Care Connect Washington

Iwapo umepatikana na maambukizo ya COVID-19 na unahitaji chakula au usaidizi mwingine ukiwa umejitenga, tafadhali piga simu kwa nambari ya simu ya COVID-19 kupitia 1-800-525-0127, kisha ubonyeze #. Usaidizi wa lugha unapatikana.

Care Connect Washington ni mpango wa kutoa chakula na vitu vingine muhimu kwa watu ambao ama wamepatikana na maambukizo ya COVID-19 au wamekuwa na mfiduo na wanahitaji usaidizi wa kujitenga au kukaa karantini nyumbani. Department of Health katika jimbo, ikifanya kazi na mipaka ya afya na washirika wao, inaendesha Care Connect Washington kulingana na kigezo cha eneo hadi eneo. Kila eneo hufanya kazi na washirika wa jumuiya kuwaunganisha watu na huduma wanazostahiki kupata, kama vile uwasilishaji wa matibabu, utunzaji wa kiafya, usaidizi wa kutuma ombi la ukosefu wa ajira, mashirika ya nyumba ya ndani, benki za chakula, watoaji huduma ya utunzaji wa watoto na zaidi. Usaidizi unatolewa kutegemea haja.

Ili kuwezeshea watu waliojitenga au waliopo karantini kukaa nyumbani, Care Connect Washington hutoa vitu kama vifaa vya utunzaji wa kibinafsi, vifaa vya vyakula visivyoharibika kwa haraka, na maagizo ya vyakula vibichi kwa nyumba zao. Iwapo mahitaji mengine muhimu yametambuliwa, kama vile usaidizi wa kifedha wa kulipa matumizi, mratibu wa utunzaji wa ndani husaidia watu kuomba rasilimali za ndani au huduma ambazo huenda wanastahiki kupata, au kuwapa usaidizi wa moja kwa moja katika kulipa matumizi kama vile kodi ya nyumba, malipo ya nyumba, na matumizi. Wakati ambapo kujitenga au kukaa karantini itakapoisha, mratibu wa utunzaji anaweza kuwaunganisha watu na huduma za ndani za muda mrefu ili kusaidia mahitaji ya kiafya na kijamii yanayoendelea. Care Connect Washington inatoa maelezo ambayo watu wanahitaji katika lugha wanayopendelea.

Iwapo umepatikana na maambukizo ya COVID-19 na unahitaji chakula au usaidizi mwingine ili kujitenga nyumbani, wasiliana na Nambari ya Simu ya Taarifa ya COVID-19   -1-800-525-0127, kisha ubonyeze #. Usaidizi wa lugha unapatikana. Saa za kupiga simu ni:

  • Jumatatu saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku
  • Saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni, Jumanne hadi Jumapili, na sikukuu za jimbo zinazofuatiliwa (katika Kiingereza pekee)

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Care Connect regions map with services in these counties: Grays Harbor, Mason, Thurston, Pacific, Wahkiakum, Lewis, Cowlitz, Clark, Skamania, Clickitat, Yakima, Benton, Franklin, Adams, Lincoln, Ferry, Stevens, Pend Oreille, Spokane, King, Pierce, Snohomish, Skagit, Whatcom

Mtazamo wa Kiukanda wa Msaada wa COVID-19

Department of Health katika jimbo, ikifanya kazi na mipaka ya afya na washirika wao, inaendesha Care Connect Washington kulingana na kigezo cha eneo hadi eneo. Kila eneo hufanya kazi na washirika wa jumuiya kuwaunganisha watu na huduma wanazostahiki kupata, kama vile uwasilishaji wa matibabu, utunzaji wa kiafya, usaidizi wa kutuma ombi la ukosefu wa ajira, mashirika ya nyumba ya ndani, benki za chakula, watoaji huduma ya utunzaji wa watoto na zaidi.

Huduma Zinapatikana Wapi?

Huduma zinapatikana katika sehemu kadhaa za jimbo kwa watu wanaokubali kujitenga au kukaa kwenye karantini nyumbani lakini wanahitaji usaidizi kufanya hivyo.

Ukanda wa Mashariki

Better Health Together (Kiingereza pekee) inahudumu kama Care Connect Washington Kituo cha kaunti za Adams, Ferry, Lincoln, Pend Oreille, Spokane, na Stevens.

Kaunti ya King

Department of health (DOH, Idara ya Afya) inahudumu kama Kituo cha Care Connect Washington katika King County na WithinReach (katika Kiingereza pekee) hutoa huduma za uratibu wa utunzaji.

Ukanda wa Kaskazini mwa Kati

DOH kwa sasa inaratibu huduma za eneo hili. Inafanya kazi kuanzia Aprili tarehe 1, 2022, Action Health Partners katika Kiingereza pekee) itahudumu kama Kituo cha Care Connect Washington katika kaunti za Chelan, Douglas, Grant na Okanogan.

Ukanda wa Kaskazini

North Sound Accountable Community of Health (katika Kiingereza pekee) inahudumu kama Kituo cha Care Connect Washington katika kaunti za Island, San Juan, Skagit, Snohomish, na Whatcom.

Ukanda wa Kaskazini Magharibi

DOH kwa sasa inaratibu huduma za eneo hili kwa huduma zinazopatikana katika Clallam County.

Kaunti ya Pierce

Elevate Health (katika Kiingereza pekee) inahudumu kama Kituo cha Care Connect Washington katika Pierce County.

Ukanda wa Kusini mwa Kati

Providence St. Mary (katika Kiingereza pekee) inahudumu kama Kituo cha Care Connect Washington katika Kittitas, Walla Walla, Whitman, Columbia, Garfield, Asotin, Yakima, Benton na Franklin.

Ukanda wa Kusini Magharibi

Southwest Washington Accountable Community of Health (SWACH) (katika Kiingereza pekee) inahumu kama Kituo cha Care Connect Washington katika kaunti Clark, Klickitat, na Skamania.

Ukanda wa Magharibi

Community CarePort (katika Kiingereza pekee) ya Cascade Pacific Action Alliance inahudumu kama Kituo cha Care Connect Washington katika kaunti za Cowlitz, Wahkiakum, Pacific, Grays Harbor, Mason, Thurston, na Lewis.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Je, huduma Care Connect Washington zinapatikana kwa ajili yangu?

Unastahiki kupata huduma iwapo utapatikana na maambukizo ya COVID-19 na umejitenga kwa uamilifu nyumbani. Iwapo umekuwa katika mfiduo wa karibu na mtu aliyepatikana na maambukizo na unakarantini nyumbani, wewe pia huenda ukastahiki.

Piga Nambari ya Simu ya Maelezo ya COVID-19 katika 1-800-525-0127, kisha ubonyeze #. Usaidizi wa lugha unapatikana. 

  • Jumatatu saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku
  • Saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni, Jumnne hadi Jumapili, na sikukuu za jimbo zinazofuatiliwa

Mratibu wako wa ndani wa utunzaji atawasiliana na wewe ili kuunda mpango wa utunzaji ili kukidhi mahitaji yako wakati wa kujitenga. Kipindi chako cha kujitenga kikiisha, mratibu wako wa utunzaji atakuunganisha na usaidizi wa uratibu wa muda mrefu, iwapo utahitaji.

Naweza kutarajia aina gani ya usaidizi?

Mratibu wako wa ndani wa utunzaji ataainisha rasilimali zinazopatikana ili kukusaidia ukiwa umejitenga au kuingia karantini nyumbani. Pia watakusaidia kwa kutoa chakula, usambazaji, na usaidizi wa kifedha wa kodi ya nyumba, malipo ya nyumba, na bili za matumizi iwapo rasilimali za ndani hazipatikani wakati umejitenga au kuingia karantini nyumbani. Mratibu wako wa utunzaji anaweza pia kukuunganisha na huduma unazohitaji zikiwemo huduma za utoaji wa matibabu, utunzajiw a kiafya, kutuma ombi la kutoajiriwa, na zaidi. Huduma nyingine zinaweza kujumuisha kuunganisha na mashirika ya ndani ya nyumba, benki za chakula, vituo vya utunzaji wa afya, utunzaji wa wazee, watoaji wa afya ya kitabia, watoaji wa utunzaji wa watoto, na huduma za kijamii zinazofaa katika utamaduni husika. Huduma zitatofautiana kulingana na ukanda. Wakati ambapo kujitenga au kukaa karantini itakapoisha, mratibu wako wa utunzaji anaweza kukuunganisha na huduma za ukanda za muda mrefu ili kusaidia mahitaji yanayoendelea. Care Connect Washington itatoa maelezo ambayo unahitaji katika lugha unayopendelea.

Je, nafuzu kupokea Care Connect Washington?

Unafuzu iwapo:

  • Ulipatikana na maambukizo ya COVID-19 au ulikuwa karibu sana na mtu ambaye alipatikana na maambukizo; na
  • Umejitenga au kuingia karantini nyumbani.

Huduma za Care Connect Washington zinapatikana bila gharama yoyote kwa wanaofuzu. Usaidizi utatolewa kulingana na haja.

Je, huduma Care Connect Washington zinapatikana wapi?

Department of Health katika jimbo, ikifanya kazi na mipaka ya afya na washirika wao, inaendesha Care Connect Washington kulingana na kigezo cha ukanda. Hii hapa ni ramani inayoonyesha mahali ambapo huduma zinapatikana kwa sasa:

Care Connect regions map with services in these counties: Grays Harbor, Mason, Thurston, Pacific, Wahkiakum, Lewis, Cowlitz, Clark, Skamania, Clickitat, Yakima, Benton, Franklin, Adams, Lincoln, Ferry, Stevens, Pend Oreille, Spokane, King, Pierce, Snohomish, Skagit, Whatcom
Itanigharimu pesa ngapi?

Hutatoza ili kupokea huduma hii. Care Connect Washington ilipokea fedha serikali ya shirikisho za kusaidia katika kukabiliana na COVID-19 katika jimbo la Washington.

Itachukua muda upi kabla ya kuweza kupokea usaidizi?

Mratibu wako wa utunzaji katika ukanda atafanya kila juhudi kutoa usaidizi ndani ya simu moja baada ya kupokea kutumwa kwako.

Je, bado nitahitaji kujitenga au kukaa katika karantini huku nikipokea usaidizi huu?

Ndiyo. Kujitenga na kukaa karantini ni zana muhimu zinazotumika kuepuka kusambaza COVID-19 kwa majirani, marafiki, familia na wafanyakazi wenzi - na kupunguza athari zake hasi zinazowafikia wengi katika jamii zetu. Iwapo unahitaji usaidizi baada ya kipindi chako cha kujitenga au karantini, mratibu wako wa utunzaji katika kanda anaweza kukuunganisha na huduma za ndani za muda mrefu ili kusaidia mahitaji ya kiafya na kijamii yanayoendelea.

Kuna tofauti gani kati ya kujitenga na karantini?

Kujitenga: Ukipatikana na maambukizo ya COVID-19, una dalili, au unasubiri matokeo ya kipimo, unahitaji kujitenga ili kuepuka kusambazia wengine magonjwa yako.

Karantini: Iwapo ulikuwa na mfiduo wa COVID-19 lakini huna dalili, unaweza kuhitaji kukaa karantini, kutegemea na hali yako ya chanjo. Hii itazuia kusambaza virusi kabla ya kujua kuwa wewe ni mgonjwa.

Fuata mwongozo wa hivi karibuni zaidi (katika Kiingereza pekee) kutoka kwa CDC (katika Kiingereza pekee) na DOH (katika Kiingereza pekee) kuhusu urefu wa kipindi cha karantini.

Nafaa kufanya nini iwapo dalili zangu za COVID-19 zitaendelea kuwa hatari?

Pata usaidizi wa matibabu kwa haraka ikiwa dalili zako zitaongezeka sana. Iwapo mtu ataonyesha dalili yoyote kati ya zifuatazo, tafuta usaidizi wa kimatibabu wa dharura mara moja:

  • Tatizo la kupumua
  • Maumivu au shinikizo la muda mrefu kwenye kifua
  • Kuchanganyikiwa mpya
  • Kutoweza kuamka au kukaa macho
  • Midomo au uso wa samawati

*Hii si orodha kamili. Tafadhali wasiliana na mtoa huduma wako wa matibabu kwa dalili nyingine zozote ambazo ni mbaya au zikunatia wasiwasi.

Ukiwa na dharura ya matibabu na unahitaji kupiga 911, mwambie mhudumu huyo kuwa una au huenda una COVID-19. Ikiwezekana, vaa barakoa kabla ya huduma za kimatibabu za dharura kutokea.

Je, naweza kupokea huduma za Care Connect Washington kwa muda gani?

Mratibu wako wa utunzaji katika ukanda atakusaidia kwa hadi siku 21. Katika hali fulani, mratibu wako wa utunzaji anaweza kukuunganisha na huduma za muda mrefu ili kusaidia mahitaji ya kiafya na kijamii yanayoendelea.

Je, Care Connect Washington inafanya kazi vipi?

Care Connect Washington ni mtazamo unaoauniwa na jimbo, unaojikita sana maeneo ya ndani kwa utunzaji unaoratibiwa.

Washington State Department of Health inasimamia juhudi za uratibu wa utunzaji katika ukanda, inasaidia kuajiri na kutoa mafunzo, inazuia mapengo katika rasilimali za jimbo zima na za ndani, na kuhakikisha matokeo ya juu zaidi kwa kusimamia rasilimali zilizokusanywa pamoja, kama vile ufadhili na muundomsingi wa kiufundi.

Kanda maalum hutambua na kutuma jopo kazi linalojikita katika jamii ili kutoa usaidizi na kuunganisha watu kwa rasilimali za ndani ili kusaidia kujitenga na kukaa karantini kwa mafanikio. Kanda hizo zinafanya kazi na wauzaji wa ndani ili kusambaza bidhaa na huduma zinazohitajika, kusaidia kuchangia kwa ufufuaji wa uchumi wa ndani.

Waratibu wa utunzaji wametolewa ili kutathmini, kusaidia, na kufuatilia afya na mahitaji ya kijamii ya kipekee ya kila mtu na kuunda Mpango wa Hatua ya Utunzaji wa COVID. Mpango huo unaunganisha watu na rasilimali katika lugha wanayopendelea popote panapowezekana na kuwaelekeza kwenye mchakato wa kuhakikisha kuwa wamesaidiwa.

Utalindaje maelezo yangu?

Mratibu wako wa utunzaji atathibitisha maelezo wanayopata kutoka kwa Nambari ya Simu ya Taarifa ya COVID-19 na kuuliza kuhusu mahitaji yako. Maelezo yoyote unayoshiriki na mratibu wako wa utunzaji utasalia kuwa ya siri. Wafanyakazi wanaotoa huduma za uratibu na Department of Health watatumia maelezo ili kubainisha huduma muhimu ambazo huenda ukahitaji. Hawatashiriki maelezo ya kiafya ya kibinafsi au ya faragha.

Care Connect Washington huzuia vipi msambao wa COVID-19?

Watu wanaopokea usaidizi wa kukidhi mahitaji ya kijamii na kiafya wana uwezekano mkubwa zaidi wa kufanikiwa kukamilisha kujitenga nyumbani na kukaa kwenye karantini. Kwa kuhakikisha kuwa watu ambao wamepatikana na maambukizo ya COVID-19 au walikuwa na mfiduo kwa mtu mwingine aliyeambukizwa huendelea kujitenga au kukaa karantini, Care Connect Washington inaweza kupunguza msambao wa COVID-19 na kuboresha ufufuaji wa uchumi. Kwa sababu mfumo uawalenga watu walio na mahitaji ya kiafya na kijamii ambao wanaweza kudhurika zaidi na COVID-19, inaweza kusaidia kutatua ukosefu uliopo wa usawa kiafya na kusaidia jamii zilizoathiriwa na COVID-19.

Nawasiliana na nani iwapo namjua mtu ambaye anahitaji utunzaji kutoka kwa Care Connect Washington?

Iwapo wewe au mtu unayemjua amejitenga kwa uamilifu au ameingia karantini nyumbani na anahitaji usaidizi, wasiliana na Nambari ya Simu ya Taarifa ya COVID-19 ya Jimbo.

Nambari ya Simu ya Taarifa ya COVID-19 ya Jimbo: Bofya 1-800-525-0127, kisha ubonyeze #. Usaidizi wa lugha unapatikana.

  • Jumatatu saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku
  • Saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni, Jumnne hadi Jumapili, na sikukuu za jimbo zinazofuatiliwa
Je, Care Connect Washington inajumuisha huduma za afya ya kitabia?

Ndiyo! Mratibu wako wa utunzaji anaweza kukusaidia kupata huduma za kiafya za kitabia katika jamii yako.

Je, huduma za msaada wa uratibu wa usaidizi zina[atikana kwa wanachama wa Tribal Nations (Mataifa ya Kikabila)?

Ndiyo. Ili kujifunza zaidi, tuma barua pepe kwa COVID19.CareCoordination@doh.wa.gov aupiga 564-999-1565.

Je, huduma za ukalimani zinapatikana?

Ndiyo. Ukipiga Nambari ya Simu ya Maelezo ya COVID-19 katika 1-800-525-0127 na kisha kubonyeza #, usaidizi wa lugha utapatikana.

Mara tu umeunganishwa kwa mratibu wa utunzaji, Care Connect Washington itatoa maelezo ambayo unahitaji katika lugha unayopendelea.

Rasilimali