WA Notify (Arifa ya WA) (inayojulikana pia kama Taarifa za Mfiduo wa Washington ni zana ya bila malipo unayoweza kuongeza kwenye simu yako mahiri kuwaarifu watumiaji kuhusu mifiduo ya COVID-19 ambayo huenda imetokea. Ni ya kibinafsi kabisa, haikusanyi au kushiriki maelezo yoyote ya kibinafsi, na haifuatilii mahali unapoenda.
Ninaweza kuongeza vipi WA Notify kwenye simu yangu?

Kwenye iPhone, wezesha Taarifa za Mfiduo katika Mipangilio:
-
Nenda kwenye Mipangilio (Settings)
- Telezesha chini hadi kwa Exposure Notifications
- Bofya "Washa Exposure Notifications”
- Teua United States (Marekani)
- Teua Washington
Kwa Android au iPhone, tambaza msimbo wa QR au ongeza WA Notify kwenye simu yako iwapo unatumia kifaa cha mkononi.

Inafanya kazi vipi?
Unapoamilisha WA Notify, simu yako hubadilisha misimbo nasibu isiyofahamika kwenye simu za watu ulio karibu nao ambao tayari wamewezeshwa WA Notify. Mfumo huo hutumia faragha inayohifadhi taknolojia ya Bluetooth ya Kawi ya Chini kubadilisha misimbo hii bila kutoa maelezo yoyote kukuhusu. Iwapo mtumiaji mwingine wa WA Notify ambaye umekuwa karibu naye hivi karibuni baadaye atapatikana na maambukizo ya COVID-19 na anafuata hatua za kuwaarifu wengine bila kujitambulisha, utapata taarifa. Hatua hii itakusaidia kupata huduma unayohitaji kwa haraka na pia itakusaidia kujikinga na kusambaza COVID-19 kwa watu walio karibu nawe.
Algorathim hufanya hesabu ya kutambua matukio yanayoweza kusambaza COVID-19 kutoka kwa wale walio katika umbali salama au fupi ya kutosha ambayo huhitaji kuonywa. WA Notify itakuarifu tu ikiwa huenda umekuwa karibu na mtu aliyeambukizwa. Hivyo kutopokea arifa ni habari njema.
WA Notify pia inapatikana katika lugha zaidi ya 30.

Faragha yangu inalindwa vipi?
WA Notify inategemea teknolojia ya Taarifa ya Mfiduo wa Google Apple, ambayo imeundwa ili kulinda faragha yako. Inafanya kazi kwenye mandharinyuma bila kukusanya au kufichua eneo lolote au data ya kibinafsi. WA Notify haihitaji kujua wewe ni nani au uko wapi ili kufanya kazi kwa ufanisi. Kwa kutumia vidude hivi vidogo vya Bluetooth, betri yako haiathiriwi.
Ushiriki ni wa kujitolea. Mtumiaji anaweza kuingia au kujitoa wakati wowote. Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ambavyo faragha ya mtumiaji inalindwa, tazama sera ya faragha ya WA Notify.
Taarifa hukaa vipi?
Kuna aina mbili za taarifa unazoweza kupokea. Wanaopatikana na maambukizo watapokea ujumbe wa matini wenye kiungo cha uthibitishaji na/au taarifa ibukizi. Watumiaji wa WA Notify ambao huenda walikuwa na mfiduo watapokea taarifa ya mfiduo. Jifunze zaidi kuhusu taarifa hizi na uone zinavyokaa.
Je, WA Notify husaidiaje?
Utafiti umepata kuwa watu wanavyozidi kutumia taarifa ya mfiduo, ndivyo manufaa yanakuwa makubwa. Zoezi hili likiwa limefanyika katika kaunti tatu za Jimbo la Washington linaonyesha kwamba hata idadi ndogo tu ya watu eneo lile wanaotumia WA Notify hupunguza maambukizi na hata vifo. Tukipokea chanjo na kuvaa barakoa, tunaweza kuokoa maisha. Tunaporejea kwenye matukio ya mtu mwenyewe, WA Notify ni safu ya ziada ya ulinzi. Ni kitu kimoja zaidi unachoweza kufanya ili kuhakikisha usalama wako na wa watu wengine walio karibu na wewe.
Jinsi ya kuwaarifu wengine ukipatikana na maambukizo ya COVID-19 kwa kipimo cha kibinafsi
Watumiaji wa WA Notify wanaotumia kifaa cha kipimo cha kibinafsi (kinachoitwa pia vipimo vya nyumbani) na kupatikana na maambukizo ya COVID-19 wanaweza kuomba msimbo wa uthibitisho ili kuwaarifu bila kujulikana watumiaji wengine wa WA Notify ambao huenda wamekuwa na mfiduo wa COVID-19.

Kwenye iPhone:
- Nenda kwenye Settings (Mipangillio) na ufungue Exposure Notifications (Taarifa Kuhusu kuwa hatarini mwa Kuambukizwa).
- Chagua “Share a COVID-19 Diagnosis.” (“Shiriki Utambuzi wa COVID-19.”)
- Chagua “Continue.” (“Endelea.”)
- Ukiona chaguo la kuingiza msimbo, teua "Didn’t get a code (Hukupata msimbo)? Visit WA State Dept. of Health Website.” (Tembelea Tovuti ya Idara ya Afya ya Jimbo la WA.") Usipoona chaguo la kuingiza msimbo wako, nenda kwenye hatua inayofuata.
- Ingiza nambari ya simu ya kifaa chako kinachotumia WA Notify na tarehe ya kipimo chako chanya cha COVID-19.
- Chagua “Continue.” (“Endelea.”)

Kwenye Android phone:
- Fungua WA Notify na uchague “Share your test result to help stop the spread of COVID-19” ("Shiriki matokeo ya kipimo chako ili usaidie katika kukomesha kuenea kwa COVID-19").
- Chagua “Continue (Endelea)” kisha uchague “I need a code” (“Ninahitaji msimbo”).
- Ingiza nambari ya simu ya kifaa chako kinachotumia WA Notify na tarehe ya kipimo chako chanya cha COVID-19.
- Chagua “Send Code” (“Tuma Msimbo”).
Kwa Android au iPhone, tambaza msimbo wa QR au omba msimbo wa uthibitisho iwapo unatumia kifaa cha mkononi.

Utapokea taarifa ibukizi na ujumbe mfupi wenye kiungo chako cha uthibitishaji. Unahitaji tu kudonoa taarifa au kubofya kiungo kilicho katika ujumbe mfupi ili ufuate hatua zilizo katika WA Notify ili uwajulishe watumiaji wengine bila kujulikana kuhusu ikiwa wako hatarini mwa kuambukizwa.
Ikiwa huwezi kuomba msimbo wa uthibitishaji kwenye WA Notify, unapaswa kupiga simu ya dharura ya COVID-19 ya jimbo, 1-800-525-0127, kisha ubonyeze #, na uwajulishe wafanyikazi wa simu ya dharura kwamba wewe ni mtumiaji wa WA Notify. Mfanyakazi wa nambari ya simu anaweza kukupatia kiungo cha uthibitisho unachoweza kutumia ili kuwaarifu watumiaji wengine wa WA Notify kuwa huenda wamekuwa na mfiduo.
Jinsi ya kuripoti matokeo yako ya kipimo cha kibinafsi cha COVID-19 yanayoonyesha kuwa una maambukizo
Watu wanaotumia kifaa cha kipimo cha kibinafsi (kinachoitwa pia vipimo vya nyumbani) na kupatikana na maambukizo ya COVID-19 wanaweza kuripoti matokeo yanayoonyesha wameambukizwa kwa Department of Health (DOH, Idara ya Afya), nje ya programu ya WA Notify. Kwa mwongozo wa sasa kuhusu jinsi ya kuripoti matokeo ya kipimo yanayoonyesha kuwa umeambukizwa, rejelea ukurasa wa DOH wa Kipimo cha COVID-19.
Vifaa vya kipimo cha kibinafsi Vya bila malipo vinapatikana pia kwenye Say Yes! (Sema Ndiyo!) COVID Test (Kipimo cha COVID).
Mwongozo wa ziada unaweza kupatikana kwenye rasilimali ya DOH ya Jambo la kufanya iwapo utapatikana na maambukizo ya COVID-19.
Tafadhali kumbuka: WA Notify ni zana ya taarifa ya mfiduo. Haikuundwa ili watumiaji waripoti matokeo yao ya kipimo kwa DOH. Kuripoti matokeo kwa DOH ni nje ya mfumo wa programu ya WA Notify.
Kwa nini tunahitaji kufuatilia mwasilani na WA Notify?
Kufuatilia mwasilani kumekuwa uingiliaji faafu wa afya ya umma kwa miongo. WA Notify huauni kazi hii bila kujulikana. Huu ni mfano: Ukipatikana na COVID-19, maafisa wa afya ya umma wanaweza kukupigia na kukuomba kusambaza waasilani wako wa karibu wa hivi karibuni. Huwezi kumtaja mtu ambaye humjui lakini uliketi karibu naye kwenye basi. Iwapo nyinyi nyote wawili mna WA Notify, mtu huyo asiyejulikana kwenye basi anaweza kuarifiwa kuhusu mfiduo unaowezekana na kuchukua hatua za kuzuia msambao wa COVID-19 kwa marafiki na familia. Sawa tu na chanjo na kuvaa barakoa husaidia kumaliza msambao wa COVID-19, pamoja ni faafu zaidi.
Je, nahitaji kuendelea kutumia WA Notify au naweza kuizima sasa?
Tunahimiza kila mtu kuhakikisha amewezesha WA Notify kila mara kwenye simu yao na kutoizima. Huku vizuizi vinapungua na shughuli zikirejea, WA Notify ni njia rahisi ya kuwa na safu ya ziada ya ulinzi na wewe.
Je, nahitaji WA Notify ikiwa nimepokea chanjo?
Ndiyo! Jimbo la Washington litakuwa linakabiliana na COVID-19 kwa muda. Bado tunajifunza vitu vingi kuhusu virusi hivi, kama vile muda ambao chanjo zitakuwa na ufanisi na jinsi ambavyo chanjo zinalinda dhidi ya aina mpya ya COVID-19. Hata kama hatari hiyo ni kidogo kwa watu waliopokea chanjo, tunajua kuwa watu waliopokea chanjo kamili bado wanaweza kuambukizwa na kusambaza COVID-19. Pia, tunajua kuwa kuna watu ambao bado hawajapokea chanjo. Kutokana na sababu hizi zote, tunawahimiza wakazi wote wa Washington kuwezesha WA Notify kwenye simu zao- ili kusaidia kusimamisha msambao wa COVID-19.
Unataka kusaidia kutangaza habari kuhusu WA Notify (Taarifa za WA)?
Angalia chombo cha zana cha WA Notify kwa ajili ya utumaji ujumbe kwenye mtandao wa kijamii, mabango, sampuli ya matangao ya redio na televisheni, na zaidi. Pia, waambie marafiki na familia yako. Watu wanavyozidi kutumia WA Notify, ndivyo inakuwa bora zaidi kusaidia kukulinda wewe pamoja na jumuiya yako.
Maswali mengine yanayoulizwa mara kwa mara
- Nitapataje tarehe yangu ya mfiduo katika WA Notify?
-
Kwenye iPhone:
- Nenda kwenye Settings (Mipangilio)
- Chagua Exposure Notifications (Taarifa Kuhusu Kuwa hatarini mwa Kuambukizwa) au ingiza Exposure Notifications (Taarifa Kuhusu Kuwa hatarini mwa Kuambukizwa) kwenye Upau wa Utafutaji
- Tarehe yako ya karibu ya mfiduo unaoweza kutokea itaonyeshwa chini ya "You may have been exposed to COVID-19 (Huenda umeambukizwa COVID-19)"
Kwenye Android:
- Fungua programu ya WA Notify
- Teua See Details (Tazama Maelezo) chini ya "Possible exposure reported (Mfiduo unaowezekana ulioripotiwa)"
- Tarehe yako ya karibu ya mfiduo unaoweza kutokea itaonyeshwa chini ya “Possible Exposure Date” (Tarehe ya Mfiduo Inayowezekana)"
-
Nilipokea taarifa na/au matini kutoka kwa Washington State Department of Health (DOH, Idara ya Afya ya Jimbo la Washington). Kwa nini?
-
DOH hutuma ujumbe wa matini na/au taarifa ibukizi kwa kila mtu ambao hivi karibuni walipatikana na maambukizo ya COVID-19 ili watumiaji wa WA Notify waweze kuwaarifu watumiaji wengine kwa haraka na bila kujulikana kuhusu mfiduo. Jifunze zaidi kuhusu taarifa hizi na uone zinavyokaa.
Ukipokea ujumbe wa matini na taarifa, unahitaji tu kudonoa taarifa au kubofya kwenye kiungo katika ujumbe wa matini na kufuata hatua katika WA Notify ili kuwaarifu watumiaji wengine bila kujulikana kuhusu mfiduo ambao huenda ulitokea.
-
Nilipata arifa kuhusu kuchangia data yangu ya WA Notify kwa afya ya umma. Kwa nini?
-
DOH inataka kujua jinsi WA Notify inafanya kazi vizuri ili tuweze kufanya uboreshaji wowote unaohitajika kwenye zana hiyo. Ukikubali kushiriki data yako ya WA Notify, faragha yako bado inalindwa kamili. Hakuna maelezo ya kibinafsi yatakayokusanywa au kushirikiwa na hakuna njia ya kukutambua. DOH pekee ndiyo inaweza kufikia data hii na katika kiwango cha jimbo pekee.
-
Ikiwa watumiaji wa WA Notify watakubali kushiriki data yao, ni nini itakusanywa?
-
Ukikubali kushiriki data yako, faragha yako bado inalindwa kamili. Hakuna maelezo ya kibinafsi yatakayokusanywa au kushirikiwa hivyo hakuna njia ya kukutambua. DOH pekee ndiyo inaweza kuona data hii ya kiwango cha jimbo, itakayojumuisha:
- Idadi ya watu wanaokubali kushiriki data yao kutoka WA Notify. Hii hutusaidia kujua jinsi sampuli yetu inawakilisha.
- Idadi ya Exposure Notifications zilizopokelewa na watumiaji wa WA Notify. Hii hutusaidia kuona mwelekeo katika msambao wa COVID-19.
- Idadi ya watu wanaobofya kwenye taarifa ya mfiduo. Hii hutusaidia kuchunguza jinsi watu wako tayari ili kuzingatia mapendekezo ya afya ya umma.
- Idadi ya watu waliokuwa karibu na mtu aliyepatikana na maambukizo ya COVID-19, lakini si karibu ya kutosha au kwa muda wa kutosha kuarifiwa kuhusu mfiduo. Hii hutusaidia kuzingatia kama kanuni ambayo huamua mfiduo katika WA Notify inafaa kurekebishwa.
-
Nikiwezesha WA Notify kwenye iPhone yangu, nafaa kuwasha au kuzima togoa ya "Availability Alerts (Arifa za Upatikanaji)"?
-
Kuzima ni sawa. Ijapokuwa kuwasha kumependekezwa ikiwa unasafiri nje ya jimbo la Washington kwa kipindi kirefu cha muda. Availability Alerts (Arifa za Upatikanaji) zikiwa zimewashwa, unaweza kupokea taarifa ukisafiri kwenda kwa eneo lingine linalotoa zana ya taarifa ya mfiduo inayofanana na WA Notify. Ikiwa una iPhone, unaweza kuongeza maeneo anuwai lakini eneo moja tu ndilo linaweza kuwa amilifu kwa wakati moja. Huhitaji kuondoa eneo ili kuwezesha mpya. Ikiwa una simu ya Android, unaweza kusakinisha programu za taarifa ya mfiduo kama WA Notify kutoka majimbo kadhaa, lakini programu moja pekee inayotumia teknolojia inayoendana na WA Notify ndiyo inaweza kuwa amilifu kwa wakati.
-
Je, ni lazima niingie ili kutumia WA Notify?
-
Ndiyo. Kutumia WA Notify ni ya bure na ya kujitolea. Unaweza kujiondoa wakati wowote. Kufanya hii, washa tu kipengele hicho kwenye iPhone au ufute programu hiyo kwenye simu ya Android. Mara tu umejiondoa, misimbo yote nasibu ambayo simu imehifadhi kutoka kwa watumiaji wa karibu itafutwa na haiwezi kupatikana tena.
-
Je, WA Notify ni programu ya kufuatilia mwasilani?
-
La. WA Notify haifuatilii maelezo kuhusu watu ambao umekuwa karibu nao, hivyo "haifuatilii waasilani". Ufuatiliaji wa mwasilani hutambua mtu yeyote ambaye mtu aliyepatikana na maambukizo ya COVID-19 huenda amekuwa karibu naye. Zana hiyo haikusanyi au kubadilisha maelezo yoyote ya kibinafsi, hivyo haiwezekani kwa mtu yeyote kujua mwasilani wako.
-
"Mfiduo" ni nini?
-
Mfiduo hutokea pale unapotumia muda ukiwa karibu na mtumiaji mwingine wa WA Notify ambaye baadaye hukutwa na ugonjwa wa COVID-19. Ili kubaini mfiduo, WA Notify hutumia kanuni pepe kutambua matukio ambayo yanaweza kusambaza COVID-19 kutoka kwa wale ambao walikuwa kwenye umbali salama au umbali mfupi sana ambao hauhitaji kupewa onyo. WA Notify itakutumia taarifa za mfiduo ikiwa kujumuika kwako na mtumiaji mwingine ni kwa ukaribu na kwa kipindi cha kutosha ambacho kinaendana na mazingira ambayo DOH inaamini kuwa kuna hatari kubwa ya kusambaa kwa COVID-19. Kanuni pepe hii inaweza kurekebishwa na maafisa wa afya ya umma.
-
Nini hufanyika iwapo WA Notify inaniambia kuwa huenda nimeambukizwa?
-
Iwapo WA Notify itagundua kuwa huenda umeambukizwa, taarifa kwenye simu yako itakupeleka kwenye wavuti ulio na maelezo kuhusu unachofaa kufanya. Hii inajumuisha jinsi na pahali pa kupimwa, maelezo kuhusu kujiweka salama na kuweka walio karibu nawe salama, na rasilimali za kujibu maswali yako. Ni muhimu kusoma na kufuata maelekezo kwenye wavuti kwa uangalifu.
-
Je, watu watajua iwapo nitapatikana na COVID-19?
-
La. WA Notify haishiriki maelezo yoyote kukuhusu na mtu yeyote mwingine. Mtu akipokea taarifa kuhusu mfiduo unaowezekana, wanajua tu kuwa mtu ambaye walikuwa karibu naye hivi karibuni ameambukizwa COVID-19. Hawatajua mtu huyo au mahali aliambukizwa.
-
Je, nastahili kulipi WA Notify?
-
La. WA Notify ni ya bure.
-
Je, WA Notify itasaidia vipi jimbo la Washington?
-
Utafiti wa University of Washington (Kiingereza pekee) ulipata kuwa watu wanavyozidi kutumia taarifa ya mfiduo, ndivyo manufaa yanakuwa makubwa. Matokeo yalionyesha kuwa WA Notify iliokoa karibu maisha 40 hadi 115 na huenda ikazuia karibu visa 5,500 vya COVID-19 wakati wa miezi minne ya kwanza ilipotumika. Mifumo ya data inaonyesha kuwa hata idadi ndogo ya watu wanaotumia WA Notify inaweza kupunguza maambukizo na vifo vya COVID-19, ikionyesha kuwa WA Notify ni zana bora ya kuzuia msambao wa COVID-19.
-
Je, WA Notify hufanya kazi nikisafiri nje ya jimbo?
-
Ndiyo. Ikiwa utasafiri nje ya jimbo ukiwa na programu ambayo inatumia teknolojia ile ile ya Google/Apple (Kiingereza Pekee), simu yako itaendelea kubadili misimbo isiyokuwa na mpangilio na watumiaji kwenye jimbo hilo. Hakuna haja ya kubadilisha chochote katika mipangilio ya simu janja yako. Ukitoka nje ya Washington kwa kipindi kirefu, unapaswa kukagua machaguo katika jimbo lako jipya ili kupata usaidizi na arifa za eneo hilo.
-
WA Notify huchukua muda upi kuwaarifu watumiaji wengine?
-
Watumiaji ambao huenda wameambukizwa COVID-19 na mtumiaji mwingine watapokea taarifa ndani ya saa 24 baada ya mtumiaji aliyeambikizwa COVID atafuata hatua katika WA Notify ili kuwaarifu watumiaji wengine wa WA Notify bila kujulikana.
-
Je, inawezekana kupokea arifa anuwai kutoka kwa WA Notify?
-
Watumiaji wanaopatikana na maambukizo wanaweza kupokea taarifa ibukizi na ujumbe mfupi. Watumiaji ambao huenda waliambukizwa mara kadhaa wataarifiwa kuhusu kila mfiduo mpya.
-
Ni vipi naweza kuambia WA Notify iwapo nimeambukizwa COVID?
-
Iwapo umeambukizwa ugonjwa, na mtu kutoka DOH au mamlaka yako ya ndani ya afya ya umma amewasiliana nawe, watauliza iwapo unatumia WA Notify. Iwapo unatumia, watakutumia kiungo na/au taarifa ya uthibitishaji na kukusaidia kufuata hatua za kuiingiza kwenye WA Notify. Kiungo/taarifa hazijafunganishwa na maelezo yako ya kibinafsi. DOH pia hutuma ujumbe wa matini na/au taarifa kwa nambari za simu zilizotumika na watu ambao hivi karibuni walipatikana na maambukizo ya COVID-19.
DOH haina njia yoyote ya kujua ni nani atapokea taarifa za mfiduo za WA Notify ukifuata hatua hizi. Taarifa hiyo ya mfiduo haitakuwa na maelezo yoyote kukuhusu. Watu wanaothibitisha matokeo yao bila kujulikana katika WA Notify wanavyozidi kushiriki misimbo yao, ndivyo tunaweza kuzuia bora msambao wa COVID-19.
Ukiwa na maambukizo na bado unahitaji kuthibitisha bila kujulikana matokeo yako katika WA Notify, rejelea sehemu ya "Jinsi ya kuwaarifu wengine ukipatikana na maambukizo ya COVID-19 kwa kutumia kipimo cha kibinafsi" kwenye ukurasa huu kwa hatua za kuomba msimbo wa uthibitisho ili kuwaarifu watumiaji wengine wa WA Notify bila kujulikana iwapo huenda una mfiduo.
-
Je, kuna kitu nahitaji kufanya baada ya kuongeza WA Notify kwenye simu yangu?
-
Kitendo cha ziada kinahitajika tu iwapo:
-
Utapatikana na COVID-19, au
-
Utapokea taarifa kuwa huenda umeambukizwa.
Iwapo umeambukizwa ugonjwa, na mtu kutoka DOH au mamlaka yako ya ndani ya afya ya umma amewasiliana nawe, watauliza iwapo unatumia WA Notify. Iwapo unatumia, watakutumia kiungo na/au taarifa ya uthibitishaji na kukusaidia kufuata hatua za kuiingiza kwenye WA Notify. Kiungo/taarifa hazijafunganishwa na maelezo yako ya kibinafsi. DOH haina njia ya kujua ni nani atakayearifiwa na programu kuhusu kuwa hatarini mwa kuambukizwa. Taarifa hiyo ya mfiduo haitakuwa na maelezo yoyote kukuhusu. Watu wanaothibitisha matokeo yao bila kujulikana katika WA Notify wanavyozidi kushiriki misimbo yao, ndivyo tunaweza kuzuia bora msambao wa COVID-19.
Ukiwa na maambukizo na unahitaji msimbo wa uthibitisho, rejelea sehemu ya "Jinsi ya kuwaarifu wengine ukipatikana na maambukizo ya COVID-19 kwa kutumia kipimo cha kibinafsi" kwenye ukurasa huu kwa hatua za kuomba msimbo wa uthibitisho ili kuwaarifu watumiaji wengine wa WA Notify bila kujulikana iwapo huenda una mfiduo.
-
-
Je, kutumia WA Notify kutamaliza betri yangu au kutumia data nyingi zaidi?
-
La. Imeundwa ili kuwa na athari ya chini kabisa kwenye data yako na maisha ya betri yako kwa kutumia teknolojia ya Bluetooth Low Energy technology.
- Kwa nini inaonekana kama WA Notify inatumia betri zaidi?
-
Kwa kweli, haitumii. Utumiaji wa betri kwenye kifaa chako unaonyesha asilimia ya betri inayotumika kila siku inajumuisha programu kama WA Notify. Programu na zana nyingi hazitumiki usiku kucha. WA Notify pia haiendeshwi usiku, lakini huwa inaangalia misimbo ya nasibu baada ya kila saa mbili kwa milingano ya mtumiaji mwenye maambukizo ili iweze kukuarifu kuhusu mfiduo wowote. Hivyo, kwa mfano, ikiwa hakuna programu nyingine ambazo zinaendeshwa wakati umelala, WA Notify itawakilisha asilimia ya juu ya betri iliyotumika wakati huo. Hiyo haimaanishi kuwa WA Notify inatumia betri nyingi - asilimia ya juu tu ya kiwango cha chini cha betri iliyotumika.
-
Je, nahitaji kuwasha Bluetooth kila mara ili WA Notify iweze kufanya kazi?
-
Ndiyo. WA Notify inatumia Bluetooth Low Energy, hivyo lazima Bluetooth iwe amilifu ili mfumo uweze kuwagundua watumiaji wengine wa karibu.
-
Je, nahitaji kufungua WA Notify kwenye simu yangu ili iweze kufanya kazi?
-
La. WA Notify itafanya kazi katika mandhari nyuma.
-
Je, WA Notify inaauniwa kwenye simu janja mzee?
-
Watumiaji wa iPhone wanaweza kutumia WA Notify iwapo mfumo wako wa uendeshaji ni:
-
iOS toleo la 13.7 au la hivi karibuni (kwa iPhone 6s, 6s Plus, SE au mpya)
-
iOS toleo la 12.5 (kwa iPhone 6, 6 plus, 5s)
Watumiaji wa Android wanaweza kutumia WA Notify iwapo simu yako ya Android inatumia Nishati ya Chini ya Bluetooth na Android Toleo la 6 (API 23) au zaidi.
-
-
Je, ni lazima niwe na umri wa miaka 18 ili kutumia WA Notify?
-
La. WA Notify haijui wala kuangalia umri wako.
-
Je, teknolojia hii itafanya kazi nikishiriki simu na mtu mwingine?
-
WA Notify haiwezi kujua aliyekuwa akitumia simu wakati wa mfiduo. Iwapo mnashiriki simu, kila mtu anayetumia simu hiyo anahitaji kufuata maelekezo ya afya ya umma iwapo WA Notify itaonyesha kuwa huenda umeambukizwa COVID-19.
- Nilipokea taarifa na/au ujumbe wa matini lakini mtu aliyepimwa alikuwa mwanafamilia au mtu wa kaya. Nafaa kufanya nini?
-
Mtumiaji wa WA Notify aliyepatikana na maambukizo anafaa kuruhusu hatua za kuwaarifu wengine bila kujulikana ambao huenda wakaambukizwa, hivyo unafaa kupuuza ujumbe wowote au taarifa ambazo si zako.
Ikiwa mwanafamilia au mwanachama wa kaya yako ni mtumiaji wa WA Notify, amepatikana na maambukizo, na bado wanahitaji kuthibitisha matokeo yao katika WA Notify, wanaweza kufuata hatua katika sehemu ya "Jinsi ya kuwaarifu wengine ukipatikana na maambukizo ya COVID-19 kwa kutumia kipimo cha kibinafsi" ya ukurasa huu.
-
Je, WA Notify hufanya kazi katika vifaa kama iPad au saa janja?
-
La. Mfumo wa Taarifa ya Mfiduo ulisanidiwa hasa kwa simu janja na haifanyi kazi kwenye iPad.
-
Jimbo la Washington linafanya nini kutoa ufikiaji kwa teknolojia hii kwa watu ambao hawana simu janja?
-
WA Notify si zana pekee ya kusaidia kuzuia msambao wa COVID-19. Ufuatiliaji wa mwasilani na juhudi nyingine zinasaidia kila mkaaji wa Washington, hata kama hawana simu janja. Chanjo ni njia bora ya kukomesha msambao wa COVID-19, na kuvaa barakoa, kukaa mbali na wengine, na kupunguza ukubwa wa mikutano ni njia nyingine kila mtu anaweza kusaidia kukomesha msambao wa COVID-19.
Lifeline program (Mpango muhimu) wa serikali ya muungano unatoa mkopo wa bili ya simu kila mwezi kwa wanaofuzu. Baadhi ya watoaji huduma wa pasi waya wanaoshiriki wanaweza pia kutoa simu mahiri ya bila malipo. Jifunze mengi kuhusu mpango huo, anayefuzu, jinsi ya kutuma ombi na watoaji huduma wa pasi waya wanaoshiriki (Kiingereza pekee).
-
Washington ilitoa WA Notify katika zaidi ya lugha 30, kwa hivyo ni kwa nini naiona tu katika Kiingereza na Kihispania pekee kwenye duka la Google Play?
-
WA Notify hufanya kazi kutegemea lugha iliyowekwa kama chaguo msingi kwenye simu ya mtumiaji. Kuna toleo moja tu la WA Notify, lakini mizuko yoyote - taarifa ya mfiduo, kwa mfano - itaonekana kwa lugha ambayo mtumiaji anapendelea kati ya lugha zaidi ya 30.
-
Nina muda upi wa kudonoa taarifa au kuwezesha kiungo cha uthibitishaji?
-
Una saa 24 baada ya kupokea taarifa au ujumbe wa matini ili kufuata hatua za kuwaarifu wengine katika WA Notify. Iwapo huwezi kudonoa taarifa au kubofya kiungo cha uthibitisho ndani ya muda, unaweza kuomba kiungo cha uthibitisho katika WA Notify kwa kufuata hatua katika sehemu ya "Jinsi ya kuwaarifu wengine ukipatikana na maambukizo ya COVID-19 kwa kutumia kipimo cha kibinafsi" kwenye ukurasa huu. Unaweza pia kuomba kiungo cha uthibitisho ikiwa mtu kutoka DOH au mamlaka yako ya ndani ya afya ya umma itawasiliana na wewe kuhusu matokeo yako ya COVID-19.
-
Kwa nini Washington ilichagua suluhisho hili?
-
Washington iliunda kikundi cha jimbo cha uangalizi, ikijumuisha wataalamu wa usalama na uhuru wa kiraia na wanachama wa jumuiya nyingi, ili kukagua mfumo wa taarifa ya mfiduo wa Google/Apple. Kikundi hicho kilipendekeza ukubalifu utakaozingatia uaminifu wa jukwaa hilo, ulinzi wa data wa kiwango cha juu na matumizi ya majimbo mengine.