COVID-19

This page is being reviewed for updates. The Washington State Department of Health has updated its guidance for what to do if you are sick with COVID-19 or were exposed to COVID-19. This page may have content that is inconsistent with the new guidance.

Nambari ya Simu ya Taarifa ya COVID-19

Ukiwa na maswali kuhusu COVID-19, piga 1-800-525-0127 na kubonyeza 7. Wakipokea, sema lugha yako ili kufikia huduma za ukalimani. Nambari hiyo ya simu inapatikana Jumatatu kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku, na Jumanne hadi Jumapili (na sikukuu) saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni.

Huwezi kutoka nyumbani na unahitaji chanjo ya COVID-19?

Kuna njia tatu za kujisajili.

Jitunze WA - Kuishi Vyema na Salama Kupitia COVID-19

Sasa tunajua kuwa COVID-19 iko hapa na itaendelea kuishi kwa siku zisizojulikana. Ni muhimu kufahamu namna ya kuishi maisha yetu huku tukihakikisha sisi, wapendwa wetu na jamii iko salama kila mara. Tunawezaje kufanya hiyo? Kwa kutumia zana zote ambazo tumejifunza kufikia sasa: kupokea chanjo na busta, kupimwa na kukaa nyumbani iwapo umeambukizwa au una mfiduo, kuvaa barakoa ukiwa katika umati, na kukaa mbali na wengine.

Haya ni mambo unayohitaji kujua tunapoingia wkenye hatua mpya ya maisha ya kuishi pamoja na COVID-19 katika jamii yetu.

Chukua Hatua, Jitunze

Decorative

Pokea Chanjo na Busta

Chanjo na busta za COVID-19 ndizo kinga nambari moja dhidi ya maambukizo na maradhi makali.

Jifunze Zaidi

Decorative

Jua Wakati wa Kupimwa

Punguza hatari ya kusambaza COVID-19 kwa kupima iwapo unahisi wewe ni mgonjwa, unahudhuria mkutano, au umekuwa na mfiduo wa COVID-19.

Jifunze Zaidi

Decorative

Vaa Barakoa

Kuvaa barakoa kumethibitishwa kuwa kunapunguza msambao wa COVID-19 na barakoa bado zinahitajika katika mazingira mengine.

Jifunze Zaidi

 

Iwapo Una Maambukizo ya COVID-19 Sasa

Angalia Miongozo ya Hivi Karibuni Zaidi

Kaa nyumbani na mbali na wengine, na ufuate miongozo ya hivi karibuni zaidi ya kujitenga.

Jifunze Zaidi

Pata Matibabu

Wasiliana na mhudumu wako wa afya ili kujua zaidi kuhusu chaguo zako za matibabu.

Jifunze Zaidi

Pata Msaada wa Kupata Nafuu

Pata kuletewa chakula na dawa nyumbani, utunzaji wa mtoto, na huduma nyingine huku ukiendelea kupata nafuu kutokana na COVID-19.

Jifunze Zaidi

Long COVID

Watu walioambukizwa COVID-19 wanaweza kuwa na dalili ambazo zinadumu kwa wiki hadi miaka baada ya maambukizo. Zuia COVID ya muda mrefu kwa kuzuia maambukizo ya COVID-19.

Jifunze Zaidi

Taarifa ya Ziada

Dalili, ishara na uzuiaji wa COVID-19

Dalili kuu za COVID-19 ni zifuatazo:

  • Kikohozi, upungufu wa pumzi au ugumu wa kupumua, joto kali, baridi, maumivu ya misuli, vidonda vya koo, kupoteza uwezo wa kuonja au kunusa. Dalili nyingine zisizo za kawaida sana ni kichefuchefu, kutapika au kuhara.
  • Piga 911 iwapo utaona yoyote kati ya dalili zifuatazo za onyo la dharura za COVID-19:
    • Tatizo la kupumua
    • Maumivu ya mara kwa mara ya kifua au shinikizo
    • Kuchanganyikiwa kwa ghafla
    • Kutoweza kuamka au kukaa macho
    • Ngozi, midomo, au kucha zilizokwajuka, za rangi ya kahawia au buluu, kutegemea ulaini wa ngozi
  • Vikundi vipi vipo hatarini?
    • Watu wazee, watu wa umri wowote walio na hali za kimatibabu, na wanawake wajawazito wanaweza kuwa katika hatari ya maradhi makali kutokana na COVID-19.

Naweza kujilinda na kulinda familia yangu kwa njia gani?

  • Pokea chanjo na busta unapostahili.
  • Kaa nyumbani iwapo wewe ni mgonjwa.
  • Vaa barakoa na ukaeumbali wa futi sita (mita mbili) mbali na wengine ukienda katika maeneo yaliyo na umati wa watu.
  • Epukana na umati na maeneo yenye mzunguko duni wa hewa.
  • Nawa mikono yako sikuzote au tumia kieuzi cha mkono.
  • Funika kikohozi na chafya zako kwa kisugudi chako au shashi.
  • Usiguse uso, mdomo, pua au macho yako.
  • Safisha sehemu katika nyumba yako.
  • Ukiwa na dalili za COVID-19, mwone mhudumu wako wa afya.
Tembelea maduka na maeneo ya umma salama zaidi

Kuna mambo mengi ya kukumbuka ili kujilinda na kulinda wengine kabla ya na baada ya kwenda nje ukiwa mbali na nyumbani.

Kabla ya kuondoka:

  • Kadri inavyowezekana, usiende kwenye duka au mahali pa umma iwapo wewe ni mgonjwa. Acha mtu wa familia au rafiki akuchukulie bidhaa.
  • Zingatia kuagiza mboga, dawa, na bidhaa nyingine mtandaoni ili uweze kuletewa nyumbani mwako.
  • Zingatia kwenda kwenye duka wakati ambao hakuna watu wengi, ikiwezekana.
  • Nawa mikono yako kabla ya kuondoka nyumbani.

Ukiwa ndani ya nyumba penye watu wengi:

  • Vaa barakoa inayofunika pua na mdomo wako.
  • Kaa angalau umbali wa futi sita (mita mbili) kati yako na wengine, ikiwa pamoja na katika foleni ya kulipa.
  • Jifunike ukikohoa au kupiga chafya.
  • Usiguse uso wako.
  • Ukiwa umeenda nje kufanya manunuzi, tumia kieuzi cha mkono au vitambaa vyenye kiua viini ili kusafisha mkono wa toroli yako au mkoba wa ununuzi.

Unaporudi nyumbani:

  • Osha kitambaa hicho cha kufunika uso na ukihifadhi vizuri. Tupa barakoa yako ya kutupwa.
  • Nawa mikono yako.
  • Tumia matendo ya usalama wa chakula. Usieue bidhaa za chakua. Osha matunda mboga kama kawaida.
Ujauzito, watoto na COVID-19

Unachofaa kujua iwapo wewe ni mjamzito

  • Wajawazito au waliokuwa wajawazito hivi karibuni wapo katika hatari ya juu ya maradhi makali ya COVID-19 wakilinganishwa na watu ambao si wajawazito.
  • Watu wanaoambukizwa COVID-19 wakati wa ujauzito pia wapo katika hatari ya juu ya kuzaa mtoto kabla ya muda (kuzaa kabla ya kufikisha wiki 37) na kuzaa mtoto aliyekufa, na wanaweza kuwa katika hatari ya juu ya matatizo mengine ya ujauzito.
  • Watu ambao ni wajawazito au walikuwa wajawazito hivi karibuni na watu wanaogusana nao wanafaa kuchukua hatua hizi ili kusaidia kujilinda dhidi ya kusambaza COVID-19:
    • Pokea chanjo na upokee dozi mbili za busta.
    • Vaa barakoa.
    • Kaa futi sita mbali na wengine, na kuepuka umati na maeneo yenye mzunguko duni wa hewa.
    • Pata kupimwa ili kuepuka kusambaza ugonjwa huo kwa watu wengine.
    • Nawa mikono yako mara kwa mara na ufunike kikohozi na chafya zako kwa kisugudi chako au shashi.
    • Safisha na kuua viini nyumbani mwako mara kwa mara.
    • Angalia afya yako kila siku.
    • Wapigie mhudumu wao wa afya mara moja iwapo wana ujauzito wowote kuhusu ujauzito wao, wakiwa wagonjwa, au wakidhani kuwa huenda wameambukizwa COVID-19.

Ujauzito na chanjo ya COVID-19

  • Chanjo ya COVID-19 inapendekezwa kwa watu ambao ni wajawazito, wanaonyonyesha, wanaojaribu kuwa wajawazito, au wanaoweza kuwa wajawazito katika siku zijazo.
  • Ushahidi kuhusu usalama na ufanisi wa chanjo ya COVID-19 wakati wa ujauzito unaongezeka. Data inapendekeza kuwa manufaa ya kupokea chanjo ya COVID-19 yanashinda hatari yoyote ya chanjo inayojulikana au inayoweza kutokea wakati wa ujauzito.
  • Watu wajawazito wanafaa kupokea dozi ya busta ya chanjo ya COVID-19 wanapostahiki.
  • Chanjo za COVID-19 hazisababishi maambukizo ya COVID-19, hata katika watu ambao ni wajawazito au watoto wao.
  • Kwa sasa hakuna ushahidi kuwa chanjo zozote, zikiwemo chanjo za COVID-19, husababisha matatizo ya nguvu za uzazi kwa wanawake au wanaume.
  • Je, wewe ni mjamzito na una maswali zaidi kuhusu chanjo ya COVID-19? Ongea na mhudumu wako wa afya au wasiliana wa MotherToBaby, ambao wataalamu wao wanapatikana ili kuyajibu maswali yako kwa simu au gumzo. Huduma hii ya bila malipo ya usiri inapatikana Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 2 asubuhi hadi 11 jioni. Tembelea MotherToBaby (Kiingereza na Kihispania pekee) ili kupiga gumzo moja kwa moja au tuma barua pepe, au piga 1-866-626-6847 (inapatikana tu katika Kiingereza na Kihispania).

Jinsi ya kumtunza mtoto aliyezaliwa iwapo wana COVID-19

  • Watoto wachanga wengi waliozaliwa na watu ambao wameambukizwa COVID-19 wakati wa ujauzito huwa hawana COVID-19 wakati wa kuzaliwa.
  • Watoto wachanga wengi waliopatikana na maambukizo ya COVID-19 walikuwa na dalili kidogo au bila dalili na walipona. Ripoti zinajumuisha kuwa watoto wengine waliozaliwa walikuwa na maradhi makali ya COVID-19.
  • Iwapo umejitenga kwa sababu ya COVID-19 na una mtoto mchanga, fuatilia tahadhari zifuatazo hadi wakati ambapo kipindi chako cha kujitenga kitaisha:
    • Kaa nyumbani ili kujitenga na wengine ambao hawaishi na wewe.
    • Jitenge (kaa mbali) na wanachama wengine wa kaya yako ambao hawajaambukizwa na uvae barakoa katika maeneo ya kushirikiwa.
    • Tafuta mtoaji huduma ya utunzaji wa afya ambaye amepokea chanjo kamili na hayuko katika hatari ya juu ya maradhi makali ili amtunze mtoto wako mchanga. Iwapo inawezekana, ondoa maziwa yako ya mama ili mtoaji huduma mwingine aweze kumpa mtoto wako. Iwapo unampatia maziwa ya duka, mwombe mtoaji huduma ya utunzaji ayaandae.
    • Fuata tahadhari zilizopendekezwa iwapo unahitaji kumtunza mtoto wako mchanga kabla ya kipindi cha kujitenga kuisha, ikiwemo kuvaa barakoa wakati wa kumlisha au kumbeba mtoto wako.
    • Mfuatilie mtoto wako mchanga iwapo ana dalili za COVID-19.
  • Ushahidi wa sasa unapendekeza kuwa maziwa ya mama hayana uwezekano wa kusambaza virusi kwa watoto. Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa watu ambao wamepokea chanjo ya COVID-19 huhamisha kingamwili za kinga kwa mtoto wao kupitia maziwa ya mama. Iwapo una COVID-19 na umeamua kunyonyesha au unanyonyesha:
    • Nawa mikono yako kabla ya kumhudia mtoto.
    • Vaa barakoa unapombeba au unaponyonyesha na wakati wowote ambao upo ndani ya futi sita (mita mbili) ya mtoto wako.

Laini ya Perinatal Support Washington inapatikana kwa wazazi wote wapya na wanaotarajia, au wapendwa wao, wakati wowote wanapohitaji taarifa na usaidizi wa afya ya kiakili. Piga simu kwa Laini ya Perinatal Support Washington kupitia 1-888-404-7763 au tembelea tovuti ya Perinatal Support website (Kiingereza pekee). Tuma ujumbe au barua pepe kwa warmline@perinatalsupport.org.

Ni muhimu kupata usaidizi. Laini hiyo inajibiwa hewani Jumatatu hadi Ijumaa saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:30 jioni. (Katika Kiingereza na Kihispania pekee). Jioni na wikendi tafadhali tuma ujumbe na mtu atakupigia simu ndani ya saa 1-12. Laini yetu inahudumiwa na wafanyakazi wa jamii, wataalamu wa tiba walio na leseni, au wazazi waliopitia mfadhaiko wa baada ya kuzaa na kiwewe.

Jitunze na utunze familia yako

Washington Listens: Iwapo unahitaji kuongea na mtu kuhusu msongo wa mawazo wa COVID-19, piga simu kwa Washington Listens kupitia 1-833-681-0211. Huwa kuna mtu wa kuongea naye kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 3:00 usiku na wikendi kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni. TTY na huduma za kufikia lugha zinapatikana. Maelezo zaidi yanapatikana kwenye ukurasa wetu wa Afya ya Kiakili na Ustahi wa Kihisia (Kiingereza pekee).

  • Pata habari ya kutosha ya hali ya kisasa ya janga na mapendekezo ya ziada yaliyo na taarifa ya kutegemewa kutoka vyombo vya habari vya kuaminiwa, mashirika ya afya ya umma na ndani, na visasisho kutoka tovuti za afya ya umma.
  • Unda orodha ya rasilimali ya jamii, kama vile nambari za simu, tovuti na akaunti za mtandao wa kijamii. Unaweza kuongeza shule, madaktari, mashirika ya afya ya umma, huduma za kijamii, vituo vya jamii vya afya ya kiakili na nambari za simu za dharura.
  • Endelea kuwasiliana na wanafamilia na marafiki kwa simu au kupitia huduma za kijamii.
  • Kuwa na vifaa vya kimsingi vya afya (kama vile sabuni, kieuzi cha mkono cha alkoholi, shashi, kipimajoto, dawa za kupunguza joto kali, na vifaa vya kujipima COVID-19 nyumbani) vilivyopo.
  • Jaribu kuwa na usambazaji wa dawa ambazo wewe au wanafamilia wako hutumia kila mara.

Usaidizi wa wanafamilia wako wadogo

  • Tafuta usaidizi na muunganisho unaoendelea kutoka kwa marafiki na familia kwa kuongea na wao kupitia simu, ujumbe, barua pepe, au mtandao wa kijamii.
  • Iwapo habari hiyo inawafadhaisha watoto wako, usisahau kuchukua muda wa mapumziko. Ongea na wao ili kufafanua taarifa yoyote ambayo wanaweza kupata kwenye Intaneti au vyanzo vingine vya taarifa.
  • Lenga kuwasaidia watoto kwa kuwahimiza kuuliza maswali na kuwasaidia kufahamu hali ya sasa.
  • Ongea kuhusu hisia ulizo nazo na uzitambue.
  • Wasaidie kuelezea hisia zao kupitia michoro au shughuli nyingine.
  • Toa starehe na uvumilivu kiasi zaidi ya kawaida.