Walioambukizwa COVID-19

Ukiambukizwa COVID-19, habari nzuri ni kuwa kuna hatua unazoweza kuchukua ili kusaidia kujilinda na kuwalinda wengine.

Jambo la kufanya iwapo utaambukizwa

Kaa nyumbani na mbali na wengine. Fuata mwongozo wa hivi karibuni zaidi wa kujitenga (Kiingereza pekee) kutoka Centers for Disease Control and Prevention (CDC, Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Ugonjwa) na Washington State Department of Health (DOH, Idara ya Afya ya Jimbo la Washington). Iwapo unahitaji msaada wakati wa kujitenga, huenda ukaweza kupata msaada kutoka Care Connect Washington.

  • Jitenge na wengine nyumbani mwako. Iwapo unaweza, kaa katika chumba tofauti mbali na watu wengine unaoishi na wao na utumie choo na bafu tofauti.

Fuatilia dalili zako. Dalili zako zikiwa mbaya, au ukiwa na dalili mpya zinazokutia wasiwasi, wasiliana na mhudumu wako wa afya. Piga 9-1-1 iwapo utagundua yoyote kati ya dalili zifuatazo za onyo la dharura za COVID-19:

  • Tatizo la kupumua
  • Maumivu ya mara kwa mara ya kifua au shinikizo
  • Kuchanganyikiwa kwa ghafla
  • Ukosefu wa uwezo wa kujibu
  • Ngozi, midomo, au kucha zilizokwajuka, za rangi ya kahawia au buluu, kutegemea ulaini wa ngozi

Vaa barakoa inayofunika pua na mdomo wako iwapo unahitaji kuwa karibu na wengine, hata nyumbani. Watu wengine katika kaya yako wanafaa kuvaa barakoa, pia.

Waarifu wengine ili kutosambaza ugonjwa. Wasiliana na waasiliani wako wa karibu (katika Kiingereza) na kuwafahamisha kuwa huenda wameambukizwa COVID-19. Mtu ambaye ameambukizwa anaweza kusambaza COVID-19 hata kabla ya kuwa na dalili. Ukiwaarifu waasiliani wako wa karibu, wanaweza kupimwa na kukaa karantini au kujitenga iwapo inahitajika ili kuepuka kusambaza virusi kwa wengine.

  • Iwapo ulitumia kipimo cha kujipima mwenyewe nyumbani, ripoti matokeo yako yanayoonyesha umeambukizwa kwa nambari ya simu ya COVID-19 katika Washington kupitia 1–800–525–0127. Hii inasaidia juhudi za kufuatilia mwasiliani (katika Kiingereza) na kuzuia ugonjwa dhidi ya kuenea zaidi katika jamii zetu. Nambari hiyo ya simu inapatikana Jumatatu kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku, na Jumanne hadi Jumapili (na sikukuu) kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni. Usaidizi wa lugha unapatikana.
  • Iwapo ulitumia kipimo cha nyumbani, omba msimbo wa uthibitisho kupitia WA Notify (Arifu WA) ili kuwaarifu watumiaji wengine wa WA Notify ambao huenda wana mfiduo.

Wasiliana na mhudumu wako wa afya - iwapo una mmoja - au kliniki ya ndani ya afya ili kupata ushauri wa matibabu. Wanaweza kukupatia vidokezo vingine vya jinsi ya kukaa sawa unapopata nafuu. Pia watakuambia kuhusu dalili za maradhi makali za kufuatilia, ili uweze kupata utunzaji wa ziada iwapo unauhitaji.

Hakikisha kuna mzunguko wa hewa wa kutosha kadri uwezavyo. Iwapo inawezekana, fungua madirisha, tumia kiyoyozi cha kasi ya juu, badilisha kichujio chako cha HVAC, au tumia kichuja hewa cha HEPA.

Hata kama umepona COVID-19 na unaweza kutamatisha kipindi chako cha kujitenga, ni muhimu kuendelea kujilinda na kuwalinda wengine. Unaweza kufanya hii kwa kupata chanjo yako ya COVID-19 na dozi ya kiongeza nguvu, kuvaa barakoa yako kwa umma, kuepuka umati mkubwa, kunawa mikono yako, na kuwezesha WA Notify kwenye simu yako mahiri.