Kipimo cha COVID-19

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Tafuta Eneo la Kipimo Karibu Nami (katika Kiingereza)

Ripoti kwa urahisi matokeo yako ya kipimo cha nyumbani yanayoonyesha kuwa una maambukizo

Watu wanaonunua vifaa vya kipimo vya kununuliwa dukani na kupokea matokeo yanayoonyesha wana maambukizo wanafaa kupiga nambari ya simu ya COVID-19 ya jimbo, 1-800-525-0127 kisha kubonyeza #, mara tu wanapopokea matokeo. Nambari hiyo ya simu inapatikana Jumatatu kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku, na Jumanne hadi Jumapili (na sikukuu) saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni. Usaidizi wa lugha unapatikana.

Kwa Nini Upimwe

Kipimo kinaokoa maisha. Kipimo huwaruhusu watu kutahadhari, kama kukaa karantini, kwa wakati unaofaa ili kusimamisha kuenea kwa virusi; watu walioambukizwa bila dalili bado wanaweza kusambaza virusi. Kipimo pia husaidia maafisa wa afya ya umma kutambua na kukabiliana na mkurupuko, na kufuatilia aina mpya za virusi. Kipimo ni kijenzi muhimu katika kusaidia kurejea shughuli za kawaida.

Watafiti kutoka University of Washington na Department of Health (DOH, Idara ya Afya) waligundua kuwa kupima COVID-19 na kufuatilia kupitia WA Notify (Arifu WA) huenda ilizuia takriban visa 6,000 kutoka Desemba 2020 hadi Machi 2021.

Wakati wa Kupimwa

Jipime wakati unahisi wewe ni mgonjwa. COVID-19 ina masafa marefu ya dalili (katika Kiingereza), hivyo iwapo huhisi vizuri, ni vyema ujipime haraka iwezekanavyo.

Pima kama umekuwa na mfiduo na mtu aliyepatikana na maambukizo ya COVID-19. Pimwa mara moja iwapo una dalili. Iwapo huna dalili, subiri kwa siku tano baada ya mfiduo na kisha upumzike.

Biashara na nafasi za tukio katika Washington zinaweza kuwa na mahitaji ya kipimo na/au chanjo kabla ya kuingia kwenye jengo au tukio. Piga simu mapema au angalia tovuti yao kabla ya kuwatembelea.

Huenda ukahitaji kujipima kabla ya na/au baada ya kusafiri. Angalia mwongozo wa hivi karibuni zaidi wa Centers for Disease Control and Prevention (CDC, Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Ugonjwa) (katika Kiingereza).

Wakati unaenda kukutana na kikundi cha watu, haswa walio katika hatari ya juu ya magonjwa makali au huenda hawajapokea chanjo zao zote za COVID-19 (katika Kiingereza).

Mahali pa Kupimwa

Tovuti ya Department of Health Jimbo la WA ina orodha ya vituo vya kipimo inayopatikana katika kila kaunti, na saa za kufanya kazi pamoja na mahitaji. Kwa maelezo zaidi kuhusu vituo vya kipimo, piga 2-1-1. Vifaa vya kipimo vya kununuliwa dukani pia vinapatikana kwa kuagiza na katika famasia kwa urahisi, katika kipimo cha nyumbani.

Gharama

Watoaji wa bima sasa wafidia familia kwa hadi vipimo nane kila mwezi. Jifunze zaidi kuhusu fidia ya bima (katika Kiingereza).

Hakuna gharama zozote za kujilipia mwenyewe kwa vipimo vinavyofanywa katika kaunti au vituo vya kipimo vinafosaidiwa na jimbo. Vipimo vingi, hasa vya watu wanaopitia dalili, vinaweza kugharamiwa na bima au kupunguzwa na Department of Health.

Pia unaweza kununua vifaa vya ziada vya kipimo cha nyumbani katika wauzaji rejareja na famasia wa ndani au mtandaoni. Hakuna bima au pendekezo linalohitajika.

Aina za Vipimo

Vipimo vya sasa vinavyopatikana ni vipimo vya haraka vya antijeni, vipimo vya molekuli (vya maabara na eneo la utunzaji), na vipimo vya kujipima nyumbani. Usambazaji wa kipimo chochote maalum unatofautiana kulingana na mahitaji na uwezo wa mtengenezaji.

Jinsi Ya Kufanya Kipimo Cha Nyumbani

Ni muhimu kufuata maelekezo ndani ya kifaa cha vipimo vya haraka nyumbani ili kupata matokeo sahihi zaidi. Chapa kadhaa pia hutoa maelekezo ya video. Kwa matendo zaidi bora, angalia vidokezo vya CDC vya kipimo cha nyumbani.

Matokeo ya uwongo yanayoonyesha huna maambukizo yanaweza kutokea kwa vipimo vya haraka. Baadhi ya vifaa vya kipimo vinaweza kujumuisha vipimo viwili (unafaa kufuata maelekezo kwenye kisanduku ili kujua wakati wa kujipima).

Kwa mengi kuhusu jinsi ambavyo kipimo hufanya kazi, tembelea ukurasa wetu wa maswali yanayoulizwa mara kwa mara wa kipimo.

Jinsi Ambavyo Kipimo Hufanya Kazi

Vipimo vingi vinafanywa kutumia pamba za pua. Baadhi ya vipimo vinaweza kufanywa kwa kukusanya mate. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana kwenye ukurasa wa maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu kipimo.

Wakati wa Kuingia Karantini au Kujitenga

Huenda ukahitaji kuingia karantini au kujitenga kabla ya kufanya kipimo chako na baada ya kupokea matokeo yako. Hii itategemea hali yako ya chanjo na kama una dalili. Mwongozo wa hivi karibuni zaidi wa CDC unafafanua hali hii (katika Kiingereza). Pia unaweza kufuata mwongozo wetu kwa watu ambao wana dalili na/au walio na mfiduo wa COVID-19.

Ufuatiliaji

Kaa nyumbani kadri uwezavyo iwapo inawezekana iwapo una dalili.  Ukiambukizwa COVID-19, habari nzuri ni kuwa kuna hatua unazoweza kuchukua ili kusaidia kujilinda na kuwalinda wengine. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana hapa: Jambo la kufanya iwapo utaambukizwa.