Matibabu ya COVID-19

Watu wanaogunduliwa kuwa na COVID-19 na wako katika hatari kubwa ya kuugua sana wanaweza kufaidika na tiba (dawa) zinazopatikana za COVID-19. Matibabu haya yanaweza kusaidia kuzuia maradhi makali, kulazwa hospitalini na kifo kutokana na COVID-19. Zungumza na mtoa huduma wako wa afya mara moja ikiwa umegunduliwa kuwa na maambukizi na uko katika hatari kubwa ya kuugua sana kwani matibabu yanahitaji kuanzishwa mapema ili yawe na ufanisi zaidi. Mtoa huduma wako wa afya atakusaidia kubainisha ni dawa gani ya COVID-19 inayokufaa zaidi.

Matibabu/dawa za COVID-19 si mbadala wa uzuiaji. Bado inapendekezwa kwamba kila mtu anayestahiki apate chanjo na achukue hatua zingine ili kuzuia ueneaji wa COVID-19.

Matibabu ya Kingamwili ya Monokloni ni Nini?

Kingamwili ni protini ambazo miili ya watu hutengeneza ili kupambana na virusi, kama vile virusi vinavyosababisha COVID-19. Kingamwili zinazotengenezwa katika maabara hufanya kazi kama kingamwili asilia ili kupunguza kiwango cha virusi mwilini mwako. Zinaitwa kingamwili za monokloni. Ukiwa katika hatari ya kuugua maradhi makali ya COVID-19 na umepatikana na maambukizi ya COVID-19 au umekaribiana na mtu aliyeambukizwa, huenda ukataka kuzingatia matibabu ya kingamwili ya monokloni (mAb). Unaweza kustahiki kupata matibabu ya mAb (bebtelovimab) ya kutibu COVID-19 kulingana na umri, historia yako ya afya, na kipindi ambacho umekuwa na dalili.

Dawa ya Proflaksisi ya Kabla ya Kuwa katika Hatari ya COVID-19 ni Nini?

Dawa ya Proflaksisi ya Kabla ya Kuwa katika Hatari (PrEP) ni dawa iliyoundwa ili kuzuia virusi kujishikilia na kuingia kwenye seli za binadamu. Tofauti na kingamwili zingine za monokloni zinazopatikana kwa sasa, Evusheld ni kingamwili inayofanya kazi kwa muda mrefu ambayo imeidhinishwa tu ili kuzuia au kumlinda mtu kabla ya kuwa katika hatari ya kuambukizwa COVID-19. Evusheld haikusudiwi kutibu dalili zinazotokana na COVID-19 na haitolewi baada ya kukaribiana na mtu aliye na COVID-19; inatolewa ili kuzuia maambukizi kabla ya kuwa katika hatari.

Dawa za Kumeza za Kuzuia Virusi ni Nini?

Matibabu ya dawa za kumeza za kuzuia virusi husaidia mwili wako kupambana na COVID-19 kwa kuzuia virusi vya SARS-CoV-2 (virusi vinavyosababisha COVID-19) dhidi ya kuongezeka mwilini mwako, kupunguza idadi ya virusi ndani ya mwili wako, au kuimarisha mfumo wako wa kinga. Kwa kupata matibabu, unaweza kupata dalili zisizo hatari sana na yanaweza kupunguza uwezekano wa kuwa na maradhi makali na kuhitaji huduma hospitalini. Matibabu ya dawa za kuzuia virusi vya COVID-19 yanapatikana kwa wagonjwa walio na dalili nyepesi hadi wastani, ambao hawajalazwa hospitalini, na ambao wamekuwa na dalili kwa siku tano au chini, na walio katika hatari kubwa ya kuugua sana.

Dawa ya Kuzuia Virusi ya Sindano (IV) ni Nini?

Remdesivir (Kiingereza Pekee) ni dawa imara ya kuzuia virusi ambayo imeidhinishwa na Food and Drug Administration (FDA, Mamlaka ya Vyakula na Dawa) na haisambazwi kwa sasa na Washington State Department of Health (WADOH, Idara ya Afya ya Jimbo la Washington). Inafanya kazi kwa kuzuia virusi dhidi ya kuunda nakala zake yenyewe (kujinakili). Remdesivir hutolewa kupitia kudungwa sindano kwenye mshipa (mishipani) baada ya muda, ambayo huitwa uwekaji wa IV.

Remdesivir imeidhinishwa kwa matibabu ya watu wazima na watoto ambao hawajalazwa hospitalini ambao wako katika hatari kubwa ya kuugua COVID-19 kali. Mnamo tarehe 25 Aprili 2022, FDA ilipanua idhini hii ili kujumuisha watoto walio na umri wa angalau siku 28 ambao wana uzani wa angalau kilo 3 (takriban pauni 6.6) na ambao wako katika hatari ya kuugua sana, na kufanya remdesivir kuwa matibabu ya kwanza yaliyoidhinishwa na FDA kwa watoto chini ya umri wa miaka 12.

Matibabu ya Remdesivir yanapaswa kuanzishwa haraka iwezekanavyo, na ndani ya siku saba baada ya dalili kuanza, kwa hivyo ni muhimu kwa watu walio katika hatari ya kuugua sana kuwasiliana na mtoa huduma wao wa afya ikiwa wana dalili na wanagunduliwa kuwa na COVID-19. Matibabu hutolewa kama mfululizo wa sindano tatu za IV, zinazotolewa mara moja kwa siku kwa siku tatu mfululizo.

Sio vituo vyote vya huduma ya afya vinaweza kutoa matibabu ya remdesivir kwa wagonjwa wasiolazwa – wagonjwa wanapaswa kuwasiliana na mtoa huduma wao wa afya ili kubaini kama wanaweza kupata matibabu haya.

Remdesivir pia hutumiwa kutibu wagonjwa ambao wamelazwa hospitalini kutokana na maradhi kali zaidi kutokana na COVID-19. Iwapo umelazwa hospitalini kutokana na COVID-19, watoa huduma wako wa afya wataamua ikiwa remdesivir au matibabu mengine yanahitajika.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Je matibabu ya mAbs huwasaidia watu walio na COVID-19 vipi?

Matibabu ya mAb yaliyoidhinishwa na Food and Drug Administration ya Marekani (FDA, Mamlaka ya Vyakula na Dawa) kwa matumizi ya dharura yanaweza kuwasaidia watu walio katika hatari ya kuugua sana (Kiingereza na Kihispania pekee) kwa dalili kali za ugonjwa kwa:

  • Kupunguza uwezekano wa kulazwa hospitalini
  • Kupata nafuu haraka kutokana na COVID-19
Nani anaweza kupokea matibabu ya mAb?

MAb imeundwa kwa ajili ya watu ambao:

  • Wamegunduliwa kuwa na maambukizi ya COVID-19
  • Wana dalili nyepesi hadi wastani za ugonjwa kwa muda wa siku 10 au chini
  • Wako katika hatari kubwa ya kuugua sana
Je, ninaweza kupata chanjo ya COVID baada ya kupokea matibabu ya kingamwili ya monokloni?

Iwapo ulipokea matibabu ya kingamwili kutoka kwa watu waliopata afueni (tiba ya kingamwili ya monokloni au utegili kutoka kwa watu waliopata afueni) baada ya kuambukizwa COVID-19, unaweza kupokea chanjo ya COVID-19 wakati wowote baada ya kukamilisha matibabu. Watu hawahitajiki tena kusubiri siku 90 baada ya kukamilisha matibabu ya kingamwili kutoka kwa watu waliopata afueni.

Kwa maswali kuhusu ustahiki wa matibabu ya kingamwili kutoka kwa watu waliopata afueni, wasiliana na mtoa huduma wako.

Je, ninawezaje kuonyesha kwamba nimepokea matibabu ya kingamwili ya monokloni?

Mtoa huduma wa matibabu aliyetoa matibabu ya mAb anaweza kukupa hati zinazoonyesha wakati ulipopokea matibabu.

Ni nani anayestahiki kupokea dawa za kuzuia virusi za kumeza?

Paxlovid: Wagonjwa watu wazima na watoto (umri wa miaka 12 na zaidi wenye uzani wa angalau pauni 88/kilo 40) walio katika hatari kubwa ya kupata COVID-19 kali, ikijumuisha kulazwa hospitalini au kufariki.

Molnupiravir: Watu wazima walio katika hatari kubwa ya kupata COVID-19 kali, ikijumuisha kulazwa hospitalini au kufariki, na ambao chaguo mbadala za matibabu ya COVID-19 zilizoidhinishwa na Food and Drug Administration (FDA, Mamlaka ya Vyakula na Dawa) hazipatikani au hazifai kiafya.

Je, matibabu yanalipiwa na Medicaid/Children’s Health Insurance Program (CHIP)?

Ndiyo. Medicaid/Children’s Health Insurance Program (CHIP, Mpango wa Bima ya Afya ya Watoto) inalipia ada ya usimamizi (Kiingereza pekee) kwa matibabu ya mAbs. Ada ya usimamizi ni ada ambayo mtoa huduma ya afya hutoza ili kukupatia matibabu. Kwa matibabu mengi ya mAbs, gharama ya bidhaa yenyewe inalipwa na serikali ya nchi.

Ikiwa sina bima, je, bado ninaweza kupokea matibabu ya COVID-19?

Matibabu ya COVID-19 ambayo hununuliwa na serikali ya nchi hutolewa bila gharama kwa wagonjwa. Hata hivyo, watoa huduma wanaweza kutoza ada za usambazaji, matibabu na usimamizi ambazo zinaweza kulipiwa na bima, wagonjwa au mipango ya nchi. Ili kujua ni aina gani ya bima inayopatikana unapotafuta matibabu, tafadhali wasiliana na mtoa huduma wako.

Je, watu ambao hawajasajiliwa kisheria nchini wanaweza kupokea matibabu ya COVID-19?

Watu ambao hawajasajiliwa kisheria nchini wanaweza kupokea huduma kutoka kwa Alien Emergency Medical Programme (AEM, Mpango wa Dharura ya Afya ya Wageni) (Kiingereza pekee) kwa:

  • Dharura zinazostahiki ili kujumuisha tathmini na matibabu ya COVID-19. 
  • Mazingira ya upimaji na matibabu ili kujumuisha ofisi, kliniki au kupitia simu.
  • Huduma zilizoidhinishwa. Watu waliogunduliwa kuwa na COVID-19 wanaweza kulipiwa dawa na huduma za mfumo wa kupumua. Watu walio na uwezekano wa kuwa na COVID-19 wanaweza kulipiwa ziara za ufuatiliaji na dawa

Jinsi ya kutuma ombi kwa AEM

Watu wazima wenye umri wa miaka 19 hadi 64:

Watu wazima wenye umri wa miaka 65 au zaidi, vipofu, walemavu, au wanaohitaji huduma za muda mrefu:

Pata matibabu ya COVID-19

Mpango wa Test to Treat (Mpango wa Kupimwa ili Kutibiwa) (Kiingereza pekee) unaweza kutoa huduma za haraka na rahisi za matibabu ya COVID-19. Ukigunduliwa kuwa na virusi, unaweza kukutana na mtoa huduma ya afya (aidha katika eneo la huduma au matibabu ya mtandaoni), na ikiwa unastahiki, upate dawa za kumeza za matibabu ya kuzuia virusi na uwekewe dawa hizi—zote katika eneo moja.

Tembelea kitambua mahali pa Test to Treat au piga simu kwa 1-800-232-0233 (TTY 1-888-720-7489) ili upate usaidizi katika Kiingereza, Kihispania, na zaidi ya lugha zingine 150. Kituo cha simu kinafunguliwa kuanzia saa 8 asubuhi hadi saa sita usiku (ET), siku zote za wiki, na kitakusaidia kupata eneo karibu nawe.

Nyenzo kwa Watu Wasio na Bima

Watu wasio na bima wanaohitaji matibabu ya COVID-19 au huduma zingine za afya wanaweza kupata:

Watu wasio na bima pia wanaweza kupata huduma katika kliniki nyingi ambazo ni sehemu ya Vituo vya Afya Vilivyoidhinishwa na Nchi (Federally Qualified Health Centers (FQHCs)): 

Je, unahitaji usaidizi wa kutafuta mahali pa kupata dawa? Piga simu 1-800-232-0233 (TTY 888-720-7489) ili upate eneo la Test to Treat (Kiingereza pekee).

Nyenzo za Ziada

Nambari ya simu ya dharura ya jimbo kuhusu COVID-19 inapatikana ili kujibu maswali ya ziada. Maelezo ya simu ya Dharura yanapatikana kwenye Ukurasa wa Wasiliana Nasi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu matibabu ya COVID-19, tembelea ukurasa wa Tiba ya COVID-19 wa Centers for Disease Control and Prevention (Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa).