatikana iwapo huwezi au hauko tayari kupata chanjo yoyote kati ya hizi mbili. Tafadhali wasiliana na mhudumu wa afya ili kuongea kuhusu chaguo zako.

Iwapo ulipokea chanjo ya COVID-19 ya J&J ndani ya wiki tatu zilizopita au unapanga kupata chanjo ya COVID-19 ya J&J , jua ishara za onyo za aina ya mgando wa damu unaosababishwa na TTS. Zinajumuisha maumivu makali ya kichwa, maumivu ya chini ya tumbo, maumivu kwenye mguu, na/au upungufu wa pumzi. Ukipitia yoyote kati ya dalili hizi, tafadhali pata utunzaji wa kimatibabu mara moja.

Ni kawaida kuwa na dalili za chini hadi za wastani, ikijumuisha homa, maumivu ya kichwa, uchovu, na maumivu ya kiungo/misuli, wakati wa wiki ya kwanza baada ya kupokea chanjo yoyote ya COVID-19 Madhara haya mara nyingi yanafaa kuanza ndani ya siku tatu baada ya kupata chanjo na yanafaa kukaa tu kwa siku chache.

Inamaanisha nini iwapo chanjo ina uidhinishaji wa FDA?

Kwa ajili ya uidhinishaji kamili, FDA hukagua data kwa kipindi kirefu cha wakati ikilinganishwa na uidhinishaji wa matumizi ya dharura. Ili chanjo iweze kupewa uidhinishaji kamili, data lazima ionyeshe kiwango cha juu cha usalama, ufaafu, na udhibiti wa ubora katika uzalishaji wa chanjo.

Uidhinishaji wa matumizi ya dharura (EUA) huruhusu FDA kufanya bidhaa kupatikana wakati dharura ya jimbo imetangazwa kabla ya kupewa leseni kamili. Azma ya EUA ni kuhakikisha kuwa watu wanaweza kupata chanjo za kuokoa maisha kabla ya uchanganuzi wa data kwa muda mrefu. Hata hivyo, EUA bado inahitaji ukaguzi wa data za kimatibabu wa kina zaidi—kwa kipindi kifupi cha wakati tu. EUA yoyote itakayoidhinishwa na FDA itapigwa msasa zaidi na Scientific Safety Review Workgroup (Kikundi cha Kazi cha Ukaguzi wa Usalama wa Kisayansi), kama sehemu ya Western States Pact (Muungano wa Majimbo ya Magharibi) (Kiingereza pekee).

Western States Pact ni nini?

Mnamo Oktoba 2020, Washington ilijiunga na Oregon, Nevada, Colorado na California kuunda Kikundi cha Kazi cha Ukaguzi wa Usalama wa Kisayansi cha Majimbo ya Magharibi (Muungano wa Majimbo ya Magharibi) kukagua usalama na ufaafu wa chanjo za COVID-19 baada ya kuidhinidhwa na FDA. Kikundi hiki cha kazi kina toa safu nyingine ya ukaguzi wa mtaalamu kuhusu usalama wa chanjo.

Jopo linajumuisha wataalamu walioteuliwa na majimbo yote wanachama, na wanasayansi wanaotambuliwa kitaifa katika utoaji chanjo na afya ya umma. FDA ikiidhinisha chanjo kwa ajili ya matumizi ya dharura, jopo hilo linakagua data zote zinazopatikana kwa umma pamoja na ukaguzi wa muungano, na kuwasilisha ripoti. Mchakato huu ulifanyika katika chanjo tatu ambazo tuko nazo kwa sasa katika jimbo la Washington, na utafanyika kwa chanjo zote za COVID-19 ambazo zimepewa Emercenty Use Authorization (EUA) baadaye. Soma matokeo ya Western States Scientific Safety Review Workgroup:

Je, chanjo ya COVID-19 itafanya kazi vipi katika mwili wangu?

Tazama video hii kwenye jinsi ambavyo chanjo zinafanya kazi mwilini mwako (Kiingereza pekee).

Chanjo za mRNA (Chanjo za COVID-19 za Pfizer na Moderna)

Chanjo mbili kati ya chanjo zinazopatikana zinaitwa chanjo za messenger RNA (mRNA).

Chanjo za mRNA hufunza seli zako kuunda protini ya kipande cha virusi vya korona isiyoweza kukudhuru. Mfumo wako wa kingamaradhi huona kuwa protini hiyo si ya hapo, na mwili wako unaanza kuunda kingamwili. Kingamwili hizi hukumbuka jinsi ya kupigana na COVID-19 ukiambukizwa katika siku zijazo. Ukipewa chanjo, unajenga kingamaradhi ya COVID-19 bila kuhitaji kupata ugonjwa huo. Mara tu imefanya kazi yake, mRNA huyeyuka kwa haraka na mwili huisafisha baada ya siku chache.

Chanjo za vekta ya virusi (Chanjo ya COVID-19 ya Johnson & Johnson)

Mojawapo ya chanjo za COVID-19 inaitwa chanjo ya vekta ya virusi.

Chanjo za vekta zimeundwa na toleo la wikendi la vieusi (virusi tofauti kando na ile inayosababisha COVID-19). Chanjo hizi hufunza seli zako kuunda protini ya kipande cha virusi vya korona isiyoweza kukudhuru. Mfumo wako wa kingamaradhi huona kuwa protini hiyo si ya hapo, na unaanza kuunda kingamwili. Mwili wako hujifunza jinsi ya kukukulinda dhidi ya maambukizo ya COVID-19 katika siku za baadaye, bila wewe kuhitaji kuwa mgonjwa.

Chanjo ya vekta tuliyo nayo ni dozi moja. Kimsingi inachukua karibu wiki mbili baada ya dozi ili kupata ulinzi kamili.

Chanjo za kitengo kidogo cha protini (Chanjo ya COVID-19 ya Novavax)

Mojawapo ya chanjo za COVID-19 zilizoidhinishwa na Food and Drug Administration (FDA, Utawala wa Chakula na Dawa) ni chanjo ya kitengo kidogo cha protini. Chanjo za kitengo kidogo cha protini zina vipande vya virusi (protini) ambavyo husababisha COVID-19 (vimetengenezwa bila kutumia virusi vyovyote viliyo hai) pamoja na nyongeza inayolenga kusaidia chanjo kufanya kazi vizuri zaidi katika mwili. Mara tu mfumo wako wa kingamwili umejua jinsi ya kuitikia protini ya haraka, utaweza kujibu kwa haraka kwa virusi vyenyewe na kulinda mwili wako dhidi ya COVID-19. Chanjo za vitengo vidogo haziwezi kusababisha maambukizo na virusi ambavyo husababisha COVID-19 na haziingiliani na DNA yako.

Chanjo ya virusi ya kitengo kidogo inayopatikana ni chanjo ya dozi mbili. Kimsingi huwa inachukua karibu wiki mbili baada ya dozi ya pili ili kulindwa kamili.

Wakati mwingine chanjo inaweza kuleta homa kiasi au dalili zinazofanana na za homa, lakini hizi si uchungu.

Kwa taarifa zaidi, tazama rasilimali hizi: Picha ya haraka ya Chanjo za COVID-19 na Chanjo za COVID-19: Jambo la Kujua.

Wakati watu wa kutosha katika jumuiya wanaweza kupigana na virusi vya korona, havitakuwa na popote pa kuenda. Hii inamaanisha tunaweza kusimamisha msambao kwa haraka na kuwa karibu kiasi na kumaliza janga hili la tandavu.

Je, chanjo za COVID-19 huwa zinatengenezwa aje?

Video hii fupi inafafanua jinsi ambavyo chanjo za COVID huwa zinatengenezwa (Kiingereza pekee).

Chanjo ya mRNA ni nini?

messenger RNA, au chanjo ya mRNA ni aina mpya ya chanjo. chanjo za mRNA zinafunza seli zako jinsi ya kuunda "protini kali" isiyoweza kukudhuru. Protini hiyo ndiyo huwa unaona kwenye sehemu ya virusi vya korona. Mfumo wako wa kingamaradhi huona kuwa protini hiyo si ya hapo na mwili wako utaanza kuunda mwitikio wa kingamaradhi na kutengeneza kingamwili. Hii inafanana na jambo ambalo hufanyika tukipata maambukizo ya COVID-19 "kiasili". Mara tu imefanya kazi yake, mRNA huyeyuka kwa haraka na mwili huisafisha baada ya siku chache.

Ijapokuwa tumetumia mRNA kwa aina nyingine za matibabu na utunzaji wa wanyama hapo awali, kuunda chanjo kwa kutumia njia hii ni hatua kubwa mbele katika sayansi na inaweza kumaanisha chanjo za baadaye zinaweza kuundwa kwa urahisi zaidi.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu jinsi ambavyo chanjo za mRNA hufanya kazi kwenye tovuti ya CDC (Kiingereza pekee)

Chanjo ya vekta ya virusi ni nini?

Aina hii ya chanjo hutumia toleo dhaifu la virusi tofauti ("vekta") ambayo hupatia seli zako maelekezo. Vekta huingia kwenye seli na kutumia mashine ya seli kuunda kipande cha protini ya COVID-19 ambacho hakina madhara yoyote. Seli hiyo huonyesha protini hiyo kwenye sehemu yake, na mfumo wako wa kingamwili utaona kuwa haifai kuwa hapo. Mfumo wako wa kingamwili utaanza kuunda kingamaradhi na kuwezesha seli nyingine za kingamwili ili kupigana na kile ambacho inadhani ni maambukizo. Mwili wako hujifunza jinsi ya kukukulinda dhidi ya maambukizo ya COVID-19 katika siku za baadaye, bila wewe kuhitaji kuwa mgonjwa.

Chanjo ya kitengo kidogo cha protini ni nini?

Mojawapo ya chanjo za COVID-19 zilizoidhinishwa na Food and Drug Administration (FDA, Utawala wa Chakula na Dawa) ni chanjo ya kitengo kidogo cha protini. Chanjo za kitengo kidogo cha protini zina vipande vya virusi (protini) ambavyo husababisha COVID-19 (vimetengenezwa bila kutumia virusi vyovyote viliyo hai) pamoja na nyongeza inayolenga kusaidia chanjo kufanya kazi vizuri zaidi katika mwili. Mara tu mfumo wako wa kingamwili umejua jinsi ya kuitikia protini ya haraka, utaweza kujibu kwa haraka kwa virusi vyenyewe na kulinda mwili wako dhidi ya COVID-19. Chanjo za vitengo vidogo haziwezi kusababisha maambukizo na virusi ambavyo husababisha COVID-19 na haziingiliani na DNA yako.

Kisaidizi ni nini?

Kisaidizi katika Novavax ndiyo nyongeza inayolenga kusaidia kuhimiza mwitikio wa kingamwili ya mwili.

Kuna viambato gani katika chanjo?

Viambato katika chanjo za COVID-19 chanjo ni kawaida sana kwa chanjo. Zina viambato amilifu vya mRNA au virusi vya adeno vilivyorekebishwa pamoja na viambato vingine kama mafuta, chumvi, na sukari zinazolinda kiambato amilifu, kuisaidia kufanya kazi vizuri kwa mwili, na kulinda chanjo wakati wa uhifadhi na usafirishaji.

Chanjo ya COVID-19 ya Novavax ni chanjo ya kitengo kidogo cha protini iliyo na nyongeza, pamoja na mafuta na sukari za kusaidia chanjo kufanya kazi vizuri katika mwili. Chanjo hiyo haitumii mRNA.

Chanjo za Pfizer, Moderna, Novavax na Johnson and Johnson hazina seli za binadamu (ikijumuisha seli za kijusi), virusi vya COVID-19, mpira, vifaa vya kuhifadhi, au bidhaa yoyote kutoka kwa mnyama ikijumuisha bidhaa za nyama ya nguruwe. Chanjo hizi hazikuzwi kwenye mayai na hazina bidhaa zozote za mayai.

Tazama ukurasa huu wa wavuti wa Swali na Jibu; kutoka Children's Hospital of Philadelphia (Kiingereza pekee) kwa maelezo zaidi kuhusu viambato. Unaweza pia kupata orodha kamili za viambato katika karatasi za ukweli za Pfizer (Kiingereza pekee), Moderna (Kiingereza pekee), na Johnson & Johnson (Kiingereza pekee).

Je, chanjo ya Johnson & Johnson ina tishu ya kijusi?

Chanjo ya COVID-19 ya Johnson & Johnson iliundwa kwa kutumia teknolojia sawa na chanjo nyingine nyingi. Haina sehemu za kijusi au seli za kijusi. Kipande kimoja cha chanjo kimeundwa ndani ya nakala za seli zilizoundwa ndani ya maabara ambazo asili yao ni mimba ya kuavya iliyofanyika zaidi ya miaka 35 iliyopita. Tangu wakati huo, laini za seli kwa ajili ya chanjo hizi zimedumishwa kwenye maabara na hakuna vyanzo zaidi vya seli za kijusi vinatumika kutengeneza chanjo hizi. Hii inaweza kuwa taarifa mpya kwa baadhi ya watu. Hata hivyo, chanjo ya tetekuwanga, surua, na homa ya manjano A, zimeundwa kwa njia sawa.

Je, chanjo ya COVID-19 husababisha utasa?

Hakuna ushahidi wa kisayansi kuwa chanjo zinasababisha utasa. Chanjo ikiingia mwilini mwako, inafanya kazi na mfumo wako wa kingamwili ili kuunda kingamaradhi za kupigana na virusi vya korona. Mchakato huu hauingiliani na viungo vyako vya uzazi.

Centers for Disease Control and Prevention (CDC), American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG), na Society for Maternal-Fetal Medicine (SMFM) (Kiingereza pekee) inapendekeza chanjo ya COVID-19 kwa watu wajawazito, wanaonyonyesha, au wanaopanga kuwa wajawazito. Watu wengi waliopata chanjo dhidi ya COVID-19 wameweza kupata ujauzito au kuzaa watoto walio na afya.

Kwa sasa hakuna ushahidi unaonyesha kuwa chanjo zozote, zikiwemo chanjo za COVID-19, husababisha matatizo ya nguvu za kiume. Utafiti mdogo wa hivi karibuni wa wanaume 45 walio na afya nzuri (Kiingereza pekee) waliopokea chanjo ya COVID-19 ya mRNA (yaani, Pfizer-BioNTech au Moderna) uliangalia sifa za manii, kama idadi na miondoko, kabla na baada ya chanjo. Watafiti hawakupata mabadiliko yoyote makubwa katika sifa hizi za manii baada ya chanjo.

Joto kali kutoka kwa maradhi limehusishwa na upungufu wa muda mfupi katika uzalishaji wa manii katika wanaume wenye afya nzuri. Ijapokuwa homa inaweza kuwa madhara ya muda ya chanjo ya COVID-19, hakuna ushahidi wa sasa kuwa homa baada ya chanjo ya COVID huathiri uzalishaji wa manii.

Tazama Maelezo ya CDC kuhusu Chanjo za COVID-19 kwa watu ambao wangependa kupata mtoto (Kiingereza pekee) kwa maelezo zaidi. Unaweza pia kuona ukurasa wa wavuti wa CDC kuhusu Chanjo za COVID-19 (Kiingereza pekee) ili kupata ukweli kuhusu chanjo hizo.

Aina gani za dalili ni kawaida baada ya kupokea chanjo?

Sawa na chanjo nyingine za kidesturi, madhara ya kawaida zaidi ni maumivu ya mkono, uchovu, maumivu ya kichwa, na maumivu ya misuli.

Dalili hizi ni ishara kuwa chanjo inafanya kazi. Katika majaribio ya Pfizer na Moderna, madhara hizi zilitokea mara kwa mara ndani ya siku mbili baada ya kupata chanjo, na kukaa kwa karibu siku moja. Madhara yalionekana kuwa za kawaida zaidi baada ya dozi ya pili ikilinganishwa na dozi ya kwanza. Katika majaribio ya kimatibabu ya Johnson & Johnson, madhara yalikaa kwa wastani wa siku moja hadi mbili.

Kwa chanjo zote tatu, watu walio na umri wa zaidi ya 55 walikuwa na uwezekano mdogo wa kuripoti madhara ikilinganishwa na watu wadogo.

Unaweza kuona baadhi ya uvumi kuhusu madhara yasiyo kweli mtandaoni au kwenye mtandao wa kijamii. Hakikisha wakati wowote umeona dai kuhusu madhara huwa unaangalia chanzo cha dai hilo.

Ni nini hufanyika nikiwa mgonjwa baada ya kupata chanjo ya COVID-19?

Kama chanjo nyingine za kawaida, chanjo ya COVID-19 mara nyingi huleta madhara; kama vile uvimbe katika mkono, homa, maumivu ya kichwa, au uchovu baada ya kupewa chanjo. Hizi ni dalili kuwa chanjo inafanya kazi. Jifunze zaidi kuhusu madhara yanayoweza kutokea baada ya kupata chanjo ya COVID-19.

Ukiwa mgonjwa baada ya kupata chanjo, unafaa kuripoti tukio hilo baya kwenye Vaccine Adverse Event Reporting System (VAERS, Mfumo wa Kuripoti Tukio Baya la Chanjo) (Kiingereza pekee). "Tukio kali" ni tatizo lolote la kiafya au "madhara" yoyote ambayo hutokea baada ya chanjo. Kwa maelezo zaidi kuhusu VAERS, angalia "VAERS ni Nini?" hapo chini

VAERS ni Nini?

VAERS ni mfumo wa onyo la mapema unaongozwa na Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Ugonjwa (CDC) na Utawala wa Chakula na Dawa (FDA). VAERS zinaweza kusaidia kugundua matatizo ambayo huenda yanahusiana na chanjo.

Mtu yeyote (mtoaji huduma ya afya, mgonjwa, mtoaji utunzaji) anaweza kuripoti miitikio mikali ya VAERS inayoweza kutokea (Kiingereza pekee).

Kuna vizuizi kwenye mfumo huo. Ripoti ya VAERS haimaanishi kuwa chanjo hiyo ilisababisha mwitikio au matokeo. Inamaanisha tu kuwa chanjo ilifanyika kwa haraka.

VAERS imeundwa ili kuwasaidia wanasayansi kugundua mielekeo au sababu za wao kuchunguza shida inayoweza kutokea. Si orodha ya matokeo ya chanjo yaliyoidhinishwa.

Ukiripoti kwenye VAERS, unasaidia CDC na FDA kutambua wasiwasi wa afya unaoweza kutokea na kuhakikisha kuwa chanjo ziko salama. Suala lolote likitokea, watachukua hatua na kuarifu wahudumu wa afya kuhusu masuala yanayoweza kutokea.

Je, naweza kupata chanjo ya COVID-19 iwapo nimekuwa na COVID-19?

Ndiyo, Advisory Committee on Immunization Practices (ACIP, Kamati ya Ushauri kuhusu Matendo ya Chanjo) inapendekeza mtu yeyote ambaye amekuwa na COVID-19 akapate chanjo.

Data inaonyesha kuwa si kawaida kuambukizwa tena na COVID-19 katika siku 90 baada ya kuambukizwa, hivyo unafaa kuwa na kinga (inaitwa kingamwili asilia). Hata hivyo, hatujui muda ambao kingamwili asilia itakaa.

Watu ambao kwa sasa wana COVID-19 wanafaa kusubiri kupokea chanjo hadi watakapohisi vizuri na kipindi chao cha kujitenga kimeisha.

Watu ambao hivi karibuni walikuwa karibu na mtu aliyeambukizwa na COVID-19 wanafaa pia kusubiri hadi baada ya kipindi chao cha karantini, iwapo wanaweza kuingia karantini salama mbali na watu wengine. Iwapo kuna hatari ya juu wanaweza kuambukiza upya wengine, wanaweza kupata chanjo wakati wa kipindi cha karantini yao ili kuzuia kusambaza ugonjwa.

Tafadhali rejelea ukurasa wetu wa Kutengwa na Karantini ya COVID-19 ili kupata miongozo ya kujitenga na karantini.

Je, naweza kupata chanjo ya COVID-19 iwapo nimekuwa na mzio wa chanjo katika siku zilizotangulia?

Chanjo haifai kupewa watu walio na historia ya mizio mikali inayojulikana, kama vile mmenyuko wa mzio, kwa dozi ya awali ya mRNA au chanjo ya vekta ya virusi, au kiambato chochote cha Chanjo za COVID-19 za Pfizer-BioNTech/Comirnaty (Kiingereza pekee), Moderna/Spikevax (Kiingereza pekee), au Johnson & Johnson–Janssen (Kiingereza pekee).

Watu ambao wamekuwa na mzio mkali kwa chanjo nyingine au tiba za kudungwa sindano bado wanaweza kupokea chanjo hiyo. Hata hivyo, watoaji wanafaa kufanya tathmini ya hatari na kuwashauri kuhusu hatari zinazoweza kutokea. Iwapo mgonjwa ataamua kupata chanjo, mtoaji anafaa kuwachunguza kwa dakia 30 ili kuangalia iwapo kuna mizio yoyote ya mara moja.

Advisory Committee on Immunization Practices (ACIP) inapendekeza kuwa watoaji wachunguze wagonjwa wengine wote kwa angalau dakika 15 baada ya kupokea chanjo ili kufuatilia mzio. Tazama mambo ya kuzingatiwa kwa muda kuhusu chanjo za mRNA (Kiingereza) kutoka kwa ACIP ili kupata maelezo zaidi.

Mahitaji ya Chanjo

Je, Chanjo ya COVID-19 Inahitajika?

Itakuwa chaguo lako kama utapata chanjo ya COVID-19, lakini baadhi ya waajiri, vyuo, na vyuo vikuu vinahitaji chanjo.

Washington kwa sasa inahitaji chanjo ya COVID-19 kwa:

Waajiriwa hawa wanahitajika kupokea chanjo kamili dhidi ya COVID-19 (angalau wiki mbili baada ya kukamikisha misururu ya chanjo) kufikia Oktoba tarehe 18, 2021. Mahitaji hayo yanajumuisha watoa zabuni, watu wa kujitolea, na nafasi zozote nyingine inayofanya kazi katika mipangilio hii.

Iwapo upo kwenye mojawapo ya vikundi hivi au mwajiri wako au shule yako inahitaji chanjo ya COVID-19, ongea na idara zako za rasilimali za kibinadamu, mwajiri, au shule ili kujua jambo la kufanya. Idara ya Afya haihusiki na sera ya mwajiri au chuo/chuo kikuu.

Chanjo itasaidia kulinda wewe na wengine wa karibu na wewe dhidi ya kupata COVID-19, na tunakuhimiza uongee na daktari wako kuhusu manufaa hayo.

Je, mahitaji ya Chanjo ya COVID-19 kwa waajiriwa wa K-12 ni gani?

Mnamo Agosti tarehe 18, 2021, Gavana Inslee alitangaza mwelekeo unaowahitaji waajiriwa wote wa chule za umma na za kibinafsi za K–12 kupokea chanjo kamili dhidi ya COVID-19, au kupata barua ya kidini au kimatibabu inayowaruhusu kutopata chanjo kufikia Oktoba tarehe 18, 2021.

Amri hiyo inatumika kwa waajiriwa wote katika mazingira ya elimu (Kiingereza pekee), ikijumuisha:

 • Waajiriwa na wazabuni wanaofanya kazi na shule za kibinafsi za K-12, shule za umma za wilaya za K-12, shule za mkataba, wilaya wa huduma ya elimu (amri hiyo haitumiki kwa shule au wanafunzi wa maeneo ya elimu ya kikabila katika jimbo),
 • Wahudumu wa sehemu za kuwatunza mtoto na elimu ya mapema wanaowahudumia watoto kutoka kwa kaya mbalimbali, na
 • Waajiriwa katika elimu ya juu.

Kwa maelezo zaidi, tazama mahitaji ya chanjo ya COVID-19 kwa waajiriwa wa shule ya K-12: maswali yanayoulizwa mara kwa mara (PDF) (Kiingereza pekee) (Ofisi ya Mkubwa wa Afya wa Kutoa Maagizo kwa Umma).

Nitakosaje kujumuishwa kwenye mahitaji ya chanjo?

Ikiwa mwajiri wako au chuo/chuo kikuu chako kinahitaji chanjo ya COVID-19, au unahitajika kuwa na chanjo hiyo kwa mujibu wa tamko la Gavana Jay Inslee la Agosti tarehe 9 (Kiingereza pekee) au tamko la Agosti tarehe 18 (Kiingereza pekee), unafaa kuwasiliana na mwajiri wako au chuo/chuo kikuu chako ili kujua wanavyokusanya uthibitisho wa chanjo, ikiwa wana sera ya kujiondoa, na kile ambacho ungehitaji kujiondoa. Idara ya Afya haihusiki na sera ya mwajiri au chuo/chuo kikuu.

Huhitaji fomu ya kutojumuishwa kutoka kwa Department of Health (DOH, Idara ya Afya) kwa ajili ya chanjo ya COVID-19. DOH haina fomu za kutojumuishwa za chanjo ya COVID-19. Certificate of Exemption (COE, Cheti cha Kutojumuishwa) cha jimbo la Washington ni cha wazazi/waleti tu wanaotaka kutowajumuisha watoto wako kwenye chanjo inayohitajika kwa watoto wa shule za K-12, chekechea na utunzaji wa mtoto. Kwa sasa, Washington haihitaji chanjo ya COVID-19 ili watoto waweze kuhudhuria shule au utunzaji wa mtoto, hivyo haijumuishwi kwenye COE.

Shule na Utunzaji wa Watoto

Je, watu walio na umri wa chini ya Miaka 18 wanaweza kupata chanjo?

Wakati huu, chapa za chanjo ya COVID-19 ya Pfizer-BioNTech (Pfizer) na chanjo ya Moderna zimeidhinishwa kwa watoto walio na umri wa miezi 6 na zaidi.

Vijana walio na umri wa chini ya miaka 17 wanaweza kuhitaji ridhaa kutoka kwa mzazi au mlezi (Kiingereza pekee) ili kupata chanjo, isipokuwa wamekubaliwa chini ya sheria. Tembelea ukurasa wetu wa wavuti kuhusu Vaccinating Youth (Kuwapa Vijana Chanjo) kwa maelezo zaidi.

Angalia na kliniki ya chanjo kuhusu mahitaji yao ya kuonyesha uthibitisho wa ridhaa ya mzazi au wamekubaliwa chini ya sheria.

Je, jimbo litahitaji chanjo ya COVID-19 ili kuweza kuingia katika shule ya K-12?

Washington State Board of Health (Bodi ya Afya katika Jimbo la Washington), si Department of Health (Idara ya Afya), ina mamlaka ya kuunda mahitaji ya chanjo kwa watoto waliopo katika shule za K-12 Revised Code of Washington (RCW, Msimbo wa Washington Uliorekebishwa) 28A.210.140. Hakuna mahitaji ya chanjo ya COVID-19 katika shule au kituo cha kutunzia mtoto kwa wakati huu.

Je, mtoto wangu anaweza kupata chanjo nyingine huku wakipata chanjo yao ya COVID-19?

Watu sasa wanaweza kupata chanjo ya COVID-19 ndani ya siku 14 baada ya chanjo nyingine, ikiwa na hata siku hiyo hiyo.

Je, kutakuwa na uhuru wowote katika mahitaji ya chanjo za shule kwa mwaka wa shule wa 2021-2022 kwa sababu ya janga la COVID-19?

Bodi ya Afya katika Jimbo inaamua ikiwa kunafaa kuwa na mabadiliko kwenye mahitaji ya chanjo ya shule. Kwa sasa, mahitaji ya chanjo za shule yatasalia tu. Watoto watahitaji kutimiza mahitaji ya chanjo kabla ya kuweza kuhudhuria siku ya kwanza shuleni.

Maisha baada ya Chanjo

Kupokea chanjo kamili kuna maana gani?

Mtu anakuwa amepokea chanjo kamili wiki mbili baada ya kupokea dozi zote zilizopendekezwa katika misururu ya msingi ya chanjo yao ya COVID-19.

Mtu anakuwa amepokea chanjo zote za COVID-19 iwapo wamepokea dozi zote zilizopendekezwa katika misururu ya msingi na busta zote wanapostahiki.

Nafaa kufanya nini sasa kwa kuwa nimepokea chanjo kamili?

Mara tu umepewa chanjo kamili, unafaa:

Ikiwa nimepokea chanjo kamili ya COVID-19, bado nitahitaji kuchukua tahadhari nyingine?

Hata kama umepewa chanjo kamili, bado unafaa:

 • Kuwa "aliyepokea chanjo zote" kwa kupata dozi yako ya busta ili kupata kinga bora zaidi.
 • Heshimu kanuni za chumba. Majiji, kaunti, biashara, matukio na kumbi bado huenda zikahitaji barakoa au ithibati ya chanjo au kipimo kinachoonyesha hujaambukizwa.
 • Pata kupimwa ikiwa unapitia dalili ya COVID-19.
 • Ongeza WA Notify kwenye simu yako mahiri ili ikuarifu ikiwa huenda umekuwa na mfiduo wa COVID-19 na kuwaarifu wengine bila kutaja jina lako ikiwa utapatikana na maambukizo. WA Notify ni ya kibinafsi kabisa na haijui wewe ni nani au haifuatilii pahali unapoenda.
 • Vaa barakoa inayokutoshea vizuri katika mazingira ya umma yenye umati wa watu ndani ya nyumba ili kupata kinga bora zaidi.
 • Fuata mapendekezo ya usafiri ya Centers for Disease Control and Prevention (CDC, Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa) na idara ya afya.
 • Tahadhari baada ya kuwa na mfiduo wa COVID-19 ambao huenda ulitokea:
  • Ikiwa bado hujapokea busta na umemaliza miezi 5 au zaidi baada ya kupokea (Moderna/Pfizer) au miezi 2 baada ya kupokea (Johnson & Johnson) ili kukamilisha misururu yako ya chanjo za msingi, karantini kwa siku 5 baada ya mfiduo kufuatia utumiaji kamili wa barakoa kwa siku 5 za zaida.
  • Ikiwa ulipokea busta yako, huhitaji kuingia karantini baada ya mfiduo, lakini unafaa kuvaa barakoa kwa siku 10 baada ya mfiduo.
Je, watu ambao wamepokea chanjo na wale hawajapokea chanjo kutoka kaya tofauti wanaweza kutembeleana?

Inategemea. Ikiwa mojawapo ya kaya hizo ina watu walio katika hatari ya juu ya maradhi makali ya COVID-19 (Kiingereza pekee), basi unafaa kutembelea ndani na nje ya nyumba huku madirisha yakiwa yamefunguliwa, umevaa barakoa inayokutoshea vizuri, na unakaa mbali na wengine (angalau futi 6 / mita 2).

Ikiwa hakuna watu walio katika hatari ya juu katika mojawapo ya kaya, basi kutembeleana nje ya nyumba au mazingira ya kibinafsi ya ndani bila kuvaa barakoa ina hatari ya chini ya kusambaza COVID-19.

Na ikiwa watu wengine katika kaya yangu wamepokea chanjo kamili na wengine bado?

Ikiwa tu baadhi ya watu katika kaya yako wamepokea chanjo kamili, unafaa kutahadhari kana kwamba kaya yako bado haijapokea chanjo. Hii inamaanisha kuwa unafaa kuvaa barakoa na kukaa umbali wa futi 6 (mita 2) mkitembeleana na watu wengine kutoka katika kaya nyingine zilizo na watu ambao wamepokea sehemu ya chanjo au hawajapokea kabisa - na uepukane na mikutano kama hiyo ikiwezekana.

Unaweza kuwatembelea watu kutoka kwa kaya moja iliyo na watu waliopokea chanjo kamili kwa wakati mmoja almuradi hakuna mtu katika kaya yako aliye katika hatari ya maradhi makali ya COVID-19.

Je, naweza kukusanyika na kikundi kikubwa ikiwa sote tumepokea chanjo?

Watu waliopewa chanjo kamili ambao pia wamepokea chanjo zote wanazostahiki, wamelindwa vizuri sana dhidi ya COVID-19. Mikutano ni salama kati ya watu waliopokea chanjo kamili.

Tafadhali kumbuka kuwa baadhi ya watu huenda wasihisi sawa kuvaa baajoa - hata katika mazingira ya chini zaidi. Wengine huenda hawataki kukumbatiwa na kusalimiana kwa mkono. Na hio ni sawa. Kila mtu anaanza kuzoea hali mpya ya kawaida na sisi site tunataka mkae salama na kuwalinda wapendwa wengu.

Nitahitaji kuonyesha uthibitisho wa chanjo?

Unaweza kuhitaji kuonyesha kuwa umepokea chanjo ya COVID-19 katika baadhi ya maeneo, biashara au katika matukio maalum.

Hivyo kuhudumia kadi yako ya chanjo kama cheti cha kuzaliwa au waraka mwingine rasmi! Piga picha yake na kisha kuihifadhi nyumbani. Soma zaidi kuhusu kazi za chanjo na rekodi za chanjo.

Je, iwapo sijapokea chanjo zangu zote zote za?

Ikiwa hujapokea chanjo zako zote za COVID-19:

 • Tafuta chanjo ya COVID-19 ya bila malipo karibu nawe!
 • Hakikisha kuvaa barakoa inayokutoshea vizuri katika mazingira ya umma yenye umati wa watu ndani ya nyumba.
 • Pata kipimo cha COVID-19 ikiwa unaona dalili
 • Ikiwa ulikuwa na COVID-19, ingia karantini kwa siku 5 baada ya mfiduo kufuatia utumiaji kamili wa barakoa kwa siku 5 za ziada. Hakikisha kuwa umepimwa siku ya 5 baada ya mfiduo.
 • Ukisafiri, pata kipimo cha COVID-19 kabla ya na baada ya kusafiri.
 • Ongeza WA Notify kwenye simu yako mahiri ili ikuarifu ikiwa huenda umekuwa na mfiduo wa COVID-19 na kuwaarifu wengine bila kutaja jina lako ikiwa utapatikana na maambukizo. WA Notify ni ya kibinafsi kabisa na haijui wewe ni nani au haifuatilii pahali unapoenda.
Je, bado naweza kuugua COVID-19 baada ya kupata chanjo?

Ni bahati mbaya, lakini kuna nafasi kidogo. Chanjo zinafanya kazi sana, lakini si 100%. Ukiwa na dalili za COVID-19 (Kiingereza pekee), unafaa kukaa mbali na wengine na kuwasiliana na mhudumu wa afya. Wanaweza kupendekeza kipimo cha COVID-19.

Kwa maelezo kuhusu COVID-19, tafadhali tazama Maelezo ya Kipimo.

Je, naweza kusambaza COVID-19 baada ya kupata chanjo?

Maambukizo hufanyika tu katika sehemu ndogo ya watu ambao wamepokea chanjo kamili, na wakapokea dozi yao ya busta. Hata hivyo, watu waliopokea chanjo zote za COVID-19 ambao huambukizwa COVID-19 wanaweza kusambaza virusi kwa wengine.

Nafaa kufanya nini ikiwa nina mfiduo wa COVID-19?

Ikiwa umepokea chanjo zote na pia umepokea busta yako (chanjo zote), huhitaji kuingia karantini, lakini unafaa kuvaa barakoa kwa siku 10 baada ya mfiduo na kipimo cha COVID-19 siku ya 5 baada ya mfiduo. Ikiwa miezi 6 au zaidi imepita baada ya kupokea (Moderna/Pfizer) au miezi 2 baada ya kupokea (Johnson & Johnson) ili kukamilisha misururu yako ya chanjo za msingi, na bado hujapokea dozi ya busta, ni lazima uingie karantini kwa siku 5, na kisha kufuatwa na utumiaji wa barakoa kwa siku 5 zaidi. Kila mtu anafaa kupimwa siku ya 5 baada ya mfiduo, bila kujali hali yao ya chanjo.

Nawezaje kudhibiti msongo wa mawazo na mfadhaiko kuhusu COVID-19?

Tunafahamu kuwa janga linaweza kuathiri afya ya kimwili na kiakili. Hauko peke yako. Watu wengi Washington wanakabiliana na msongo wa mawazo na mfadhaiko unaohusiana na dhiki ya kifedha na ajira, kufungwa kwa shule, kujitenga kijamii, wasiwasi wa afya, huzuni na kufiwa, na zaidi. Hii inajumuisha mfadhaiko zaidi unaoweza kuja na kurejea kwa shughuli za umma.

Hizi hapa ni baadhi ya rasilimali zinazoweza kusaidia kudhibiti msongo wa mawazo na mfadhaiko:

 • Piga simu kwenye laini ya Washington Listens kupitia 833-681-0211 kwa ajili ya msaada na rasilimali kuhusu msongo wa mawazo unaohusiana na COVID
 • Ikiwa upo kwenye hali ya hatari:
 • Tumia Hali ya Kujali (Kiingereza pekee) ili kusikiliza, kujifunza, kushiriki na kuunganisha kuhusu ustawi na afya ya kiakili.
 • Tembelea ukurasa wetu wa Afya ya Kiakili (Kiingereza Pekee) ili kupata rasilimali zaidi.

Kiongeza Nguvu Chanjo na Dozi za Ziada

Kuna tofauti gani kati ya dozi ya ziada ya COVID-19 na kiongeza nguvu chanjo?

Dozi ya ziada (inajulikana pia kama dozi ya tatu) ni ya watu walio na kingamwili dhaifu. Wakati mwingine watu walio na kingamwili dhaifu hawajengi kinga ya kutosha mara yao ya kwanza ya kupokea chanjo kamili. Hii ikifanyika, kupata dozi nyingine ya chanjo kunaweza kuwasaidia kujenga kinga zaidi dhidi ya ugonjwa huo.

Kiongeza nguvu inarejelea dozi ya chanjo ambayo inapewa mtu aliyejenga kinga ya kutosha baada ya chanjo, lakini kinga hiyo ilipungua baada ya muda (hii inaitwa kufifisha kingamwili). Hii ndiyo sababu huwa unapewa kiongeza nguvu ya pepopunda kila baada ya miaka 10, kwa sababu kinga kutoka kwa misururu ya chanjo ya pepopunda tangu utotoni hufifia baada ya muda.

Tafadhali kagua miongozo ya Centers for Disease Control and Prevention (CDC, Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa) kwa ajili ya watu walio na kingamwili duni au tembelea tovuti ya DOH.

Ni nani anafaa kupata dozi ya ziada ya chanjo ya COVID-19?
Haddii aad qaadatay… Cidda ay tahay iney qaadato tallaalka xoojinta ah Goorta ay tahay in la qaato tallaalka xoojinta ah Tallaalka xoojinta ee la qaadanayo Ma qaadan karaa kuurada xoojisada tallaalka ee labaad?
Pfizer-BioNTech Dadka da'doodu tahay 5 sano iyo kasii weyn Ugu yaraan 5 billood kadib dhammeystirka wareegyada koobaad

Pfizer ama Moderna ayaa la door bidaa*

Dadka da'doodu tahay 17 sano iyo kayar waxaa kaliya ay qaadan karaan tallaalka Pfizer

Dadka da'doodu kawayn tahay 50 sano iyo qaar kamid ah shaqsiyaadka difaaca jirkoodu daciifka yahay, waxay hadda qaadan karaan cirbad xoojiye ah oo ah Messenger Ribonucleic acid (mRNA, hidda sidaha) COVID-19 haddii 4 billood ama in kasii badan laga soo wareegay illaa iyo markii ay qaateen kuuradoodii ugu danbeysay.
Moderna Dadka da'doodu tahay 18 sano iyo kasii weyn Ugu yaraan 5 billood kadib dhammeystirka wareegyada koobaad Pfizer ama Moderna ayaa la door bidaa* Dadka da'doodu kawayn tahay 50 sano iyo qaar kamid ah shaqsiyaadka difaaca jirkoodu daciifka yahay, waxay hadda qaadan karaan cirbad xoojiye ah oo ah Messenger Ribonucleic acid (mRNA, hidda sidaha) COVID-19 haddii 4 billood ama in kasii badan laga soo wareegay illaa iyo markii ay qaateen kuuradoodii ugu danbeysay.
Johnson & Johnson Dadka da'doodu tahay 18 sano iyo kasii weyn Ugu yaraan 2 billood kadib dhammeystirka wareegyada koobaad Pfizer ama Moderna ayaa la door bidaa*

Dadka da'doodu kawayn tahay 50 sano iyo qaar kamid ah shaqsiyaadka difaaca jirkoodu daciifka yahay, waxay hadda qaadan karaan cirbad xoojiye ah oo ah Messenger Ribonucleic acid (mRNA, hidda sidaha) COVID-19 haddii 4 billood ama in kasii badan laga soo wareegay illaa iyo markii ay qaateen kuuradoodii ugu danbeysay.

Dadka waawayn ee qaatay tallaalkii koobaad iyo daawada xoojinta ee Johnson & Johnson’s Janssen COVID-19 ugu yaraan 4 bil kahor hadda waxay qaadan karaan daawada xoojinta ah ee labaad ayagoo isticmaalaya tallaalka hidda sidaha mRNA ee COVID-19.

*Tallaalada mRNA ayaa la door bidaa, laakiin tallaalka COVID-19 ee Johnson & Johnson ayaa weli la heli karaa haddii aadan awoodin ama aadan dooneyn inaad qaadato tallaal kale.

Tafadhali kagua miongozo ya Centers for Disease Control and Prevention (CDC, Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa) kwa ajili ya watu walio na kingamwili duni au tembelea tovuti ya DOH.

Kwa nini dozi za kuongeza nguvu ni muhimu?

Dozi za kuongeza nguvu husaidia kutoa kinga azaidi dhidi ya ugonjwa mkali kwa watu walio katika hatari ya COVID-19 kali.

Hapo awali, matumizi ya dozi za kuongeza nguvu yalipendekezwa kwa baadhi ya watu ambao walikuwa kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi mabaya ya COVID-19, lakini mapendekezo yameongezwa na kujumuisha kila mtu mwenye miaka 5 na zaidi ili kuongeza uwezo wa kujikinga dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Hii ni muhimu hasa kwa ongezeko la aina zinazosambaa zaidi na visa vya COVID-19 kuongezeka Marekani.

Chanjo za COVID-19 zilizoidhinishwa au kukubaliwa Marekani bado zinafanya kazi vizuri sana katika kupunguza hatari yako ya ugonjwa mkali, kulazwa hospitalini, na kifo kutokana na COVID-19, hata dhidi ya aina. Bado, chanjo za sasa zinaweza kuhusishwa na kupungua katika kinga kwa muda. Dozi za kuongeza nguvu zitaongeza ulinzi unaoletwa na chanjo dhidi ya COVID-19 na kusaidia kingamaradhi kudumu.

Nyenzo na Maelezo ya Ziada

Rasilimali za COVID-19 kwa vikundi maalum

Watoto na Vijana

Watu wanaonyonesha na/au Walio na ujauzito

Wahamiaji na Wakimbizi

Huwezi kutoka nyumbani

Rasilimali maalum za ziada katika jamii zinaweza kupatikana kwenye ukurasa wa Usawa wa Chanjo na Uhusiano (Kiingereza pekee).

Swali langu halikujibiwa hapa. Nawezaje kupata taarifa zaidi?

Maswali ya jumla yanaweza kutumwa kwa covid.vaccine@doh.wa.gov.