Long COVID

Je, Long COVID ni nini?

Watu walioathiriwa na COVID-19 wanaweza kuendelea kuwa na dalili na athari za muda mrefu baada ya maambukizi yanayoitwa “long COVID” au “post-COVID Syndrome”. Mambo mengi bado hayajulikani kuhusu Long COVID. Tunaendelea kupata maelezo zaidi huku utafiti kuhusu long COVID ukiendelea.

Dalili za Long COVID

Watu walio na long COVID wanaweza kuwa na dalili mbalimbali zinazoweza kudumu kwa wiki, miezi au miaka mingi baada ya maambukizi.

Dailili ni pamoja na lakini si tu:

  • Kujihisi mchovu, haswa baada ya jitihada ya akili au mwili.
  • Homa
  • Tatizo la kupumua
  • Kukohoa
  • Maumivu ya kifua
  • Mabadiliko katika harufu na/au ladha
  • Matatizo ya kufikiria au kumakinika au “ukungu wa akili”
  • Maumivu ya kichwa
  • Maumivu ya tumbo
  • Mabadiliko katika mizunguko ya hedhi

Je, ni nani anayeweza kupata Long COVID?

Yeyote aliyeambukizwa COVID-19 anaweza kupata long COVID. Ni maarufu sana kwa watu waliokuwa na dalili mbaya za COVID-19, haswa wale waliohitaji kulazwa hospitalini. Watu walioshuhudia dalili ya uvimbe kwenye mifumo mingi wakati wa au baada ya maambukizi yao ya COVID-19 wanaweza kuwa kwenye hatari ya juu ya long COVID.  Wanawake, watu wazima wazee, watu walio na maradhi ya zamani na watu ambao hawakuchanjwa wanasemekana kuwa na uwezekano zaidi wa kupata long COVID. Watu wanaopata COVID-19 mara nyingi pia wanaweza kuwa kwenye hatari zaidi ya afya ikiwa ni pamoja na long COVID.  

Kuzuia Long COVID

Kuzuia maambukizi ya COVID-19 ni njia bora ya kuzuia long COVID. Jikinge na uwakinge wengine kutopata COVID-19 kwa kunawa mikono, kuvaa barakoa kwenye umati, kukaa nyumbani ukiwa mgonjwa na kupata chanjo na dozi za kiongeza nguvu zinazopendekezwa.

Watu waliochanjwa ambao bado wanapata COVID-19 huenda wakawa na uwezekano wa chini wa kupata long COVID kuliko watu ambao hawajachanjwa.

Pata maelezo kuhusu kuchanjwa kwa ajili ya COVID-19

Kutambua Long COVID

Vinaweza kuwa vigumu kutambua long COVID. Dalili zinaweza kuwa ngumu kwa wagonjwa kueleza. Hakuna kipimo cha maabara wala utafiti wa picha wa kutambua. Vipimo vya matibabu vinaweza kuonyesha matokeo ya kawaida hata ikiwa mgonjwa ana long COVID.

Watu wengine wanaoripoti dalili za long COVID hawakuonyesha dalili za COVID-19 na hawakupimwa COVID-19 walipokuwa wagonjwa mwanzo. Hali hii inatatiza kuthibitisha kwamba walikuwa na COVID-19 na inaweza kuzuia au kuchelewesha utambuzi wa long COVID. Ni muhimu upimwe COVID-19 wakati unapojihisi mgonjwa mara ya kwanza ili kusaidia katika utambuzi wako wa long COVID baadaye.

Vidokezo vya Mgonjwa: Miadi ya mtoa Huduma wa Afya kwa Maradhi ya Baada ya COVID (kwa Kiingereza)

Maradhi Mapya na Yaliyopo

Maambukizi ya COVID-19 yanaweza kuathiri mifumo mingi ya viungo na yanaweza kuchochea maradhi ya kingamwili ya asili yanayoweza kuwa sehemu ya long COVID. Maradhi ya kingamwili ya asili yanaweza kutokea wakati mfumo wa kingamwili unasababisha uvimbe au uharibifu wa tishu katika sehemu zilizoathiriwa za mwili. Hii inamaanisha kuwa watu waliokuwa na COVID-19 wana uwezekano mkubwa wa kupata matatizo mapya ya afya, kama vile ugonjwa wa kisukari au wa moyo.  Maradhi yaliyopo kama vile kisukari na ugonjwa wa moyo yanaweza pia kuwa mabaya zaidi baada ya maambukizi ya COVID-19.

Haki za Long COVID na Ulemavu

Long COVID inaweza kusababisha ulemavu wa mwili na akili na huchukuliwa kama ulemavu kulingana na Americans with Disabilities Act (ADA, Sheria ya Wamarekani Walio na Ulemavu). Watu walio na long COVID wanalindwa kisheria dhidi ya ubaguzi wa ulemavu. Wanaweza kuwa na haki ya maboresho yanayofaa kuanzia heria za biashara, serikali za jimbo na za mitaa ili kujumuisha mapungufu yanayohusiana na long COVID.

Mwongozo kuhusu “Long COVID” kama Ulemavu Kulingana na ADA (in English)

Long COVID na Ujauzito

Wajawazito na waliokuwa wajawazito hivi majuzi wana uwezekano zaidi wa kuwa wagonjwa sana kutokana na COVID-19. COVID-19 inaweza kusababisha matatizo yanayoweza kuathiri ujauzito na mtoto anayekua.

Mambo mengi bado hayajulikani kuhusu jinsi long COVID inavyoweza kuathiri ujauzito. National Institutes of Health (NIH, Asasi za Afya za Taifa) (kwa Kiingereza) itafanya utafiti wa miaka 4 kuhusu athari za muda mrefu za COVID-19 kwa wanawake waliokuwa na COVID-19 wakiwa wajawazito na watoto wao.

Long COVID na Vijana

Vijana pia wanaweza kuugua long COVID. Vijana wanaoshuhudia dalili za long COVID kama vile uchovu na matatizo ya kumakinika wanaweza kutatizika kushiriki katika mambo ya shule na shughuli nyinginezo. Watoto wachanga wanaweza kutatizika kuonyesha dalili zao.

Watoto walio na COVID wanaweza kustahiki elimu maalum, huduma za kinga au zinazohusiana kulingana na sheri 2 za Serikali Kuu (kwa Kiingereza).

Kuwashawishi vijana kuchanjwa dhidi ya COVID-19 ni njia bora ya kuzuia long COVID kwa vijana.

Pata maelezo zaidi kuhusu kuwachanja vijana.

Taarifa kwa Madaktari