Swahili

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Kwa Nini Upimwe

Kipimo kinaokoa maisha. Kipimo huwaruhusu watu kutahadhari, kama kukaa karantini, kwa wakati unaofaa ili kusimamisha kuenea kwa virusi; watu walioambukizwa bila dalili bado wanaweza kusambaza virusi. Kipimo pia husaidia maafisa wa afya ya umma kutambua na kukabiliana na mkurupuko, na kufuatilia aina mpya za virusi. Kipimo ni kijenzi muhimu katika kusaidia kurejea shughuli za kawaida.

Watafiti kutoka University of Washington na Department of Health (DOH, Idara ya Afya) waligundua kuwa kupima COVID-19 na kufuatilia kupitia WA Notify (Arifu WA) huenda ilizuia takriban visa 6,000 kutoka Desemba 2020 hadi Machi 2021.

Wakati wa Kupimwa

Enda upimwe iwapo una dalili za COVID-19 au umekuwa na mgusano wa karibu na mtu ambaye huenda ameambukizwa COVID-19. Unafaa kupimwa mara moja iwapo una dalili, au siku 3-5 baada ya mfiduo unaoshuku, hata kama huna dalili zozote.

Mahali pa Kupimwa

Tovuti ya Department of Health Jimbo la WA ina orodha ya vituo vya kipimo (katika Kiingereza) inayopatikana katika kila kaunti, na saa za kufanya kazi pamoja na mahitaji. Kwa maelezo zaidi kuhusu vituo vya kipimo, piga 2-1-1. Vifaa vya kipimo vya kununuliwa dukani pia vinapatikana kwa kuagiza na katika famasia kwa urahisi, katika kipimo cha nyumbani.

Tafuta Eneo la Kipimo Karibu Nami (katika Kiingereza)

Aina za Vipimo

Vipimo vya sasa vinavyopatikana ni vipimo vya haraka vya antijeni, vipimo vya molekuli (vya maabara na eneo la utunzaji), na vipimo vya kujipima nyumbani. Usambazaji wa kipimo chochote maalum unatofautiana kulingana na mahitaji na uwezo wa mtengenezaji.

Gharama

Hakuna gharama zozote za kujilipia mwenyewe kwa vipimo vinavyofanywa katika kaunti au vituo vya kipimo vinafosaidiwa na jimbo. Vipimo vingi, hasa vya watu wanaopitia dalili, vinaweza kugharamiwa na bima au kupunguzwa na Department of Health. Vituo vya kipimo vinavyotoza ada ya huduma vimeonyeshwa kwenye orodha ya vituo. Vipimo vingi vya kusafiri havisimamiwi na bima au mipango inayofadhiliwa na jimbo.

Jinsi Ambavyo Kipimo Hufanya Kazi

Vipimo vingi vinafanywa kutumia pamba za pua. Baadhi ya vipimo vinaweza kufanywa kwa kukusanya mate. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana kwenye ukurasa wa maswali yanayoulizwa mara kwa mara kuhusu kipimo.

Ufuatiliaji

Kaa nyumbani kadri uwezavyo iwapo inawezekana iwapo una dalili. Ukipatikana na maambukizo, kaa karantini (kulingana na miongozo ya DOH/ Ceneter for Disease Control and Prevention (CDC, Vituo vya Uzuiaji na Udhibiti wa Magonjwa) nakutafuta usaidizi kupitia Care Connect.