Stroke and Heart Attack Signs and Symptoms - Swahili

English

Kiswahili

Kiharusi na mshtuko wa moyo kila mara huwa dharura. Lakini je, unajua dalili za kiharusi na mshtuko wa moyo?

Maarifa ni nguvu. Okoa maisha kwa kujifunza dalili na ishara, kuzitambua zinapotokea, na kupiga 911 ili kupata usaidizi.

Kiharusi

  • Kukufa ganzi au unyonge kwenye uso, mkono au mguu, hasa kwenye upande mmoja wa mwili kwa ghafla
  • Kuchanganyikiwa au usemi wenye matatizo ya kufahamu kwa ghafla
  • Matatizo ya ghafla ya kuona kwa jicho moja au yote mawili
  • Matatizo ya ghafla ya kutembea, kizunguzungu, au kupoteza usawaziko au uratibu
  • Maumivu makali ya kichwa ya ghafla yasiyo na chanzo kinachojulikana

Mshtuko wa moyo

  • Uchungu au maumivu kwenye kifua
  • Kichwa chepesi, kichefuchefu ama kutapika
  • Maumivu ya taya, shingo au mgongo
  • Maumivu au uchungu kwenye mkono au bega
  • Upungufu wa pumzi

Unapofikiria kuwa huenda mtu ana kiharusi au mshtuko wa moyo, usisubiri. Piga 911 mara moja. Wataalamu wa huduma za matibabu ya dharura wamefunzwa kutambua kiharusi na mshtuko wa moyo na kumpeleka mgonjwa hospitalini kwa haraka. Dharura za kiafya zinaweza kutibiwa na kadri mgonjwa anavyopata matibabu kwa haraka, ndivyo kuna uwezekano mkubwa wa wao kurejea nyumbani kwa familia na ratiba.