Mwongozo wa Uthibitisho Rasmi wa Chanjo ya COVID-19 katika Jimbo la Washington

Chanjo ya COVID-19 inahitajika na biashara, matukio na waajiri wengi. Aina zifuatazo za uthibitisho zinakubaliwa Washington. Baadhi ya maeneo yanaweza kukubali tu aina moja kutoka kwa orodha inayofuata.

Heshimu kanuni za chumba na kujiandaa mapema ili kuonyesha aina ya uthibitisho unaohitajika.

CDC Kadi ya Rekodi ya Chanjo ya COVID-19

  • Nakala asili, nakala, au picha kwenye kifaa cha mkononi zinakubaliwa.
  • Chanjo kamili ni halali wiki mbili baada ya dozi ya mwisho iliyorekodiwa:
    • Johnson & Johnson: Dozi moja, imeidhinishwa kwa wale walio na miaka 18 na zaidi
    • Moderna: Dozi mbili zinatumiwa siku 28 tofauti kwa walio na miezi 6 na zaidi
    • Novavax: Dozi mbili zinatumiwa siku 21 tofauti kwa walio na miaka 12 na zaidi
    • Pfizer: Dozi tatu zilitolewa kwa watoto walio na umri wa miezi 6 hadi miaka 4. Dozi mbili za kwanza zinafaa kupeanwa siku 21 baada ya dozi ya kwanza na dozi ya tatu wiki 8 baada ya dozi ya pili.
    • Pfizer: Dozi mbili zinatumiwa siku 21 tofauti kwa walio na miaka 5 na zaidi
COVID-19 Vaccination Record Card Sample

Hapa ni baadhi ya vidokezo muhimu vya kukumbuka unaposhughulikia kadi yako ya chanjo:

Cheti cha Chanjo ya COVID-19 au Misimbo ya QR.

Certificate of COVID-19 Vaccination - Sample

Sampuli ya A:
Cheti cha Chanjo ya COVID-19. Zinapatikana kwenye MyIRmobile.com.
WA verify SMART Health Card QR code - Sample

Sampuli ya B:
WAverify.org Msimbo wa QR
QR Code Endorsed Partner App. - Sample

Sampuli ya C:
Msimbo wa QR umeonyeshwa kwenye programu ya simu ya mkononi iliyoteuliwa. (Programu zinaweza kutofautiana)

Chapisho la Mfumo wa Taarifa ya Chanjo katika Jimbo la WA

  • Fomu za Certificate of Immunization Status (CIS, Cheti cha Hali ya Chanjo) zilizochapishwa kutoka Washington State Immunization Information System.
  • Maingizo yaliyoandikwa kwa mkono hayazingatiwi kuwa ni halali isipokuwa yakiwa yametiwa sahihi na mhudumu wa afya.
Certificate of Immunization - Sample

Ni nini tena inastahiki kuwa rekodi rasmi ya chanjo ya COVID-19?

  • Chapisho la rekodi ya matibabu ya kieletroniki iliyothibitishwa kutoka kwa mtoaji wa huduma ya afya

Kukiwa na maswali kuhusu rekodi za chanjo, piga 1-800-525-0127, kisha ubonyeze #.